Marekani na Iran zimeripotiwa kufikia makubaliano ya kihistoria

Marekani na Iran zimeripotiwa kufikia makubaliano ya kihistoria

Ritz

JF-Expert Member
Joined
Jan 1, 2011
Posts
56,640
Reaction score
46,211
Wanaukumbi.

🇺🇸🇮🇷 Marekani na Iran zimeripotiwa kufikia makubaliano ya kihistoria.

Mambo muhimu ya makubaliano hayo ni pamoja na:

✅ Kukomeshwa kwa shughuli za kijeshi katika nyanja zote
✅ Kufunguliwa tena mara moja kwa Mlango-Bahari wa Hormuz
✅ Kuondolewa kwa kizuizi cha Marekani
✅ Iran yaahidi kutotengeneza au kununua silaha za nyuklia
✅ Kupunguzwa kwa vikwazo kwa awamu na kutolewa kwa mali zilizohifadhiwa zenye thamani ya dola bilioni 25
✅ Sherehe rasmi ya utiaji saini imepangwa kufanyika Juni 19 nchini Uswisi
========================

🇺🇸🇮🇷 The United States and Iran have reportedly reached a historic agreement.

Key points of the deal include:

✅ An end to military operations across all fronts
✅ Immediate reopening of the Strait of Hormuz
✅ Removal of the U.S. blockade
✅ Iran commits not to develop or acquire nuclear weapons
✅ Phased sanctions relief and the release of $25 billion in frozen assets
✅ Official signing ceremony scheduled for June 19 in Switzerland

View: https://x.com/americaspoof/status/2066343956569612618?s=46&t=mTROWpaJUT8H393JMgWOvw
 
Rais Trump anasema: Qatar inastahili sifa, na sifa lazima ipewe, na Waqatari walitusaidia sana katika makubaliano haya. Lazima tuelewe kwamba Qatar iko katikati ya kila kitu zaidi ya nchi nyingine yoyote na hata zaidi ya UAE.

Trump aliongeza: Tunahitaji saa moja na nusu ya ndege ili kufika huko, na vivyo hivyo kwa Saudi Arabia.

Ukishavuka mstari mmoja, uko hapo. Iko katikati ya eneo lenye uadui wa ajabu na limezungukwa na pande tofauti.

Trump aliendelea: Walitoa msaada mkubwa; Qatar ilikuwa msaada mkubwa katika kufanikisha jambo hili, na laiti watu wangetambua hilo. Walikuwa jasiri sana, na kiongozi wao, Emir, alikuwa jasiri sana.
‎#تميم_المجد
‎#قطر🇶🇦
‎#ترامب
‎#ايران🇮🇷

View: https://x.com/genalkhayareen/status/2066234525554712734?s=46&t=mTROWpaJUT8H393JMgWOvw
 
Binadamu tuna mambo ya ajabu sana. Sasa yote hayo ya Trump halafu wanayamaliza kwa maongezi?!
Kwanini Trump hakushinikiza MAONGEZI KWANZA?! Vita siyo solution ya kila kitu!
Watu wamekufa bure kisa ujinga wa orange man na genge lake!
Mjinga KABISA KABISA KABISA huyu Trump
 
Siku zote inafahamika duniani kote kwamba muafaka wa jambo lolote ni mazungumzo tu,lakini wakati mwingine mazungumzo hayafanyiki mpaka ukijiridhisha kumbe huyu ni mkubwa mwenzangu,ndio heshima inachukua mkondo wake

Sasa Trump baada ya kujiridhisha kwamba Iran ni mkubwa mwenzangu ndio wanakaa Meza moja sasa
 
Japo siafiki kipengele cha Iran kuzuiliwa kumiliki nyuklia ila sioni ni kwa namna gani Irani angekubali kusitisha kutengeneza au kununua nyuklia bila hii vita kutokea.

Nafikiri somo limeeleweka kwa pande zote mbili. Siku nyingine akipata wazo la kumshambulia Iran lazima ajiulize mara mbili.
 
Yaani USA ashinikize maongezi?? Alifanya Test ameona ugumu so ndo ikaja maongezi
 
Siku zote inafahamika duniani kote kwamba muafaka wa jambo lolote ni mazungumzo tu,lakini wakati mwingine mazungumzo hayafanyiki mpaka ukijiridhisha kumbe huyu ni mkubwa mwenzangu,ndio heshima inachukua mkondo wake

Sasa Trump baada ya kujiridhisha kwamba Iran ni mkubwa mwenzangu ndio wanakaa Meza moja sasa
Mkubwa mwenzake mtu kafyeka top leaders wako kakutia hasara ya $300b afu unasema wako sawa, mtu anatumia aircraft carrier na submarine kukubonda, anakupiga naval blockade na unaatulia
 
Japo siafiki kipengele cha Iran kuzuiliwa kumiliki nyuklia ila sioni ni kwa namna gani Irani angekubali kusitisha kutengeneza au kununua nyuklia bila hii vita kutokea.

