Uoga unavyotutesa

Uoga unavyotutesa

Joined
Nov 2, 2020
Posts
68
Reaction score
90
Kimaisha kila kitu huwa kinatakiwa kuwa kati kwa kati ,Yaani kisizidi au kisipungue sana.

Mfano kula ukavimbewa ni tabu japokuwa kula ni lazima.Sawa na matendo mengine kama kucheka,kulia ,kutabasamu au hata kukasirika.

Uoga ni moja ya hali ambayo umpata kila mmoja wetu,Lakini kwa wengine hupitia hali hii inayopitiliza ambayo mwisho wa siku hujikuta ikigeuka kuwa ni hatari kwa manufaa ya afya ya mwili na akili.

Ijapokuwa si dhambi mtu kuogopa,Kwani wakati mwingine uoga utusaidia katika kung'amua viashiria vya matatizo na kuchukua hatua stahiki.

Kuna wakati mtu hushindwa kufanya maamuzi kuhusu maisha yake,Ikiwa ni pamoja na kuamua kutulia na mwenzi mmoja kupitia ndoa halali.

Kwa uzoefu mdogo nilionao,Baadhi ya vijana hushindwa kupima afya zao kwa magonjwa kama UKIMWI na mfano wake kabla ya ndoa ,Kwa kujiogopesha tu kuwa huenda ameathirika ,na mwisho wa siku hubaki akijifariji kuwa haina ulazima wa kupima.

Kwa kiasi kikubwa hali hii unaweza kuona unajisaidia ,Lakini kiuhalisia unajiumiza kiakili.

Najua tuko wengi ambao tunakumbwa na hali kama hii,na pengine tunashindwa jua nini cha kufanya,Ila moja ya njia ya kuendea tiba ya tatizo hili ni kuamua kuzungumza na mtu unayemuamini na kumueleza kwa kiasi gani linakusumbua na ungependa akusaidie nini.

Bado hujachelewa ,Anza leo safari yako ya kuendelea kutafuta uhuru wa fikra na akili yako.

Youth Worker

Hardness, Teaches
 
Back
Top Bottom