Uonevu toka Singita Grumeti Reserve

Uonevu toka Singita Grumeti Reserve

makamaka

Member
Joined
Dec 1, 2011
Posts
55
Reaction score
28
BARUA YA WAZI KWA MHE RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA KUHUSU WATANZANIA KUFUNGIWA LOCKDOWN NDANI YA TAIFA LAO KATIKA PORI LA AKIBA LA IKORONGO CHINI YA MWEKEZAJI SINGITA GRUMETI RESERVE

Awali ya yote Mhe Rais tunakupa pole kutokana na majukumu mazito uliyo nayo na hongera sana kwa jitihada zako katika kuijenga nchi yetu na kuhakikisha tunakuwa na taifa huru lenye uchumi imara na raia wasionyanyasika katika nchi yao. Kwa masikitiko makubwa sisi wafanyakazi wa kampuni ya Singita Grumeti Reserve Ltd tuna penda kukujulisha kuwa tumewekwa LOCKDOWN ndani ya nchi yetu tokea Mwezi March 2020 katika pori la akiba la Ikorongo, Wilaya ya Serengeti, Mkoani Mara.

Isitoshe baada ya wewe Mhe Rais na Amiri Jeshi Mkuu kutoa amri ya kuondoa LOCKDOWN na shughuli za kazi ziendelee kama kawaida uongozi wa Singita Grumeti Reserve umeendelea kutufungia quarantine mpaka hivi sasa tunapo andika ujumbe huu kwako. Mhe Raisi tokea mwezi Machi tunalipwa nusu ya mshahara (50%) bila ya makubaliano baina ya mwajiri na wafanyakazi kwa kisingizo cha CORONA. Na zoezi husika limekuwa likisimamiwa na Afisa Rasilimali watu (HR) ambaye ni Raia wa Kenya Bi. Martha Baare, huyu amekuwa kinara wa kutunyanyasa na kutoa maneno machafu kwa wafanyakazi wazawa na amekuwa akiishauri kampuni kuajiri wafanyakazi wa kigeni.

Ukiachilia mbali zoezi husika, Mwekezaji ambaye ndiye mwenye kampuni Bwana Paul Tudol Jones ambaye ni raia wa taifa la Marekani alishasema tusiondolewe na nakala ya barua ya maelekezo husika tunayo wafanyakazi. Tumeshalalamika kuhusu hili suala kwa wasaidizi wako ambapo Waziri wa Maliasisili na Utalii Mhe. Kigwangala na Naibu Waziri wa Kazi Ajira na Vijana Mhe Anthony Mavunde wamefika hapa na hakuna chochote kilicho chukuliwa hatua.

Hatusemi kama wamehongwa lakini kampuni hii ni kinara kwa kuhonga viongozi waandamizi wa serikali na pia kuna maneno anayotoa huyu Afisa Rasimali watu kuwa hakuna waziri anayeweza kubadilisha suala lolote hili hapa. Pia Mhe Raisi hapa kuna raia wa kigeni wana lipwa maelfu ya dola ili hali hawana vibali vya kufanya kazi hapa nchini. Na hata nafasi husika wanazofanya kazi siyo kwamba hakuna watanzania wenye sifa.

Hawa wamekuwa wakifanya pasipo vibali na wanatumia visa za kitalii na hata ukiangalia taarifa za uhamiaji utaliona hili. Baadhi yao ni; George Tolchard, Emma Wilson, Terry Wade na wengine wengi. Sie tunakatwa fedha zetu ili kulipa malipo ya hawa raia wa kigeni. Pia chama chetu cha wafanyakazi CHODAWU badala kuwa msaada kwetu sie wafanya kazi kimekuwa ni kinara wa kutukandamiza na wamekuwa wakitukana hela kwenye mishahara yetu kila kukicha.

Tunavyo andika barua hii leo Tarehe 17th Julai 2020, huyu Afisa Rasilimali watu Raia wa Kenya anaushawishi uongozi utufukuze kazi ilihali Mwekezaji kupitia kwa bwana Luke Belle walituambia kwa barua dhamira yao ya sie kuendelea kufanya kazi katika kipindi hichi cha CORONA. Na tayari wameshaanza kuandaa barua ambazo wanataka watukabizi wakati wowote ule ili tuondoke pasipo kulipwa stahiki zetu.

Na hili wanalifanya kwa haraka kabla ya Mwekezaji mwenye kampuni Bwana Paul Jones kuwasilini Nchini Tarehe 2 Agosti 2020. Hivyo Mhe Raisi tunaomba msaada wako kwanza tuondolewe quarantine lakini kama wamenuia kutufukuza kazi basi watulipe stahiki zetu kwa mujibu wa mikataba yetu na kuzngatia sharia za nchi. Mwisho kabisa tunakuomba Mhe Raisi uitazame kwa kina hii kampuni ya Singita Grumeti Reserve jinsi inayo endeshwa kuna ukiukwaji mkubwa sana wa sheria kwenye masuala mengi.

Mhe Rais wewe kwa sasa ndiyo mwokozi wetu tunaye kutegemea na sie tupo tayari kutoa ushirikiano kwa serikali ili kuhakikisha ili suala lina kwisha salama pasipo kuathiri shughuri za uwekezaji na soko la utalii kwa ujumla.

SISI WAFANYAKAZI WA SINGITA GRUMETI RESERVE TULIOKO LOCKDOWN!
 
Kwanza pole na poleni nyote. Matumaini jamii forum ni pana sana. Ujumbe adhimu kama huu naamini utafanyiwa kazi.
Jisimamie na ongeza umakini kwa kipindi hiki.
 
Hiyo Singita nimeisikia sana kuhusu unyanyasaji wa raia hapo kupitia huyo Mkenya sema kazi ipo hapo nadhani maswala yenu yataishia mahakamani hao jamaa wanajiamini mno kama wao ndio kila kitu ngoja tuone hii movie itaishaje maana Sterling yupo sawa kama wale wa No retreat no surrender.
 
Yaonekana mmiliki ni kigogo mkubwa aliyestaafu ndio maana hatua hazichukuliwi.
 
Kwa kipindi hiki cha Corona biashara zilivyo ngumu mshukuruni Mungu nyie mnapata hata hiyo 50%, kuna watu hawapati chochote, biashara ngumu, na wengine wamepunguzwa kazi kabisa!

Watanzania tujifunze sana kuendana na mazingira na hali ya kibiashara inavyoenda!

Serikali inataarifa jinsi sekta mbalimbali haswa binafsi zilivyoadhirika haswa sekta ya utalii! Hamna wageni wanaoingia nchini kabisa! Mapato hata kwa serikali yenyewe kwa sekta ya utalii yamepungua sana. So usitegemee kupata usaidizi wowote maana kila kitu kipo wazi.

Mshukurini sana Mungu kwa kidogo mnachopokea kwa ajili ya kuendeleza familia na maisha yenu kipindi hiki. Ikitokea mkapunguzwa na mkapewa stahiki zenu mtaikumbuka hiyo kazi!

Nawashaurini badala ya kutengeneza mgogoro na mwajiri muombeni angalau hali ikishakuwa sawa kama anaweza kufidia hiyo 50% ya mishahara iliyobakia kwa miezi ambayo hamkupata full salary.
 
Yani sekta ya utalii mnapata 50% kila bado mnalia lia. Hio ni sekta ambayo kiuhalisi imekufa kabisa. TRA na serikali wanalijua hili. Kwa sababu wanaona mapato yalivyokata ghafla.
 
Back
Top Bottom