elmagnifico
JF-Expert Member
- Jul 7, 2011
- 8,261
- 9,732
Jana mida ya saa nane usiku nilikuwa nimesimama sehemu moja pale kunduch mtongani, ambapo kuna vijana wanauza chips usiku.
Pembeni yangu nilikuta kuna noah na landcruiser yenye namba za STL.
Mwenye noah akawa anamwambia mwenye cruiser umewasha taa full then waendesha gari upande usio wa kwako we vipi wewe.
Yule dereva wa cruiser akamjibu hii serikali, mwenye noah akamjbu hata kama serikali lazima kufuata sheria.
Jamaa wa noah akaondoa gari akaondoka, mara ghafla ile cruiser ikachomoka speed ikamfuata nyuma na kumblock kwa mbele kumbe ilikuwa ina polis wakatoka na bunduk wakamchomoa kwenye gari.
Pale mtongani pia kuna kituo cha askari sasa sijui walipiga simu kituoni likaja gari lingine la askari wakajumuika na wale wa awali na bunduki wakaanza mzingua jamaa wakamteremsha wakaanza pekua gari.
Niliondoka bila kujua mwisho wake.
Ila nikabaki najiuliza hivi polisi wa Tanzania wanaweza kuwa rafiki kwa jamii kweli maana kwa wenzetu polisi wako friendly kwa jamii kuliko hawa wa kwetu wanatumia sana mabavu hata ambapo wamekosea.