Ungekua wewe, ungefanyaje?

Ungekua wewe, ungefanyaje?

edward93

JF-Expert Member
Joined
Jun 27, 2015
Posts
563
Reaction score
1,354
Nakumbuka miaka kama miwili nyuma nlikutana na mzee mmoja akanipa kisa hiki.

Kuna marafiki wawili walioshibana walianza maisha pamoja, wakiwa wamepanga chumba kimoja ila baada ya miaka miwili ya utafutaji na mambo kuanza kukaa kwenye mstari! Mmoja (Hapa tumuite K) alimtaarifu mwenzie kuwa anataka kuoa!
Rafiki yake akasema jambo la heri na ukiangalia now uchumi sio mbaya sana basi mimi nitatafuta chumba sehemu nyingne ila bahati nzur kwenye nyumba hiyo hiyo kuna mtu alihama so yule rafiki mwingine (J) akahamia "next door" alipohama mtu na baada ya mwezi tu kweli yule K akaoa.
Maisha yakaendelea ila katika kuishi kwao bado mambo mengi walikua wanashare na urafiki ukazidi na pamoja na kugawana vitu vya ndani still bado vitu vidgo vidgo walikua wanashare (tunaoishi nyumba za kupanga tunaelewa).
Basi siku moja wakati k ameenda kazini bwana J alitaka kwenda kuoga lakin alikuta ndoo(wanashare) ina maji, akamuuliza shemeji yake, shem akasema ameweka yy anataka akaoge, basi bwana J akamwambia ukimaliza naomba ndoo na mm, shemeji akaoga then akamwmbia ndoo tayri! Ila bwana J alipotoka akaona kwenye ndoo kuna chupi ya shemeji amesahau, akili zikacharge akaona sio heshima kusema basi akaiangushia ndani kwake kwa mawazo kuwa akitoka kuoga atairudsha pamoja na ndoo yake bila kusema kitu.
Akajifunga taulo lake kaingiza ndoo ndani anachota maji mara ghafla anaskia shemeji anauliza "shem ujaona mzigo wangu?" Jamaa akajibu "nimeuona shem ingia uuchukue" bas shemeji kaingia ndani kaokota chupi yake anatoka, ile anatoka tu hamadi mumewe huyu hapa anaingia anamkuta mkewe anatoka chumba cha rafiki yake kavaa khanga moja bila chupi ndani, kaishikilia mkononi na kbla ajakaa sawa rafiki yake anatoka nae akiwa na taulo anaenda kuoga.

Ungekua ww ndio mume, ungejenga picha gani na je ungewaelewa? Na kama unavyojua nyumba za kupanga pengine ulishaskia za chini chini

Happy new year fellas!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wasubiri wakitoka kanisani watakuja kukujibu.

Ila huyo mzee mwishoni alikuambia kitu gani?
 
Si rafiki hata siwezi kuumia eti.😀
Angakuwa bwege mwingine hapo ingekuwa world war III.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom