Unyanyasaji, ukatili watesa Watanzania ughaibuni

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,242
34,903
ZAIDI ya Watanzania 500 walioko nchini India pia nchi nyngine wameomba msaada wa kurejeshwa nyumbani baada ya kufanyiwa matendo ya kikatili na kukiukwa kwa mikataba yao na waajiri wao, anaandika Regina Mkonde.

Hayo yamesemwa na Mindi Kasiga, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali na Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakati akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam.

“Miezi ya hivi karibuni hususan kati ya mwezi Machi hadi Mei, 2016 balozi zetu nchini India na Malaysia zimepokea maombi ya kusaidia kuwarejesha nyumbani Watanzania ambao walipelekwa kwa ahadi za kupatiwa ajira.

“Baadhi ya wahanga wamekuwa wakikimbilia kwenye ofisi zetu za ubalozi kuomba msaada na kwamba, zilikuwa zikiwahifadhi ubalozini na kisha kuwasiliana na jamaa zao ili wawatumie nauli na kurejea nyumbani,” amesema.

Amesema, changamoto wanazokutana nazo ndizo zinawasukuma kuomba msaada wa kurejeshwa nyumbani huku akiwataka wananchi kutokubali kurubuniwa na ahadi za kwenda kufanya kazi nje ya nchi hasa zile ambazo zisizo za ujuzi.

“Wakifika huko hulazimishwa kufanya ukahaba na kunyang’anywa hati zao za kusafiria ili kudhibitiwa wasitoroke na ndiyo matatizo makubwa zaidi ambayo yamekuwa yakiwakabili watanzania,” amesema.

Sambamba na matatizo hayo, Kasiga ameeleza matatizo mengine yakiwemo ya kufanyishwakazi bila mikataba, kazi nyingi ambazo kimsingi zingetakiwa kufanywa na watu wa kada mbili au tatu pamoja kukiuka makubaliano ya awali.

Aidha, wizara imetoa wito kwa wananchi kutoa ushirikiano katika kutoa taarifa za watu wasio waaminifu wanaoshukiwa kujihusisha na mtandao wa biashara ya kusafiisha binadamu ambao uhusisha raia wa Tanzania waliopo ndani na nje ya nchi pamoja na wageni waliopo kwenye nchi hizo.

“Wizara inataka ushirikiano kutoka kwa wananchi katika kukabiliana na changamoto wanazozipata Watanzania nje ya nchi wakitafuta maslahi ya kiuchumi ambazo zinaviashiria vya biashara haramu ya binadamu,”amesema.

Amesema serikali haitowafumbia macho watu watakaobainika kujihusisha na mtandao huo na kwamba itawatia katika miko ya sheria kwa lengo la kutokomeza biashara hizo.

“Ni wazi kwamba vitendo hivyo ni uvunjwaji wa sheria na vya kinyama na kwamba vinakiuka haki za binadamu.Ifahamike kwamba usafirishaji wa binadamu ni uhalifu kwa mujibu wa makosa ya kupangwa ya Azimio la Umoja wa Mataifa Na. 55/25 la mwaka 2003,” amesema na kuongeza;

“Ambalo linazuia, kukomesha na kuadhibu usafirishaji wa binadamu hasa kwa wanawake na watoto chini ya itifaki yake, pia ni kinyume cha sheria ya Kupambana na Biashara Haramu ya Usafirishaji wa Binadamu ya mwaka 2008.”
 
India of all places????
Hii ni nchi ya matabaka hata kwao wenyewe. Ukiwa 'Harijan'[hili ni tabaka duni sana hairuhusiwi hata kidogo kugusana na aryans. mfumo wa india umekuwa hivyo na ingawa serikali imepiga marufuku tabia hizo lakini kwa vile zimekuwa ni mila na tamaduni ubaguzi/udhalilisha baina ya tabaka mbali mbali nchini india zinafanyika sembuse aende mwafrika????
 
True Mkuu
 
hao ujanjawaote Egypit huwakuti hao pale kiboko ya Farao na Mussa hawalembeshi Speed mchaka mchaka ya Maisha pale aswa kwa hao wados.....
 
Sasa hili litadhibitiwaje na serikali wakati ni maelewano ya watu wawili.mi nadhan labda ile sheria irejewe upya ili kila anaekwenda huko nje,hasa huko uarabuni,mashariki ya mbali na india ziangaliwe sababu maalum.inasikitisha bint anatoka hapa na furaha ya kupata kazi huko,anaenda kuishia ktk mateso tena akiwa mbali na jamii yake bila msaada hata wa serikali za huko!
 
Hayo manyanyaso yapo kweli hata nchi za Arabuni ndio yamekithiri dada zetu wanaochukuliwa kufanya kazi za ndani wakikuhadithia wanayokumbana nayo unaweza kulia
 
Mmbunge alokuwa akihamasisha vijana waende huko inabidi atumwe akaongee na hao walokuwa wakimpa fursa za kuwapelekeA watu huko wajue watz wameshoshwa na manyanyaso wanayoyapata.au wanaharakati andaeeni maandamano ya amani kuelekea baloz zao hapa nchin tuufikishe ujumbe
 
mkuu india sio ugaibuni mkuu huko ni kwa waindi

swissme
Huyo anachuki tu na warabu ndiomaana anatumia mada hiyo ugabuni mbona hamuogelei waAfrica wanaoteswa uraya wamebaki ugabuni ugabuni warabu mambo super kama hamuwapendi Warabu msiede dubai bc si warabu pumbafu
 
walitesa sana wazanzibar na mababu zetu.vipi umeolewa na waarabu? funguka tuwaite mashemeji.

swissme
 
Sasa hili litadhibitiwaje na serikali wakati ni maelewano ya watu wawili.mi nadhan labda ile sheria irejewe upya ili kila anaekwenda huko nje,hasa huko uarabuni,mashariki ya mbali na india ziangaliwe sababu maalum.inasikitisha bint anatoka hapa na furaha ya kupata kazi huko,anaenda kuishia ktk mateso tena akiwa mbali na jamii yake bila msaada hata wa serikali za huko!
Serikali ya Tanzania epegemalufuku mtanzania yayote kutoka kweye inchi yake na kwenda inchi ingine na hapo mtasema tu binadamu hawana kheri
 
walitesa sana wazanzibar na mababu zetu.vipi umeolewa na waarabu? funguka tuwaite mashemeji.

swissme
Utasema warabu waliwatesa babu zako na wazanzibari hapo ulipo mnateseka mpaka sukari kwa mgao mpaka leo hii
Mbona warabu wanaishi jagwani hakunahata miwa hawalili kusu msosi au sukari ya mgao usiongelee mambo yaliopita miaka miambili kwanza kuweni na maishabora hapo mlipo Warabu mambo super mtakujatu kufanyakazi ugabuni.....
 
sawa

sawa mke wa muarabu natumaini unatoa mkia maana waarabu kwa hayo mambo siju.

swissme
 
Mm nimwarabu walah sio mke wamwarabu nakushangaa unavyo kuwa na chuki na warabu hapo ulipo hata ujui utakula nn leo usiku
 
Huyo anachuki tu na warabu ndiomaana anatumia mada hiyo ugabuni mbona hamuogelei waAfrica wanaoteswa uraya wamebaki ugabuni ugabuni warabu mambo super kama hamuwapendi Warabu msiede dubai bc si warabu pumbafu
Duh kweli wewe kilaza ueleweki unachokiandika povu linakutoka tu.
 
Back
Top Bottom