Jodeo
JF-Expert Member
- Mar 10, 2015
- 1,286
- 1,328
Ni miaka karibu miwili sijaenda nyumbani kutokana na harakati mbali mbali za utafutaji.
Last December nikasema lazima niende nyumbani hata kama ni kwa wiki moja tu.
Baada ya kufika home kama ilivyo kawaida ya jamii zetu tunatembelea watu muhimu hususani majirani n.k miongoni mwao ni mama mjane ambaye alifiwa na mume wake wakati huo mie nikiwa mbali na hivyo sikupata nafasi ya kuwapa pole.
Jioni moja baada ya Christmas na mwaka mpya nikaenda kumsalimia huyo mama mjane na kumpa chochote kama pole ya msiba. Wakati maongezi yanaendelea kati yetu, ghafla nikahisi mabadiliko ndani mwangu ba kuhisi jambo baya linataka kutendeka. Hivyo nikakosa amani na nikatamani kuondoka haraka iwezekanavyo.
Wakati ananisindikiza na baada ya kuagana nje ya geti la nyumba yake, Mimi nikaondoka. LAKINI BAADA YA HATUA CHACHE NIKASIKIA SAUTI NDANI YANGU IKISEMA "GEUKA". Kweli nikageuka, NIKAMWONA YULE MAMA AKICHOTA MCHANGA WA NYAYO ZANGU NA BILA KUPOTEZA MUDA AKAINGIA NDANI.
Nilipigwa na butwaa na kukosa cha kufanya. Nikaendelea na safari kurudi nyumbani. Ilikuwa majira ya saa mbili Usiku nikamkuta mama yangu (wa kambo) akiwa sebuleni anaangalia taarifa ya habari. Nikamsalimia na kisha nikampa na salamu zake kutoka kwa jirani yake (yule mama mjane a.k.a mchota nyayo).
Mama akazipokea zile salamu lakini akakazia kusema;" USIPENDE KWENDA KWENDA HUKO!". Hilo jibu lilinimaliza kabisa baada ya kukumbuka tukio lililotokea muda mfupi (LA kuchotwa mchanga wa nyayo zangu). Nikajipa moyo maisha yakaendelea.
Sasa takribani miezi mitatu tangu wakati huo mambo yangu kiukweli hayaendi sawa kabisa. Kila nikijitahidi issue haziendi yani. Ndipo nikakumbuka watu husema kwamba kuna mambo ya uchawi wa mchanga na nilipokumbuka hilo tukio nikasema lazima niwajuze wana JF maana hawakosagi neno.
Hivyo basi naomba kuuliza yafuatayo;
1. Ungekuwa wewe ungefanya nini siku unaona mtu anachota mchanga wa nyayo zako?
2. Kuna uwezekano kwamba kuna mambo ya kiswahili yalifanyika kupitia mchanga huo kiasi cha kuharibu issues zangu ambazo kwa Sasa haziko sawa kabisa?
3. Kama ni jibu ni ndiyo hapo na. 3. Suluhisho ni nini?
Naomba kuwasilisha nakala hii kwa; MSHANA JR, MZIZI MKAVU, MTU MZITO, JICHAWI na wote wana jf.
Nakumbuka MISS NATAFUTA aliwahi kusema;" watu wanaweza kukufunga usifanye jambo lolote humu duniani".
Natanguliza shukrani kwa wote.
~Jodeo~