Comred Mbwana Allyamtu
JF-Expert Member
- Jun 28, 2016
- 348
- 847
UNAWEZA KUWA NA NYOTA NA USIWE NA BAHATI NA UKAWA NA BAHATI USIWE NA NYOTA.
Na. Comred Mbwana Allyamtu (CMCA)
Friday -19/02/2021
Marangu, Kilimanjaro, Tanzania
Actually iko hivyo, nyota na bahati ni vitu viwili tofauti kwenye safari ya maisha ya mwanadamu, kupata pesa ni bahati ila kuwa tajiri ni nyota, najua sijaeleweka hapa.
Any way...
Namanisha kuwa unaweza kuwa na pesa na usiwe tajiri, utajiri ni utamaduni wa kuwa na nidhamu ya pesa, muhasibu anaweza kutunza Billion's of money huku yeye akiwa masikini na akasimamia nidhamu ya fedha na kampuni isiteteleke huku yeye akilipwa laki saba kwa mwezi na akiishia kulalamika ugumu wa maisha mpaka siku anastaafu.
Hii inamaana kuwa kuitunza pesa mpaka kuwa tajiri inaitaji karma ya Mungu, no matter unaingiza pesa kiasi gani, simanishi kuwa mtu hawezi kuwa tajiri, ndio maana Bill Gates aliwahi kusema "Kuzaliwa masikini sio kosa ila kosa ni kufa masikini".
Unaweza kutengenezwa kuwa tajiri na unaweza kutengenezwa kuwa masikini, kama ambavyo matajiri wanageuzwa kuwa mashetani na masikini kuwa malaika, ila kumbuka huwezi kuwa tajiri kama huna nyota, hivi ndivo ilivyo kwenye kila kitu katika maisha ya mwanadamu.
Najua bado unastaajabu hili nalo eleza, huwezi kuwa yoyote kama huna nyota, lakini unaweza kufanya chochote ukiwa na bahati, iko hivyo.
Ebu tazama, kwa miaka 36, Maalim Seif alikuwa kwenye siasa huko Zanzibar, miaka yote hiyo alifanya siasa kutafuta uraisi, lakini Mungu hakumpa nyota ya uraisi bali Mungu alimpa bahati ya kuwa mwanasiasa bora nyakati zote Zanzibar, hata alipo shinda kwenye uchaguzi hakupewa ushindi hii ni kwasababu alikuwa na bahati ila alikosa nyota tu ya uraisi, hata alipo lazimisha aliishia umakamu rais tu, hii ndio maana halisi ya nyota na bahati.
Hii ya nyota na bahati katika maisha ya mwanadamu inamaana kubwa, ndio maana hata katika uchaguzi wa Rais Zanzibar mwaka 1985, yaani kwenye mchakato wa kupata jina la mgombea urais wa CCM, mchuano ulikuwa mkali mno baina ya Seif na Rais wa Nne wa visiwa hivyo, Idris Abdul Wakil, Kwamba Wazazibari wengi walitaka Seif ndiye awe Rais wa Zanzibar baada ya Rais Ali Hassan Mwinyi kupitishwa na Halmashauri Kuu CCM kugombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, lakini Mungu akamnyima Seif nyota ya uraisi na kumpa bahati kisha Idris Abdul Wakil akapewa nyota ndio maana hakuangaika hata kuupata uraisi, Sasa nadhani unanielewa naposema bahati na nyota.
Hata kitendo cha Abdul Wakili kupigiwa kura nyingi za hapana, bado alishida kwasababu alikuwa na nyota ya uraisi na Seif alikuwa na bahati ya uraisi.
Hicho ni kipimo tosha kuwa Seif alipendwa sana na raia wake ila alikosa nyota tu ya kuwa raisi wa nchi, ndio maana hata uchaguzi wa urais wa Zanzibar mwaka 1995, alitikisa nchi, Alitoka wa pili nyuma ya Rais wa Tano wa Zanzibar, Dk Salmin Amour Juma, katika mchuano uliokuwa mkali, yeye alidai alishinda lakini bado hakuwa raisi, kwasababu alikuwa na bahati sio nyota.
Unajua unaweza kujiuliza inakuwaje Alli Kiba anaimba vizuri kuliko Mondi, aliingia kwenye gemu mda mrefu kuliko Mondi, lakini Diamond anamzidi mafanikio Kiba? Jibu ni rahisi, ni kwamba Kiba ana bahati ya muziki ila Mondi ana 'nyota' ya muziki.
Ndivyo ilivyo kwa Lowassa na Magufuli, Magufuli alikuwa na nyota ya urais, hakuwahi kuusaka uraisi kwenye historia yake, uraisi ulimuijia tu kama kuokota dodo kwenye mkaratusi, ndio maana alipojaribu tu uraisi alisukumiziwa moja kwa moja, hii ndio maana halisi ya 'nyota', tofauti na Lowassa aliye utafuta uraisi toka 1995, alitumia nguvu zake zote, pesa zake zote ili aupate uraisi lakini bado hakuupata ni kwasababu alikuwa na bahati ya urais na sio nyota.
Ndivyo ilivyo kuwa kwa Raila Odinga, Morgan Tsvangalai wa Zimbabwe, Kiza Besige au Etienne Tsekedi, Etienne Tsekedi Wamulumba aliusaka uraisi wa Kongo toka 1993 mpaka kifo kinamkuta aliambulia Uwaziri mkuu tu, yote haya yanadhihilisha unavyoweza kuwa na bahati na kukosa Nyota.
