Hydrazin
JF-Expert Member
- Oct 3, 2015
- 253
- 372
Baada ya mihangaiko ya weekdays siku kama ya leo wengi wetu hujaribu kuipumzisha akili na mwili pia, wengine hupendelea kwenda maeneo tulivu kama beaches n.k lakini wengine tunapendelea kukaa majumbani mwetu na ma--bachelor wenzangu ambao tunakosa hata time ya kupika na kuishia kuwa wateja wazuri wa fast food basi leo tunajaribu kukaa na kujiandalia Menu yetu huku muda ukiyoyoma tukishukuru Mungu kwa pumzi ya uhai.
Leo katika kupumzika kwangu basi nikaishika album ya picha zangu ili nijikumbushe kidogo safari yangu ya kuwepo chini ya jua na kuwakumbuka ndg na jamaa ambao nimewahi ku-interact nao kwa namna moja ama nyingine, najipongeza mwenyewe kwa kuwa mtunzaji mzuri maana naziona hadi picha ambazo nimeshika kidumu na fagio la chelewa nikiwa nimesimama mguu sawa (hahaha maisha yanaenda kasi sana).
Nikiwa katika kufungua kurasa moja baada ya nyingine ya album yangu nakutana na picha ya huyu mwanamke mwenye jina zuri kabisa la "Everlight" najikuta natabasamu mwenyewe sina hakika kama ni tabasamu la furaha lakini am quite sure ni tabasamu la kushangaa kuwa hawa viumbe psychology yao ni undefined.
Everlight mmarangu heshima yako mama popote ulipo, uliyekuja kuni-prove wrong kwenye maisha yangu kwamba sina ukidume wowote katika maumivu ya moyo maana nilikuwa nashangaa wanaume wenzangu wakitiririka machozi kisa kutendwa na ninyi wavaa sketi, na kujiapia mwenyewe kwamba mimi mwanamke hawezi kunifanya nisiwe na amani, kumbe nilikuwa najifurahisha.
Ulikuja kwenye maisha yangu nikiwa niko moto, nikiwa kijana mtanashati ninaejipenda na kupendwa na wenzako wengi, nikionekana mtoto wa kishua kumbe nilipendeza kwa ileile hela ya "BOOM" kuvaa vizuri ni hulka ya mtu na kweli unadhifu huficha ufukara, background yangu ilikuwa siri yangu mwenyewe.
Pamoja na kupendwa na wenzako wengi huku wengine waki-propose wenyewe na kunipa kiburi cha kuwa-underestimate huku wengine nikiwaacha bila sababu, wakiishia kunitamkia maneno ya laana kuwa "malipo ni hapahapa duniani" lakini mimi nikiona ni dua la kuku kumbe upo njiani mama unakuja kutimiza maandiko yao (daah kweli nature iko balanced).
Haikuwa kazi rahisi kukupata hata mimi mwenyewe nilijishangaa kwamba kwanini nakupiagia Rader zisizoisha wakati wapo wanaojileta wenyewe, nakumbuka ulivyokuwa ukinigomea naishia kukutukana kwa hasira lakini kesho nilirudi tena kuomba msamaha kwanza wa matusi then ndio niendelee na ku-propose kwangu, ulinisamehe kwa matusi lakini proposal was rejected.
Nilifikia hatua ya kukata tamaa, amani kwako mwanangu Andrew kokote uliko uliyeniambia niendelee kumfukuziacheupe yule bila kukata tamaa na kweli sikukoma, siku isiyotarajiwa nikakubembeleza mpaka midomo ikakauka ndipo ulipoamua kunipunguzia mateso kwa kunitamkia kuikubali proposal yangu, Ile siku nilishangilia zaidi ya mtu aliyebet timu ya mwisho kwenye mkeka wake inaposhinda dk za nyongeza kumbe nilikuwa nashangilia maumivu.
