Jana nimeufuatilia mtanange kati ya timu ya Simba dhidi ya Singida Fountain Gate kombe la Mapinduzi 2024. Uonevu wa refa dhidi ya timu ya Singida unatakiwa kukemewa kwa kiasi kikubwa. Sababu zangu kuhusu uonevu huo ni kama ifuatavyo:-
(1) Baada ya muda wa dakika 90 kuisha refa aliongeza dakika 8 lakini hizi dakika za nyongeza mpira ulichezwa kwa muda wa dakika 11 bila Refa kupuliza kipenga cha kumaliza mpira.
(2) Kona ulioruhusiwa na Refa mpira ulikamatwa na kipa nje ya mstari na hakuna mchezaji wa Singida aliyeupiga mpira huo nje na kipa akaukamata nje ya mstari ni dhahiri mpira huo haukustahili kuwa kona. Huo mpira ulitakiwa upigwe kuelekeza kwa timu pinzani ya Simba.
(3) Huu ni ushauri kwa Timu ya Singida. Wakati wa kupiga penati mnaombwa kuchagua wachezaji maakini. Ile penati aliyopiga Kagere ilikuwa ni penati ya hovyo ambayo haijapa kutokea katika historia ya mpira. Jifunzeni kupiga penati.