SABABU KUBWA ZILIZOIFANYA SERIKALI KUJITOA KWENYE MCC-2.
Kilichofika nyuma ya MCC-2 ni zaidi ya wengi wetu tunavyooaminishwa.
Kwa kifupi Serikali ndo imekataa masharti magumu yaliyo kwenye Mkataba wa Phase tu. Miongoni mwa Masharti hayo ni Pamoja na TANESCO kujitoa kwenye uzalishji Umeme na kukabidhi jukumu hilo Kampuni ya Symbion ambayo ni Kampuni ya Kimarekani.
Lakini pia kny fedha hizo kuna fedha ambazo zimetengwa kwa ajili ya International Consultants ambao watakuwa procured na Bodi mwisho wa siku watakuwa ni Wamarekani.
Macomsultant hao watakuwa placed Wizara ya Nishati na Madini, EURA n.k na watakuwa ni sehemu kubwa ya maamuzi ya mstakabali wa Nishati nchini yakiwemo Mafuta, gesi na vyanzo vingine.
Ukiingingia kwenye mnyumbuliko/breakdown ya bajeti ya msaada huo about USD 400ml....only Usd 4m ndo zinaenda direct kwenye infrastructure za Umeme.
Kwa kifupi Serikali ya TZ imekataa masharti hayo na ndo maana juzi wakati wa uzinduzi wa Mradi wa Kinyerezi II mlisikia Presida aka Mtumbua Majipu anawatumia Salaam kuwa Serikali inatarajia kusitisha mikataba ya kununua umeme kutoka makampuni km IPTL, Symbion n.k. Ijitegemee 100% kuzalisha umeme kutoka kwenye vyanzo vyake.
Kumbukumbu zinaonyesha Kampuni ya Agreko Mkataba unaisha na serikali hairenew Mkataba mpya nao. Huo ni mfano mmojawapo.
Hivyo masuala ya Zanzibar, Cybercrime Act. Ni propaganda tu.
TULITAZAME SUALA LA MCC KIUNDANI....
Hayati Abeid Amani Karume aliwahi kusema, "Usiogope kugombana na mtu katika jambo mtakalokuja kupatana baadae". Hili la Marekani na uamuzi wa MCC ni jambo la mpito na haliwezi kuua mahusiano yetu na Marekani.
Tanzania na Marekani zinashirikiana kwa mambo mengi na MCC ni sehemu tu tena ni eneo jipya la ushirikiano. Uamuzi huu ni jaribio kwa uhuru wetu. Nasi tutalishinda kama tulivyoshinda mengine huko nyuma.
Jambo tunalopaswa kufahamu ni kuwa MCC 2 toka mwanzo imekuwa ni mtihani dhidi ya uhuru wetu. MCC 1 ilikuwa ni chambo cha kutuvuta na tulipewa bila masharti tena hela nyingi dola milioni 698 na ni fedha tulizopewa moja kwa moja na kupewa uhuru wa kuamua tuzitumieje. Tulitakiwa kuainisha maeneo kisha wao wanatoa hela. Ndio maana miradi kama ile barabara ambazo hazikuwa zikipata ufadhili kwa kuwa hazikuonekana ni za kiuchumi na miradi ya maji ya Morogoro na kwingineko iliingizwa humu na kupata ufadhili. MCC 2 sio hivyo. Kwenye MCC 2 walengwa wakubwa ni sekta binafsi ya Marekani.
Tulipoanza mchakato huu, wafanyabiashara kwa kushirikiana na Maseneta wakaanzisha hoja kuwa kwanini Marekani inatoa fedha kwa ufadhili katika nchi ambazo China ndio wenye kufaidika na fedha hizo? Wakaleta hoja ya kuwa Serikali ya Marekani ifanye jitihada ya kuweka fedha kwa kusaidia Sekta Binafsi ya Marekani kupenya Afrika.
Ukaitishwa mkutano wa US-Africa Summit na agenda kubwa ikawa Power Africa. Katika Power Africa, Marekani ikalichagua eneo la Nishati (si uzalishaji viwanda) kwa kutambua kuwa ndio eneo pekee wanaloweza kushindana na wachina. Wakasema wataelekeza fedha huko kuisaidia Afrika kutatua tatizo la nishati ambalo ndio pembejeo ya viwanda.
Wakaweka sharti kuwa fedha hizo na miradi hiyo itatekelezwa na Sekta Binafsi ya Marekani. Ndio sababu ya Rais Obama kutangazia dhamira ile pale Ubungo kwenye Mitambo ya Symbion Power.
Kuanzia hapo kumekuwepo na shinikizo kubwa sana na masharti magumu na yenye kuhamahama (shifting goal post) kutaka kuibaka sekta ya nishati nchini ikiwemo mageuzi ya TANESCO.
Zikaainishwa hatua kadhaa,ambazo utekelezaji wake baadhi ni kisheria na kisera na hivyo haziwezi kwenda kwa deadline walizotaka. Kila bodi ikikutana wanaibua hiki na kile lakini wakisema hela watatoa. Hela hizi zikawa zimeshikiliwa kama chambo ukisogelea zinasogea.
Hatimaye wakasema wanasubiri uchaguzi mkuu jambo ambalo halihusiani na madai ya mwanzoni. Baada ya uchaguzi wakaibuka na suala la Zanzibar.
Hivyo, uamuzi wao wa leo ni uamuzi uliotarajiwa. Pia ni uamuzi wenye madhara kwa sekta binafsi ya Marekani pia ambayo ndio ilikuwa itekeleze miradi hiyo.
Kama Taifa ni muhimu kulinda utu na uhuru wetu. Ndio msingi wa sera yetu ya nje toka mwanzo na hata sasa. Tumetofautiana na Marekani katika hili tutapatana katika mengine. Ndio uhai wa maisha ya diplomasia.
Tunapaswa kuheshimu uamuzi wao kama ambavyo wanapaswa kuuheshimu wetu. Hatimaye baadae tutapatana. Marekani inaihitaji Tanzania na Tanzania inaihitaji Marekani.
Marekani inahitaji MCC 2 hali kadhalika Tanzania inahitaji MCC 2. Mahusiano ya Tanzania na Marekani hayakuanza na hayataisha na MCC. MCC imeyakuta na itayaacha.
Kama marudio ya uchaguzi wa Zanzibar ndio kigezo, basi Marekani isingekuwa inatoa Dola Bilioni 3 kila mwaka kwa Egypt iliyo chini ya utawala wa kijeshi kwa sababu ya kuununua ugomvi wa Egypt na Israel na isingetoa kiasi cha dola bilioni 6 kwa Israel kila mwaka kwa yale wanayoyafanya dhidi ya Wapalestina.
Huu ni wakati ambao Taifa linawaita Wazalendo wake. Wazalendo wataitija na watasema 'Nchi yangu KWANZA, iwe Sahihi au Imekosea" na Makuwadi/vibaraka watashangilia na kusema "si mnaona sasa kiko wapi?".
#Forward kwa Wapenda Uhuru wetu.
Na Pius M. Kanssy
Mzalendo Halisi