Chuo hiki kimeanza katika hali ngumu sana na ya utisha na kusikitisha.Ukiachilia mbali uhaba wa waalimu ,wanafunzi hawajapata mikopo kwa muda mrefu tangu waanze,Hali inayowafanya waishishi maisha ya omba omba na umalaya kwa wanafunzi wa kike.
Ni kweli wazo lilikuwa ni zuri saana,Japo halikuwekewa mipango thabiti.Nilibahatika kutembelea mahali pale pakiitwa Chimwaga CCM Complex.Madarasa hayatoshi idadi iliyopo ya wanafunzi.Kwa ujumla maisha ya mwanafunzi ndani ya chuo hiki ni magumu sana.
Leo nasikia tena kuna mpango wa kuanzisha complex nyingine kubwa sana huko Bagamoyo ambayo imeshapatiwa na wafadhili.Hoja yangu kwanini wasikazanie kukamilisha hicho cha Dodoma kwanza ndipo wafikirie Bagamoyo?