Nilishangaa sana kukuta na usichana wako, nilikuwa siamini kama kweli binti anaweza kufika chuo akiwa kajitunza hiyo ilipelekea nikuheshimu sana na kuamua kuachana na wengine wote uliowakuta huku wengine nikiwa na hakika ya kuwa walikuwa wananipenda kwa dhati wala sikujali machozi yao nikaona wale walikuwa ni njia tu ya kuja kukufikia wewe wa ubavu wangu (kumbe ulikuwa ni ubavu wa yule mwamba kwangu ilikuwa ni njia yako aisee!).
Nakumbuka ulikuwa hujui lolote kuhusu haya yanayoitwa mapenzi na mimi nikawa mwl wako mpaka ukaiva, Ulinipa masharti mengi kwa kuwa ulikuwa huniamini, kupima haka kaugonjwa sikuwahi kutamani wala kujaribu lakini mbele yako nilipima mamaa (bcoz of love you may get yourself you do things seem to be terrible before in your life) unakumbuka ulikuwa huwezi kuja gheto peke yako mpaka usindikizwe na rafiki yako lakini mwisho wa siku ilibidi uweke taulo na mswaki wako gheto siyo kwangu tena bali kwetu mimi na wewe, hukuwahi kunifilisi nilivyokuwa nakupa nilijipendekeza mimi lakini hukuwahi kuniomba, nikakupandisha wadhifa kutoka kuwa demu hadi kukuchukulia kama mke.
Nikaenda mbali mpaka kukutambulisha kwa ndg zangu mimi, kumbe siku si nyingi naenda kuonekana "SORO", chuo kizima uliitwa shem na wifi kujulikana kwangu kukakufanya uwe popular within a short period of time, tulikuwa the best couple so far kwa uzuri wako niliongozana na wewe popote.
Siku ya ajali haipigi hodi, msg yako ya TUACHANE nakumbuka nilituma vi-emoji vya kucheka nikiamini ni masihara, kumbe ulimaanisha mamaa kadri masaa yalivyoyoyoma ndivyo nilivyokuwa nagundua kuwa uko serious, hapo ndipo nilipoanza kujua what does the word "love" mean!!, maisha ya chuo yalikuwa magumu back then kwa ule mwaka wa mwisho uliji-double, kilichokuwa kinaniuma zaidi kila nikikutana na wewe mwenzangu nakuona uko happy na maisha yako unacheka kabisa (khaa! the earth surely rotates).
Niligraduate kwa tabu sana, kama Mungu angenipa akili ya darasani ya kutokana na jitahada sana basi ninge-disco, haukunihurumia na kitu nilichokuwa nasomea kuwa wasn't easy ukaniongezea na kamsalaba juu, Sema Mungu wetu sote akaona bora nikomee kwenye gentleman G.P.A kwa ule mwaka otherwise ningechekesha umati.
Maandiko uliyokuja kuyatimiza yalitimia mamaa kwa 100%, machozi yenu akina E, A, D, na wengine huko machozi yenu yalishalipwa naamini mlishasahau mpaka kufikia leo. Thanks for coming into my life Everlight nilijifunza Mengi na ulinishape kuhusu ninyi. Salute mamaa.
Last updates zako nilikutana na rafiki yako aliniambia unaitwa mama (.......) ambalo ndio jina langu sitaki kuamini kama ulimpa hilo jina kwasababu ya kunifahamu mimi bali nahisi jina la babu yake mzaa baba wa huyo mtoto nae anaitwa hivyo.
Msalimie sana huyo wajina wangu mwambie uncle wake namtakia Afya njema katika nyama na mifupa, na unakumbuka ile nadhiri niliyoiweka kwamba nikija kufanikiwa nitaitimiza?? basi mamaa Mungu ni wetu sote uwezo huo wa kuitimiza umekwishapatikana najua pengine hautaweza kuupokea wewe but as long as ni kitu ambacho hata nduguyo yeyote anaweza kunufaika nacho basi pale utakapotoa ruhusa ya nani apewe basi nitafanya hivyo, lakini nitafurahi kama atapewa wajina.
Kama haitatokea kuonana maisha mema mamaa sitapenda uteseke i pray for you to have a good life coz ni mwanamke niliyekupenda kwenye hii sayari.