Ndugu zangu ninavyoona mimi very soon United State of America itakuwa failed state na majimbo yote ya USA kutawanyika kama ilivyotawanyika majimbo ya USSR kwa sababu zifuatavyo:
1. Kushindwa kupata mrithi wa Rais Barrack Obamo. Wagombea wote wa urais wa Marekani Donald Trumph Na Hilary Clinton hawa wote hawakidhi kiwango cha Rais anayetakiwa Marekani na kuna dalili katika uchaguzi huu kuna uchakachuaji wa matokeo kufanyika.
2. Kuongezeka kwa masuala ya ubaguzi kwa kiasi kikubwa haswa kwa kufanyika kwa mauaji ya watu wenye asili ya watu weusi.
3. Kuhusika na kupanga njama za ugaidi wa 9/11 uliotokea miaka kumi na tano zilizopita, baada ya watafiti na wataalam kuchunguza kwa makini waliona ugaidi huo haukufanywa na vijana kumi na tisa wa kiarabu bali It was inside job ilitekelezwa na majasusi wa kimarekani kwa idhini ya Serikali yao ili kuipa sababu ya Marekani kuvamia Afghanistan Iraq Libya Syria. Kwa kumalizia ni kwamba nguvu ya kiuchumi ya Marekani imekufa. Kilichobaki ni kuprint Dola very soon hiyo Dola ya kimarekani haitaweza kutumika tena.