Nafikiri somo limeeleweka kwa pande zote mbili. Siku nyingine akipata wazo la kumshambulia Iran lazima ajiulize mara mbili.
Mkuu,unadhani Iran wamesitisha mpango wao wa Nyuklia kisa hii vita? Wao kwanza huwa wanasema mpango wao ni amani ingawa ndo hivyo uranium imesharutubishwa kwa kiwango cha juu. Lakini kusitisha mpango wao wa Nyuklia mimi hapo nina wasiwasi
 
Naona kobazi wamelegea, hakuna nchi kiburi mbele ya US.
Kama ungekuwa wewe sio msukule wa Marekani au kilaza ungejua kuwa Marekani hii vita ameshindwa

Tokea lini Marekani akavamia nchi Kwa lengo la kupora rasilimali zao alafu akaomba mazungumzo?

Iraq
Libya
Venezuela

Huku kote mbona hakutaka mazungumzo na badala yake Hadi Leo bado anawaibia mafuta Yao
 
Mkubwa mwenzake mtu kafyeka top leaders wako kakutia hasara ya $300b afu unasema wako sawa, mtu anatumia aircraft carrier na submarine kukubonda, anakupiga naval blockade na unaatulia
Marekani na washirika wake wamepata hasara kiasi gani,au hukupata wazo la kuhesabu?..lengo ilikua regime change na nuclear program ife,wamefikia?

UK,France, Germany, Italy wanaiondolea vikwazo Iran Ili wapate mafuta, GCC countries zimeihonga Iran $12+b, USA ataondoa vikwazo,atairudishia Iran mali/pesa zake na bado Iran itaendelea na nuclear program
 
Binadamu tuna mambo ya ajabu sana. Sasa yote hayo ya Trump halafu wanayamaliza kwa maongezi?!
Kwanini Trump hakushinikiza MAONGEZI KWANZA?! Vita siyo solution ya kila kitu!
Watu wamekufa bure kisa ujinga wa orange man na genge lake!
Mjinga KABISA KABISA KABISA huyu Trump
Trump, kalazimishwa kufanya haya marengo yake ilikuwa kuingusha serikali ya Iran na kuweka kibaraka wake.

PEZESHKIAN ANAKATAA KUMSHUKURU MTU YEYOTE 🇮🇷

Katika hotuba kali Jumapili hii, Juni 14, Rais wa Iran Masoud Pezeshkian alitoa ujumbe wazi na usio na shaka licha ya shinikizo kubwa la kimataifa: "Hatutashukuru kwa nguvu yoyote, lakini tunabaki kuwajibika na kuwajibika kwa watu wa Iran na madai yao halali." Alisisitiza: Wairani wote, bila ubaguzi wa makundi.

View: https://x.com/camille_moscow/status/2066268430597054837?s=46&t=mTROWpaJUT8H393JMgWOvw
 
Marekani na washirika wake wamepata hasara kiasi gani,au hukupata wazo la kuhesabu?..lengo ilikua regime change na nuclear program ife,wamefikia?

UK,France, Germany, Italy wanaiondolea vikwazo Iran Ili wapate mafuta, GCC countries zimeihonga Iran $12+b, USA ataondoa vikwazo,atairudishia Iran mali/pesa zake na bado Iran itaendelea na nuclear program

Asante​

| Spika wa Bunge la Iran Mohammed Bagher (mjadili mkuu) na Waziri wa Mambo ya Nje Abbas Araghchi watasafiri hadi Geneva kusaini makubaliano hayo pamoja na Makamu wa Rais wa Marekani JD Vance.

Mkutano huo utaashiria ushiriki wa moja kwa moja wa ngazi ya juu zaidi kati ya Tehran na Washington katika kipindi cha miaka 47, tangu uhusiano wa kidiplomasia ulipokatizwa kufuatia Mapinduzi ya Kiislamu ya 1979 na mzozo wa mateka wa ubalozi wa Marekani.

Makubaliano hayo pia yatajumuisha ahadi ya Iran na Marekani kuheshimu uhuru wa kila mmoja na kujiepusha kuingilia mambo ya ndani ya kila mmoja.

Iran ilisubiri hadi baada ya saa sita usiku ili kukamilisha makubaliano hayo, ikiepuka kusainiwa siku ya kuzaliwa ya Trump.

Tofauti ya saa 7.5 iliruhusu Tehran na Washington kudai kwamba makubaliano hayo yalikamilishwa katika tarehe wanayopendelea—Jumapili kwa Trump na siku inayofuata kwa Iran.

View: https://x.com/visionergeo/status/2066297017542779295?s=46&t=mTROWpaJUT8H393JMgWOvw
 
Mkuu,unadhani Iran wamesitisha mpango wao wa Nyuklia kisa hii vita? Wao kwanza huwa wanasema mpango wao ni amani ingawa ndo hivyo uranium imesharutubishwa kwa kiwango cha juu. Lakini kusitisha mpango wao wa Nyuklia mimi hapo nina wasiwasi
Fatwa ishatolewa na kiongozi wa dini kwamba Nyuklia ni haramu hawana mpango wa Silaha za Nyuklia na hata hio Nyuklia Yao ya sasa haijafikia uwezo wa kutengeneza Bomu, miaka yote Iran anakaguliwa na hakuna ushahidi wowote Wana hizo Silaha.

Israel anachoogopa ni uwezo wa Iran kisayansi, unapoweza kurutubisha Nyuklia unapata source ya uhakika ya Energy, ambayo haina limit kuhusu matumizi yake,
 
Back
Top Bottom