Richard
JF-Expert Member
- Oct 23, 2006
- 15,502
- 22,355
Leo katika gazeti la Mwananchi la mtandaoni, kuna habari kwamba watoto 269 wanakufa kila siku nchini Tanzania habari ambazo zinaelekea kutia shaka.
Katika habari hiyo iloandikwa na mwandishi Lilian Timbuka ambae ameripoti habari hiyo kutokea Moshi mkoani Kilimanjaro, kuna utafiti ambao umefanywa na shirika linalohudumia watoto duniani la UNICEF ambapo kupitia mwakilishi wao hapa nchini bibie Maniza Zaman wametoa taarifa ya utafiti wao huo.
Mwakilishi huyo wa UNICEF nchini alikuwa akizungumza katika mkutani wa jukwa la wahariri nchini Tanzania TEF unaofanyika mkoani humo na akaendelea kusema kwamba akina mama wajawazito wapatao 556 hufariki dunia kutokana na matatizo ya uzazi.
Pia kwa upande wa elimu mwakilishi huyo amesema kwamba asilimia 39 ya wanafunzi wa kike na wa kiume ndiyo huhitimu elimu ya sekondari kila mwaka!
Kwanza ningependa kumpoNgeza mtafiti huyo kwa taarifa yake ambayo pengine imetumia muda mfupi au mrefu katika kuiandaa na kwamba ni mpaka shirika la kuhudumia watoto duniani limekuja kugundua idadi ya watoto 269 hufa kila siku nchini Tanzania na wizara ya Afya ipo na inaendela na shughuli zake.
Ila tabia ya watanzania kungojea kutafuniwa taarifa kama hizi kunatuweka kuwa bado tupo katika giza katika masuala ya maendeleo ya teknolojia ya habari na ufanyaji utafiti.
Nina masuali kadhaa kuhusiana na hii taarifa ya utafiti:
Je, taarifa hii haifanani na ile taarifa ya kuwepo kwa ugonjwa wa ZIKA ambayo ilisababisha Dr Mwale Malecela apoteze kazi kwa kutoa taarifa za utafiti bila kushauriana na wizara husika?
Je, hakuna mwandishi wa habari ambae anaweza kuwa ni mtafiti na Akaja na taarifa mbadala ambayo inaoanishwa na hii ya UNICEF?
Je, ni kwanini huwa watanzania tunangoja hadi mtu atoke huko nchi zingine na atuletee taarifa nyeti na muhimu ambazo zinagusa maslahi ya taifa?
Na mwisho, hili jukwaa la wahariri kazi yake ni ipi khasa kuandika tu habari maana imetolewa au kuiahiri kwa kutafuta habari zaidi kabla ya kuichapisha?