Ungekua kiongozi je ungependa uwe kama nani kati ya hawa hapa??

tikatika

JF-Expert Member
May 6, 2011
2,330
4,119
Katika maisha kila mtu ana maono yake, na sote tuna matamanio yetu ambayo tungependa kuyafikia hata kama hatuna uwezo huo!! Mfano kwa wapenzi wa mpira ukiwauliza ungependa uwe kama nan kama ungekua mchezaji?? Atakujibu kama fulan kutegemea na mapenzi yake na uchezaji wake wa mpira kwa mchezaji husika.

Sasa tukija kwa viongozi wetu kila mwananchi kuna mtu anaye penda kuwa kama yeye endapo angekuwa kiongozi. Sasa je, ungekuwa kiongozi ungependa kuwa kama hawa hapa kiutendaji na hata uongeaji??!!

Tuanze kwa wakuu wa wilaya je ungekuwa kama Kasesela wa Iringa au Hapi wa Dar ungejisikiaje!??

Ungekuwa mkuu wa mkoa je ungejisikiaje kama ungekua kama Gambo wa Arusha au Makonda wa Dar??

Ungekua mbunge ungejisikiaje uwe ndio Ally Keissy wa Rukwa au Miringa wa Morogoro??

Ungekua waziri ungejisikiaje wewe uwe ndio Mwakyembe wa Wizara ya Habari na Michezo au Waziri wa viwanda Mwijage mzee wa sound!!

Au ungefunga kazi ukaamua kuwa rais wa nchi ungejisikiaje uambiwe utendaji wako, maamuzi yako, ongea yako ni kama mheshimiwa rais wetu Magufuli??
Yaan mnafana kweli kweli!!
 
Wote hao uliowataja ni wa OVYO sana..
Sidhani kama naweza kuwa kama hao lakini kama ndio ningekuwa kama wao.. ngejisikia vibaya sana.
 
Me ningependa kua Mwijage, Nawapiga Sound tuu... Kuongoza Watanzania shids sana..
 
Back
Top Bottom