Unyapara na umangimeza kwa rasilimali za watanzania ufike kikomo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Unyapara na umangimeza kwa rasilimali za watanzania ufike kikomo

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by sammosses, Sep 18, 2012.

 1. sammosses

  sammosses JF-Expert Member

  #1
  Sep 18, 2012
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 1,205
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Tanzania nchi iliyoko dunia ya tatu yenye utajiri mkubwa wa rasilimali lakini ikiwa ni miongoni mwa nchi tatu sana kwa umaskini na kujizolea nafasi ya kwanza ya kuwa nchi omba omba(the begger nation).Ukiangalia rasilimali zetu na umasikini ulio kithiri ambao umewagubika wananchi wake unaweza kuuliza nani amewaroga Watanzania mpaka kufikia hapa tulipo.

  Wananchi wamechoshwa na kauli mbiu ambazo zimeshindwa kuwatatulia matatizo yao ya kiuchumi ilihali takwimu za kiuchumi zinaonyesha kwenye makaratasi umasikini umepunga kwa asilimia 2.1% lakini Watanzania wa leo wanaishi maisha ya kichovu na kukata tamaa.

  Wananchi wamechoshwa na hali iliyoko hapa nchini ya kila siku kupewa matumaini ilihali wachache wanajichotea keki ya taifa.

  Leo hii serikali yetu ya CCM inayoongozwa na JK inafanya kazi za kizimamoto kama vile serikali haina mpango kazi wa muda mfupi,muda wa kati na muda mrefu.Naibu waziri wa madini mh. Steven Maselle ametoa walaka kuonyesha ni jinsi gani nchi yetu inatafunwa na wajanja wachache waliojifanya ma mangimeza na manyapara wa rasilimali zetu.

  Inawezekanaje mgeni anaamua kuzalisha tu dhahabu na kujiamulia kutoa takwimu zisizo sahihi kwa minajili ya kukwepa ushuru na mapato mbali mbali ya serikali.Tunajiuliza waungwana wa nchii hii,hivi mpaka bwana mkubwa huyo anaamua kufanya atakavyo serikali ilikuwa wapi.Serikali yetu imekuwa ikiongeza pato la PAYE kwa waajiriwa wake nakuwatolea macho watumishi lakini kwenye rasilimali zinazoporwa na wavamizi (intruder) toka Ulaya wanaachiwa kufanya watakavyo.

  Niliwahi kuuliza huku siku za nyuma,kuwa nani hasa aliyewaroga Watanzania mpaka kufikia kuona kila kitu ni sawa bila kujali maslahi ya Watanzania,lakini mpaka leo sijapata jibu.Tumechoshwa na umangimeza na unyapara katika mali zetu unatoka wapi ilihali Watanzania walilelewa katika misingi ya kijamaa na kufanya kazi zao kijamii.

  Tumeona manyapara wengi waliokwisha kuletwa nchi kwetu kuiba hata kile ambacho tunajitahidi kukipigania kwa staili ya menejiment,tuliona Tanesco na tuliona Nuwa wkati ule na bado kuna sekta nyingi za umma ambazo manyapara hawa wa kigeni wanapelekwa kusimamia mali zetu kuibiwa.Ni lini basi tutajikomboa na kuamau kusimamia mali zetu wenyewe bila kuwa na napara toka ughaibuni?

  Bubu siku zote husema kwa uchungu wa mwana,uchungu umetugubika Watanzania,tusipokuwa makini nchi hii ipo siku tutaambiwa tumeuzwa .Tuamke sasa kudai haki zetu kama mabomu yanatosha kutukwamisha basi tutaona mbele ya safari

   
 2. sammosses

  sammosses JF-Expert Member

  #2
  Sep 19, 2012
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 1,205
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Haitoshi kuendelea na sifa za kijinga ambazo zinatuchosha sisi street,oh eti Tanzania kisiwa cha amani huku wachache wazawa kwa kushirikiana na wageni wana tumia hari zaidi,nguvu zaidi na kasi zaidi katika kuihujumu nchi yetu.Yaliyojiri huku Mwanza kwa waziri mkuu kuzomewa kwenye mkutano wa hadhara ni viashiria ambavyo vinaonyesha jinsi gani wananchi walivyoichoka serikali yao

  Watanzania wa leo hawatishiwi nyau kama alivyojaribu kufanya mh. mkuu wa mkoa wa Mwanza kuwa ana wajua wale wote waliokuwa wanazomea.Cha msingi si lazima tutimize miaka mitano ya uongozi,ni muda sasa wa serikali ya chama tawala kujipima na kuamua kukabidhi nchi bado mapema kwa kuwa tu wameshindwa kutekeleza wajibu wao.

  Kamwe tusitegemee mvinyo ule ule uliobadilishiwa chupa ukawa haleweshi,kilichobadilika pale ni mchezaji bali timu na jezi ni ile ile
   
Loading...