Ungefanyaje kama ungekutana na hali kama hii?

Ungefanyaje kama ungekutana na hali kama hii?

Jitu la kienyeji

JF-Expert Member
Joined
Dec 13, 2014
Posts
4,443
Reaction score
7,979
Fikiria unakutana na msichana club ambaye ulisoma nae zamani shule ya msingi. Jina lake ni Mage na wote mmelewa chakali. Mage anakuomba lift kuelekea nyumbani kwake na ni usiku wa manane. Kwa vile wote mnaishi uelekeo mmoja unakubali kumpatia lift hadi anakoishi.

Unamwambia akae seat ya mbele na unatoka kidogo kwenda kuchukua kinywaji take away. Wakati umetoka Mage anamwona jirani yake ambaye nae alikuwa anatafuta usafiri wa kurudi nyumbani. Mage pasipo aibu anamwambia huyo jirani yake akae kwa gari seat ya nyuma ya gari.

Unaporudi unaendesha gari wala hujui kama kuna mtu mwingine zaidi yenu wawili na wala hata Mage hakwambii kitu kwa vile nae kalewa sana kwa hiyo chaneli hazishiki vizuri na usingizi nao umemwelemea.

Mara unafikisha Mage anapoishi na unamsaidia kumfikisha kwake na kisha mnaagana na unaondoka kurudi kwako.
Kichwani huna habari yoyote kwamba kuna msichana Cathy yumo ndani ya gari seat ya nyuma na yuko hoi hajitambui na wala Mage hakukwambia chochote.

Unafika nyumbani na kuiweka gari yako parking na kwa vile umechoka unaenda moja kwa moja ndani na kulala.
Kesho yake kunapokucha na ni Jumapili wife wako anajiandaa kwenda kanisani na huwa analitumia gari hilo kwenda nalo.

Mkeo anapofungua mlango wa gari majira kama ya saa 1 asubuhi ili awahi misa ya kwanza anakutana na sura ya kike, kajilaza kiti cha nyuma, kavua viatu, ana min skirt na kibaya zaidi msichana hajavaa nguo za ndani na kila kitu kiko wazi.

Kwa kutumia graph eleza namna ambavyo utamshawishi mkeo aamnini kwamba huna uhusiano na Cathy na wala hata humtambui kabisa. (Alama 60)
Unaruhusiwa kutumia calculator pamoja na Four Figure
Time: 24 hours I
 
Hadithia kama ilivyokuwa,kama haelewi nenda rudi bar kanywe utamkuta wife kashaenda kwao for holiday!
 
Asubuhi mlimkuta hai? Hukufunga vioo vya gari?
 
Huyo Cathy ningemuona kabla sijaondoka club hivyo sijafikanae home.
 
Hapo sasa nitahisi wife kanitegea hasahasa kama tulikua na kaugomvi, kwaiyo itambidi yeye ndo ajieleze
 
Hii wala sio mbaya sana, mwambie ukweli wote maana ulitoa lift kwa mtu ambaye mlisoma naye na hamna uhusiano wowote ,akikataa kukuelewa huyo anatafuta vita tuu , na nani analeta mchepuko nyumbani anamwacha kwenye gari? na umwambie ungekuwa mchepuko nisingerudi nyumbani
 
Naona km imerudiwa hii au nna macho mabovu?
 
Weka link Kama kweli huna Macho mabovu!
Hii hapa mkuu
Cathy

Fikiria unakutana na msichana club ambaye ulisoma naye zamani shule ya msingi. Jina lake ni Mage na wote mmelewa chakali. Mage anakuomba lift kuelekea nyumbani kwake na ni usiku wa manane. Kwa vile wote mnaishi uelekeo mmoja unakubali kumpatia lift hadi anakoishi.

Unamwambia akae siti ya mbele na unatoka kidogo kwenda kuchukua kinywaji 'take away'. Wakati umetoka Mage anamwona jirani yake ambaye naye alikuwa anatafuta usafiri wa kurudi nyumbani. Mage pasipo aibu anamwambia huyo jirani yake akae kwa gari siti ya nyuma ya gari.

Unaporudi unaendesha gari wala hujui kama kuna mtu mwingine zaidi yenu wawili na wala hata Mage hakwambii kitu kwa vile naye kalewa sana kwa hiyo chaneli hazishiki vizuri na usingizi nao umemwelemea.

Mara unamfikisha Mage anapoishi na unamsaidia kumfikisha kwake na kisha mnaagana na unaondoka kurudi kwako.
Kichwani huna habari yoyote kwamba kuna msichana Cathy yumo ndani ya gari siti ya nyuma na yuko hoi hajitambui na wala Mage hakukwambia chochote.

Unafika nyumbani na kuiweka gari yako parking na kwa vile umechoka unaenda moja kwa moja ndani na kulala.

Kesho yake kunapokucha na ni Jumapili wife wako anajiandaa kwenda kanisani na huwa analitumia gari hilo kwenda nalo. Mkeo anapofungua mlango wa gari majira kama ya saa 1 asubuhi ili awahi misa ya kwanza anakutana na sura ya kike, kajilaza kiti cha nyuma, kavua viatu, ana min skirt na kibaya zaidi msichana hajavaa nguo za ndani na kila kitu kiko wazi.

Kwa kutumia graph eleza namna ambavyo utamshawishi mkeo aamnini kwamba huna uhusiano na Cathy na wala hata humtambui kabisa. (Alama 60)

Unaruhusiwa kutumia calculator pamoja na Four Figure.

Time: 24 hours...View attachment 2345600
 
kumbe pepa limerudiwa na watu wamelisovu

four figure ya nini hapo, wakati majibu tunayajua
 
Sasa kama mtu anafumaniwa live na wife na bado anakataa katakata kukiri kosa na kusema amesingiziwa, itakuwa hiyo. Kwa hiyo hapo ije mvua lije jua ni kukataa tu kwamba hujui chochote na msala wote utamwangukia huyo bidada..
 
Back
Top Bottom