angelita
JF-Expert Member
- Jun 13, 2013
- 3,017
- 2,446
Kila kijana au msichana anataka mwenza anayemcha Mungu, mwaminifu, mkweli, mkarimu, anayejali na mwenye upendo wa kweli. Na hayo ni mambo muhimu ya kuyatafuta kwa mwenzi wa Maisha.
Sasa cha kujiuliza kwanza ni je wewe unazo sifa zote? Je mtu akitafuta Mwenye sifa hizo unaweza kuwa mmoja wapo? Kumbuka Mungu anakupa wa kufanana naye.
Kabla hujaanza kuzunguka huku na huko, kutafuta mchumba mcha Mungu, anza leo kumcha Mungu. Haiwezekani binti au kijana unakesha bar, club na mambo Kama hayo halafu Mungu akupe mwenza mcha Mungu, Mungu hawezi kumpa mtoto wake anayemcha mtu Kama wewe, ambae haendi Kanisani, huna maombi binafsi, haufuati neno la Mungu na hauna uhusiano binafsi na Mungu.
Unataka mwenza mpole, mkarimu mwenye upendo wa kweli. Hakikisha hizo sifa unazo kwanza wewe. Jambo la kwanza la kuwa na mahusiano Imara ni kuinvest kwako kujenga kiroho chako character na muonekano. Hivyo kabla hujaangalia kushoto na kulia jiangalie kwanza wewe.