UNGUJA: Jeshi la Polisi lalazimika kufunga vituo vidogo kutokana na uhaba wa askari

Zurie

JF-Expert Member
Jul 6, 2014
2,002
5,536
Jeshi la Polisi Zanzibar limesema kuwa limelazimika kufunga vituo vidogo katika Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja kutokana kukabiliwa na upungufu wa Askari visiwani hapo.

Hayo yamesemwa na Kamishna wa Polisi Zanzibar, Hamdan Omar Makame, amesema kuwa vituo hivyo vimefungwa na sasa vitalazimika kutumiwa na askari Jamii katika kuimarisha ulinzi.

“Tuna askari wachache ndiyo maana vituo vidogo tumelazimika kuvifunga na badala yake vitatumiwa na askari Jamii kutoa huduma za ulinzi katika maeneo yao.” amesema Kamishna Hamdan.

Aidha, amesema baada ya vituo hivyo kufungwa, wananchi wanatakiwa kuripoti matatizo yao katika vituo vya polisi vya karibu yakiwamo makosa ya uhalifu yanayotokea katika maeneo yao

Hata hiyo, amevitaja vilivyofungwa kuwa ni Vituo vilijengwa chini ya mpango wa Waziri wa zamani wa Mambo ya Ndani, Augustino Mrema, ukiwa mkakati wake wa kupambana na uhalifu Zanzibar na Tanzania Bara.
 
Mbona wakati wa uchaguzi walikuwa wengi sana, aaah OK kumbe wale walikuwa wapiga kura
 
Back
Top Bottom