Unguja waongoza kwa elimu duni

Kama uko huko,fine,andaa proposal na kafanye utajua sababu!na ukiziweka mtandaoni,haziwi tata
 

Umeanza Vizuri Lakini Hukuridhika Mpaka Utie Pumba Zako!!

Nanukuu "Hijabu zipigwe marufuku, suluali kwa wasichana marufuku. Wanafunzi Wanabobea kwenye dini kuliko Elimu dunia" Mwisho Wa Kunukuu.

Hivi Mavazi Yana Uhusiano Gani Na Matokeo Ya Mtu?? Au tu uoneshe Udini wako Dhidi Ya Jamii ya Kizanzibari? Huo Ni Ujinga, Kama Hujui Kinachoidhuru Unguja hebu sema uambiwe.

Unguja inauliwa na Na CHUKI ZA KISIASA na wala si Jengine.

Wameingiza Siasa za Kikada Kuwa Ziongoze Taasisi ya Elimu badala ya Taaluma.

Katika Suluhisho lako Hukuiongelea Point hii ya Siasa, hii inaonesha wazi kuwa huna uelewa na Wazanzibari.

Sasa suluhisho Pekee La Elimu ya Zanzibar/Unguja ni "KUTENGANISHA CHUKI ZA KISIASA NA ELIMU"
Wawape Watendaji Wenye Sifa Waongoze Taasisi hii ya Elimu badala ya Kuwapa Makada wasiokuwa na Uwezo wowote.
 

Halafu Wewe Tatizo lako Huujui Uislamu Halafu Unataka Kuucomment Uislamu!!

Mara Nyingi Munatumia "MADRASA" kama ni "WEAKNESS POINT" dhidi ya Waislamu.

Na unadai Kuwa Wazanzibari Wanatumia Muda Mwingi Madrasa Kuliko Shule!! Je Hapo Dar es Salaam unapoishi Hapana Waislamu?? Je Ni wote wanakwenda Madrasa??

Sasa ukweli ni Kwamba Asilimia 99.99% ya Wazanzibari ni Waislamu, Lakini Asilimia 85% hawaendi Madrasa wala Hawakujui hasa!! ni Asilimia isiyozidi 14 ndiyo wanaokwenda Madrsa nikiwemo mimi na wala sijafeli na Chuo nategemea Kuingia mwaka huu.

Kwahiyo si Kila Muislamu Kuwa Anakwenda Madrassa, Wengi wao ni Waislamu Majina tu hawana ishu na Madrasa ni Kama Wapagani Kama unavyowaona hapo Bongo.
Usidharau Dini ya Wenzio.

Tatizo ni Siasa Kwa Zanzibar na wala si Madrassa.
 
Mkuu Tatizo pekee ni Kuwa Taasisi ya Elimu inaendeshwa Kikada na Watendaji Wabovu Wengi Wao Wana Vijidiploma Vya Miaka ya 70 na 80 ambao Ndiyo Maafisa Wa Elimu Zanzibar.

Pindipo itaondoka Siasa hii ya Uunguja na Upemba basi Tatizo litaobdoka.
 
Niko kwenye taasisi za tafiti, sema kingine.
Sasa Wewe Upo Nje ya Zanzibar Halafu Unaleta Conclusion ya Tafiti ya Zanzibar si Maajabu hayo.

Kama Kweli Wewe Ni Mtafiti Basi Nenda Zanzibar Hala Tembea Mikoa Yote 10 ya Zanzibar Ufanye Tafiti Sahihi ili Utuletee Majibu Hapa! Siyo Ufanye "TAFITI ZA KEYBOARD" ukiwa Umejifungia Ndani Halafu Unaita Utafiti duh!!
Mkuu usiitie Aibu Fani Muhimu na Nyeti ya Utafiti kwa Utafiti huo.
 
Kadhia hii SMZ kimyaa sijui zigo la aibu.
Ndiyo! Sasa Wanapanga Pa Kujitoa Kimasomaso Wadai Maalim Seif Sharif Kawafelisha Kwasababu Hakuna Watu Majuha Duniani Kama Viongozi/Makada Wa Serikali Ya Zanzibar.

Hapo Baada Ya Kutafuta Suluhu, Wao Wataangalia Kwanini ""WAPEMBA HAWAMO KATIKA 10 MBOVU?""
 
