Unyanyasaji, uonevu,na uvunjaji wa haki za binadamu

Joined
Oct 1, 2013
Posts
3
Reaction score
0
Ningependa msaada wa forum na watu wote wenye account humu wanisaidie kufikisha taarifa hii sehemu husika hasa wizara ya mali asili na utalii, kilimo na mifugo, mambo ya ndani pamoja na kamati itakayo undwa kuchunguza uvunjaji wa haki za binadamu uliofanyika kwenye operation mbalimbali hapa nchini ikiwemo oparesheni tokomeza majangili.kumekuwepo na vitendo vingi vya ukiukwaji wa haki za binadamu kama kupigwa, kuteswa,kunyanyaswa na hata kuuawa kwa baadhi ya raia hapa nchini ambavyo vimefanya raia ambao hawajafikwa na masaibu haya kuziweka roho zao juu kwa kuwaza ni lini watapatwa na kilicho wapata wenzao.Raia ktk pande zote za nchi hii wanalia kwa kupiga mayowe lakini hakuna aliye bahatika kusikia sauti zao na kuwasaidia isipokuwa wanaohusika kusikia vilio vyao huwaeleza kwa maneno yaliyo jaa unafiki na uzandiki kushugulikia matatizo yao huku ukweli ndani ya roho zao ikiwa ni uhamasishaji wa kuendelea kutendeka kwa vitendo hivi.Nielekee kueleza moja kwa moja vitendo wanavyo fanyiwa wafugaji wa wilayani Geita,Bukombe,Chato,Biharamulo na maeneo mengine ya mikoa ya Kigoma na Kagera.Wafugaji wa maeneo haya wanateswa, wananyanyaswa, wanapigwa, wanazalilishwa, na hata wengine kuuawa pamoja na ng'ombe wao ambao ndio maisha yao wakipigwa risasi, hiki kitendo kimekuwa cha muda mrefu hasa katika wilaya ya Biharamulo ambapo ng'ombe wamekuwa wakipigwa risasi na askari gemu bila hata huruma hivi hii si vita ni nini? Siwezi kusema Tanzania ni nchi ya Amani huku raia Wake hawana Amani isipokuwa kituwalichonacho ni woga. Kuna raia ameuawa muleba lakini sijaona hatua sitahiki zilizo chukuliwa na selikari isipokuwa kuendelea kushikiliwa kwa mali za marehemu kwa kisingizio kuwa walizikuta katika hifadhi ya Taifa, hata kama ingekuwa hivyo ni halali kuuawa kwa raia huyu? EMMANUEL LUGILA umeuawa kwa kupigwa risasi lakini pia mifugo wako bado wanashikiriwa kwa sababu za uongo ambapo uchunguzi ukifanyika najua utakua ni mwanzo wa kuumbuka kwao kwahiyo ukweli uko nyuma yako unambio ya kasi. Ndugu wananchi raisi wetu anahubiri Amani ktk nchi za wenzetu akisahau kuwa raia wa nchi yake hawana AMANI. Watendaji wa raisi wote wanao husika inapaswa kuwajibishwa kwa sababu ya kupoteza sifa za nchi hii zilizo achwa na waasisi wa Taifa hili wanazo zipoteza kwa kasi ya ajabu (kisiwa cha Amani). Kuna baadhi ya majina ya watu waliofanyiwa vitendo hivi ambayo ni: safari John ng'ombe 20, Nzera Kafugunya ng'ombe 30, Jeni Mpondi ng'ombe 40, Juma Kasong'hwe 12, Tebu Kafugunya 26, Doto Mabuga 41, Lumwaga kubelaho 17, Erick Antony 15, paul kefu 06, Nshimo 08, Maziku 60(bukombe). Hawa ni baadhi ya watu ktk wilaya ya Biharamulo na Bukombe ambao ng'ombe wao wamepigwa risasi na asikari gemu bila hata huruma. Baadhi ya ng'ombe wanao kamatwa kwenye hifadhi wenye nazo wanatozwa faini kubwa ambayo haizingatii hata hali halisi ya maisha ya wafugaji hao sijui kama hili linajulikana kwa wanaohusika. Bora wangetozwa hzo fedha tukajua zinawekwa kwenye mfuko gani na kusaidia nin ktk maendeleo ya maeneo husika yenye hifadhi husika. Naomba niishie hapa Kwa taarifa zaidi namba yangu ni 0684565348, pia nina mawasiliano ya watu ambao ni wahanga wa matatizo haya kwa uthibitisho zaidi.
 
Poleni sana kwa masahibu yanayo wapata. Musijali yawezekana haya ndiyo Maisha bora tuliyo ahidiwa.Ushauri wangu kwako ni huu hapa chini

Mkuu katika hili Mnaweza mukaishtaki Serikali na Kupata Haki yenu iwapo unauthibitisho wa hayo madai yako unachotakiwa kufanya ni haya yafuatayo
1.Kwanza uwe na uhakika hao waliofanya huo ukatili ni watumishi wa Uma.
2.Iwapo inawezekana kubaini Idara wanazotoka ni muhimu pia ili kuwashtaki ma waziri wao kwani ndiyo wanauwezo wa kifedha ya kulipa didia ya uovu uliofanywa.
3.Iwapo moja na mbili vimetimia unatakiwa uandike barua kuipa serikali siku Tisini ilikuwalipa fidia wote waliotendewa madhara kutokana na operation hiyo husika na Nakala apewe Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
4.Iwapo siku 90 zitatimia bila majibu ya Msingi toka Serikalini then unafungua Kesi Mahakama Kuu kudai Fidia yote yamali iliyo potea pamoja na ndugu aliye uwawa.

N.B.Tume zinazoundwa na ASerikali maranyingi huwa maamuzi yake hayaheshimiwi wala kufanyiwa kazi kikamilifu bora upime na kufanya utakalo ona lina manufaa kwenu na kwandugu zako Mkuu.
 
Inauma sana kupoteza ndugu kwa uwonevu, wanateseka na kuuwawa wengine ,,huku majangiri wakila bata mjini,,,,hiki kitendawili cha kulindana kulindana sijui nani atakitegua,,poleni sana
 
Back
Top Bottom