bachelor sugu
JF-Expert Member
- Jan 30, 2018
- 2,689
- 3,641
Habari za mchana Wakuu,
Ama kwa kweli nchi yetu tumefilisika kila kitu yaani kuanzia viongozi,skills za uongozi,pesa,hadi roho za huruma nazo tumefilisika zaidi kwa hawa viongoz/watawala wetu.
Kuna operation inayoendeshwa na jeshi la polisi hapa wilayani Kilosa ya kukamata pikipiki na pale unapobainika kuwa na kosa lolote basi kwanza unatulizwa mahabusu kisha taratibu za kupelekwa mahakamani zinafuata.
Kibaya zaidi hata ukiwa na kosa moja FAINI YAKE ni shilingi za Kitanzania 300,000/=(Laki Tatu tu) na ukiwa na makosa yote bei ni hiyo hiyo.Uonevu huo unaenda mbali zaidi kuwa ukiweza kulipa faini hiyo unahukumiwa MWEZI MMOJA JELA na ukishindwa unahukumiwa MIEZI SABA(7) JELA.
Hali imekuwa mbaya zaidi kwani mahabusu ya Polisi imejaa,Mahabusu ya Gereza imejaa mpaka wengine sasa hv wanahamishiwa Mahabusu zilizopo ktk vituo vingine vya Polisi vya wilaya hii.
Hv kweli nchi imekosa vyanzo vingine vya mapato mpaka kufikia sasa kuamua kuwa wanyang'anyi wa jasho la wananchi wake??,Lengo hasa ni nini kuwarudisha vijana wetu katika kazi zile haramu za kukaba na wizi?
Kwani watanzania tumemkosea nini huyu mtawala wetu ambaye tunaamini AMRI hizi zote ni kutoka kwake???
Dah hali ni mbaya kwa kweli jamani na tunakoelekea tusije hata siku moja kupoteza muda kumtafuta mchawi wetu maana uvumilivu nao una mwisho.
Ee M/Mungu tutupie jicho lako la huruma watanzania tunaangamia.