Matatizo ya Nchi za AFRICA yanafanana ktk Elimu, haitaji tumu kupima la damu kupima Malaria.
Ww jikite kwenye Mada, kipi siyo sahihi kuliko kuropoka hapa!!
 
Usidhani hapa Tz bara ni Wakristo tu, laa Asha! Nimchanganyiko tena mkubwa tu!!
Kwa Tanzania hakuna familia ya kikiristo 100%, bila kuwa na uncle, aunt, grandfather or grandmother, nk Muislam!! Mm binafsi nina mama zangu walio olewa na Waislam!! Hivyo nina wadogo zangu Waislam.

Pia ktk sababu hapo, hiyo ni 1 Kati ya 13. Nadhani ungejikita hasa mawazo yako ktk mada badala ya kutoa Mapovu ili halisababu zimeelezwa kutoka no 1 hadi 13. Sijui hiyo 1 ndio imekuuma ua?
 
Itikadi za dini ndizo zinazowaharibu kule visiwani hata ufanye nini watu hawapendi kabisa kusoma ila muda wa kwenda madrasah sasa ukifika mzazi anakuwa mkali sana.
 
Suluhu ya tatizo la Elimu Zanzibar siyo SIASA wala nn!! Hata Hotuba za Mhe: Duni nilikuwa sizielewi kabisaaa, licha yy kuwa na Afya tele lakini E. Lowaasa alikuwa mgonjwa!!! Tatizo ni Elimu na mfumo wake!!

Ukikuta DEMU kavaa "kimini," Kikuku, "Transparent clothes-kavaa night dress mchana" tafsiri ya kwanza kwa muoji ni ipi? Kijana kavaa Kata "K" mtizamo wako kwake ni upi?

Mada SIYO madrasa wala Hijabu!! Mada jadili tatizo la Uduni wa Elimu Unguja. Mm nimetoa ushauri au mtizamo wangu 1-14. Bora ujikite ktk sababu zote (ktk ushauri) badala ya kubisha ili uonekane bingwa wakati hakuna cha maana ndani yake.
 
Ndiyo! Hiyo Moja (1) imenigusa Kwasababu Vazi halina Uhusiano na Kufaulu au Kufeli Kwa Mtu, Nadhani Mtu Yeyote Atakae eka itikadi Mbele Na Kuangalia Uhalisia Basi Hawezi Sema Mbele Za Watu Kuwa eti "KUVAA HIJAB KUNAMFELISHA MTU" hili kweli ni wazo la Great thinker??
Nyengine Kati ya Hizo Sizicomment Kwasababu Mimi Nimuelewa na Ninajua Kuwa Zinaathiri Sekta ya Elimu Kwa Njia Moja ama Nyengine Na Ninakuunga Mkono Kwa Hilo wala sitokufanyia Wivu.

Mkuu Unakataa tu, Lakini Hiyo Point number 1 umebugi sana! Kubali tu Kuwa Hapo umeonesha hisia Zako Za Kidini tu, na wala hukukusudia Kutatua Tatizo.
 
BRN unguja.
 
Sasa Mtafiti Gani wewe usiejua Uhusiano Wa SIASA ZA KIKADA na Ufelishaji Wa Wanafunzi??

Hebu Waulize Wanafunzi Unaowahamu Wanaosoma SUZA au Katika TAASISI yoyote hile Zanzibar Wakupe Ukweli!!
 
Matatizo ya Nchi za AFRICA yanafanana ktk Elimu, haitaji tumu kupima la damu kupima Malaria.
Ww jikite kwenye Mada, kipi siyo sahihi kuliko kuropoka hapa!!
Tatizo la Mada Yako Umechanganya Upotoshaji na Ukweli.
 
Kwa mf. Tanzania bara SAUT toka 2008 kuna dressing Code huwezi kwenda pale na kimini chako, na Urasi wako eti msomi; CBE -2015 ni dress code kwenda mbele. Je tukiruhusu kila dini kuja na vazi lake itakuweje? Mf. Wapagani, Wahindi, Walokole wale wa misimamo mikali-nguo zao nyekundu (hawapandi magari, hawatumii dawa za hosp, nk) je itakuwa shule au Kitchen Party?
Pia vazi hilo lilikuwa tu mfano, ila si msumari!! Nadhani unesema sababu tajwa hapo 13 zinachangia au hazichangii kuliko kuja hapa na misimamo ya ajabu ajabu!!

Hata Primary tuna ambiwa raba lazima iwe nyeusi! Wao unadhani ni wajinga?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…