Felix Tsekedi hakuwahi kuota ndoto za uraisi, ila nyota ndio imemfanya kuwa raisi baada ya Kabila kumuhofia Moise Katumbi hivyo akauza urais kwa Felix Tsekedi na kumchinjia baharini Martin Fayulu, hivyo Felix Tsekedi Nyota ndio imemfanya kuwa raisi nafasi ambayo hakuwahi kuiangaikia.
Sasa Basi...
Nyota ni karma na ndoto ambayo Mungu amekupangia, yani mapito kwa kile ambacho Mungu amekupangia.
Ndio maana Gerald Ford alichaguliwa kuwa mjumbe wa Baraza la Wawakilishi Marekani kwa tiketi ya Republican mwaka 1949, Baada ya kuhudumia kipindi kimoja barazani, alitamani kuwa Spika, Bahati mbaya baraza lilikuwa na wawakilishi wengi wa Democrats, Hivyo, Democrats wakawa wanatoa Spika kila baada ya miaka miwili, nataka nikuoneshe tofauti ya "Bahati" na "Nyota".
Ford akaanza kuwekeza nguvu kwenye kufanya kampeni za Republican ili chama hicho kipate wawakilishi wengi, apate kutimiza azma yake ya kuwa spika.
Kila uchaguzi Republican walipigwa na Democrats, Ford akaishia kuwa kiongozi wa upinzani (house of minority), akaanza kujikatia tamaa, ilifika mahala chama chake kumpa fursa ya kugombea ugavana au useneta, aligoma, akisema ndoto yake ni Uspika.
Baada ya uchaguzi mwaka 1972, Democrats walishinda tena wawakilishi wengi, Ford akamwambia mkewe, Betty: "Nitajaribu tena mwaka 1974, tukishinda, nitakuwa Spika miaka miwili na mwaka 1976 nitastaafu, Tukishindwa, nitabaki mwakilishi mpaka mwaka 1976 halafu nitastaafu, " Ford akaendelea kuwa kiongozi wa upinzani.
Oktoba 10, 1973, Makamu wa Rais, Spiro Agnew, alijiuzulu kwa kashfa ya rushwa, Rais aliyekuwa madarakani, Richard Nixon, alikuwa Republican, Bunge (Congress) lilitawaliwa na Democrats, Nixon ikabidi afanye mazungumzo na viongozi wa Congress kuhusu uteuzi wa Makamu wa Rais, Congress wakamwambia hakuna mwingine zaidi ya Ford, nataka uone utofauti baina ya Bahati na Nyota.
Nixon akamtangaza Ford kuwa Makamu wa Rais na kupitishwa na Congress, Ford akamwambia Betty, "Nilitamani Uspika, lakini nimepata cheo kikubwa zaidi ya usipika Nadhani Umakamu wa Rais ni cheo kikubwa kunitosha kustaafu siasa 1976".
Ila kwakuwa Nyota ni karma na ndoto ambayo Mungu amekupangia, Mwaka 1974, Congress walimkuta Nixon na hatia ya kufanya faulo kwenye uchaguzi wa mwaka 1972 uliomrejesha madarakani kwa muhula wa pili, Faulo za Nixon hujulikana kama Kashfa ya Watergate, hivyo Nixon akang'oka madarakani, na makamu wake wa Rais, Ford akawa Rais, hii ndio maana halisi ya msamiati Nyota.
Nyota ni "Hidden Power" yani nguvu iliyofichwa ndani yako, Ni nguvu ambayo unakuwa nayo wewe lakini inatokana na kudra na mipango ya Mungu, ndio maana Ford aliutaka Uspika, akapambana miaka mingi na hakuupata, Ghafla akawa Makamu wa Rais kisha Rais bila kugombea, hii ndio Nyota, Huku Maalim Seif aliutaka uraisi akapambana miaka mingi na hakuupata, Ghafla akawa Makamu wa kwanza wa Rais, hii ndio bahati.
Bahati ni jitihada zilizo beba kudura ya Mungu, ndio maana unaweza kupambania ndoto yako na usifanikiwe kwa sababu kudura za Mungu kwako ni bahati tu na sio Nyota, Sasa nadhani nimeeleweka
Nyota ndio iliyomfanya Joe Biden kurejea Ikulu ya White House, alikotumikia miaka minane akiwa makamu wa rais, baada ya kuitafuta nafasi hii kwa karibu miaka 36 wakati akilitumikia Baraza la Seneti la Marekani, huku bahati aliyokuwa nayo Hillary Clinton ndio imemfanya ikulu ya White House ibaki historia kwake kuihudumu kama Rais wa nchi.
Unaweza kuwa na ndoto, lakini isitimie kwakuwa Nyota yako haiwezi kukufanya ufanikiwe, halikadharika unaweza kufanikiwa kwakuwa una bahati ila usifikie ndoto kwakuwa Nyota yako haiwezi kukufanya ufanikiwe kwenye ndoto yako.
Kwa kupata makala Zaidi wasiliana na Mimi WhatsApp 0679555526 uungwe group la Maktaba Kuu.
Ukinakili kazi zangu kumbuka kufanya acknowledgment.
Wako Mjoli wa Historia na diplomasia ya ulimwengu.
Ndimi: Comred Mbwana Allyamtu
Copyrights of this article reserved
written by Comred Mbwana Allyamtu
•Napatika Kwa mawasliano
Comred Mbwana Allyamtu
Kwa Tanzania
+255679555526.
+255765026057.
Kwa Rwanda
+250733153930
+250788214234
Kwa DRC
+243 977 860 824
Email- mbwanaallyamtu990@gmail.com
Copyright 2021, All Rights Reserved.
Maktaba Kuu.