KOLOKOLONI
JF-Expert Member
- Mar 7, 2014
- 2,476
- 2,375
Pole sana Mwanajamiiforums kwa uchungu ulioupata juu ya habari ya kusikia .Wananchi wa Ubungo wanadai kumekuwa na Uonevu unaopitiliza kwa raia wasio na hatia kuwekwa mahabusu kwa amri ya OCD Kiluvia Gogoni (wilaya ya Ubungo) kwa muda mrefu.
Tunaomba RPC, Mkuu wa Wilaya/Mkoa na Waziri Lugola aingilie kati suala hili maana wananchi wamekuwa kama wako Somalia wanateswa sana na huyu OCD anayedaiwa kuwa mla rushwa na mwizi.
Inadaiwa wanawekwa mahabusu kwa makosa ya kutengeneza na hawapelekwi Mahakamani, na wengine wameshakaa mpaka miezi 3 bila kujua kosa lao nini
Mamlaka husika na watu wenye mapenzi mema, tunaomba mfuatilieni huyu OCD maana amekuwa na kiburi kinachopitiliza ambapo inafika mahali inadaiwa hata Askari wa Kituo chake wanaswekwa ndani kwa maagizo yake inapotokea kutofautiana kwenye madili yake ya Rushwa.
Ni sauti ya Mtu aliaye Nyikani, tusaidiane tujenge jamii iliyostaarabika na Jeshi la Polisi lenye weledi na ufanisi
OCD Maana yake ni Mkuu wa Police Wilaya(Officer Commanding District) kwa Cheo anakuwa na Mwenge na Nyota moja au Mwenge peke yake na umbo la huo Mwenge linataka kufanana na ile nembo ya Bibi na Bwana. Yaani Senior Superintendent au Superintendent. (SSP au SP) .
OCD ni Mtu anayeshughulika zaidi na mambo ya Utawala wa Polisi katika Wilaya.
MTU anayeshughulika kudhibiti Hualifu moja kwa moja ni OC CID yaani Officer Commanding Criminal Investigation Department kwa kimara niliwahi kwenda mwezi uliopita nikiwa na mjanga yangu yule mkuu wa upelelezi Katika Wilaya hiyo ni Mchungaji wa kanisa la wasabato hivyo kumjumlisha kwenye rushwa moja kwa moja napata tabu.
Hao watu wawili niliowataja kwa kawaida wote wana Mwenge mabegani na wanapishana nyota Moja na mkubwa anakuwa Ocd ila Huyo oc cid havai sare kwakuwa ni mpelelezi.
Mtu unayemtaja wewe kuwa ni OCD ni dhahiri kuwa siyo OCD kwakuwa umesema anazo nyota mbili hivyo hana sifa ya kuongoza Wilaya.
Watu wenye nyota mbili na wanafanya kazi kwa level ya Wilaya wanaitwa Operation Officers katika wilaya hawa wanaongoza vile vikosi vinavyofika eneo la tukio haraka na wanavaa sare kama FFU ila kofia zao nyeusi au wanava cap (Crime Response Team CRT) hawa mambo yao yanapishana kidogo sana na FFU maana wazee wa mkong'oto na kupambana na majambazi uso kwa uso pia kudhibiti vibaka kila kichochoro. Hivyo kwa mujibu wa malalamiko yako inawezekana unamlaumu Operation Officer katika Wilaya siyo OCD maana OCD hausiki na kusaka vibaka kila kona na operesheni za kila siku maana jukumu hilo kashapangiwa mtu wa Nyota moja au mbili.
Nikinukuu malalamiko yako inaonesha kuwa wewe hujatendewa ubaya wowote ule isipokuwa umesikia tu hivyo malalamiko yako ni majungu yasiyokuwa na ushaidi.
Swala la huyo unayemtaja kuweka Mahabusu watumishi wenzake ni kwamba hayo ni mambo yao ya ndani na kudhibiti nidhamu zao pia tukumbuke Polisi ni sehemu ya jamii wanaweza kutenda uhalifu hivyo kuona askari wapo mahabusu inawezekana wanatuhuma ndani ya kazi au jinai. Kwakuwa ushaidi wa maneno yako yote ni wa Hearsay hivyo taarifa yako inaonekana ni Majungu tupu hakuna ukweli wowote.
KIMARA KWA SASA CRIMES ZA BUNDUKI NA UVUNJAJI ZIMEPUNGUA SANA HIVYO INAWEZEKANA UNAYEMLALAMIKIA KISU CHAKE KIMEGUSA MFUPA WAKO .POLE KWA KUTOA MALALAMIKO YENYE MAJUNGU AMBAYO USHAIDI WAKE DHAIFU MNO.NAPENDEKEZA CHUNGUZA TENA UJE NA DATA KAMILI ILI TUJUE NANI NI TATIZO ILI ALIPULIWE .