Ungefanya nini kwa kutoa msaada kama huu? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ungefanya nini kwa kutoa msaada kama huu?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by bhageshi, Oct 12, 2012.

 1. bhageshi

  bhageshi JF-Expert Member

  #1
  Oct 12, 2012
  Joined: Jul 24, 2010
  Messages: 264
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  Jumapili iliyopita mjomba wa rafiki yake alikuwa kwenye daladala akitokea ubungo kwenda tegeta, basi lilipofika mwenge abiria waliongezeka na wengine wakawa wamesimama,kati ya waliosimama alikuwapo mzee mmoja aliyekuwa na hand bag kama tunazobebea laptop hivi, yule mzee alimuomba mjomba wa rafiki yake amsaidie kumshikia bag lake kwa kuwa yeye alikosa siti, bila ya kusita akaamua kumsaidia bag hiyo.

  Baada ya vituo viwili yule jamaa mwenye bag; alitelemka bila mjomba wa rafiki yake kumuona na yeye hakuwa na wasiwasi kwa kuwa alijua mwenye mzigo akitaka kushuka atauchukua tu mzigo wake. Kabla gari haijafika kituo cha tatu ilisimamishwa na watu waliojitambulisha kwamba wao ni askari polisi wapelelezi kwamba kuna kitu wanapeleleza,wakawaamuru abiria wote watelemke kwenye gari,walifanya hivyo, mmoja wa wale polisi, walimfuata mjomba wa rafiki yake na kumuuliza na wewe kwenye bag lako kuna nini? Akawajibu bagi siyo langu kwa hiyo siwezi jua ndani kuna nini!! Wakamuuliza tena, mwenyewe yuko wapi tuoneshe" akaangalia kati ya wale abiria wenzake hakumuona, wakasema fungua tuone kuna nini ndani, walipofungua wakakuta kuna silaha aina ya pistol.

  Alipojaribu kujitetea wakamwambia twende kituoni utaenda kujieleza huko. Basi likaruhusiwa na yeye wakampeleka polisi, wakiwa njiani wakamwambia kama anataka wamwachie atoe laki nane 800,000/= vinginevyo watamuunganisha katika kesi ya wizi wa kutumia silaha, akawaambia sina hizo pesa na siwezi kutoa mpaka sasa bado yupo ndani.kweli tunapenda kuwasaidia watu lakini misaada mingine sometimes inaponza tuwe makini na misaada tunayoitoa.
   
 2. Lait noir

  Lait noir Member

  #2
  Oct 12, 2012
  Joined: Aug 23, 2012
  Messages: 99
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Very sad kwa kweli!
   
 3. Mkwanzania

  Mkwanzania Senior Member

  #3
  Oct 12, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 161
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 45
  Kwenye daladala msaada pekee unaoweza kutoa ni kumpisha mtu siti akae.....mambo ya kubeba mizigo ya watu ni lazima tuwe makini sana.
   
 4. bhageshi

  bhageshi JF-Expert Member

  #4
  Oct 12, 2012
  Joined: Jul 24, 2010
  Messages: 264
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  Kweli ndugu yangu inaumiza sana. lakini ukifikiria sana unahisi ni kama mchezo wa afande mwema wamecheza mchezo mchafu, inahitaji umakini sana kuchomoka katika dhahama kama hii
   
 5. Gama

  Gama JF-Expert Member

  #5
  Oct 12, 2012
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 9,227
  Likes Received: 1,414
  Trophy Points: 280
  Mbona hii kitu ina postiwa kila wiki, ikidai last wiki?
   
 6. BRO LEE

  BRO LEE JF-Expert Member

  #6
  Oct 12, 2012
  Joined: Dec 25, 2011
  Messages: 580
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 45
  Huo utakuwa mchezo tu umepangwa siamini kama askari wetu wana uwezo mkubwa wa kubaini vyanzo vya uhalifu/uhalifu bila kupewa taarifa na m2 wa tatu, hapo anasubiriwa mtu aende kumdhamini asomeshwe hiyo hela ilipwe.

  Wanao kwenda jela siyo wote wana hatia( sababu baadhi ya polisi wa upelelezi kwa njaa zao na utovu wa maadidili huwa wanaamua kutoa maelezo ya uongo kwa kupewa rushwa.
   
Loading...