Unaweza kuwa bora sana, lakini ukienda nje ya field yako maisha yako yote utakua mtu wa kawaida tuu

Unaweza kuwa bora sana, lakini ukienda nje ya field yako maisha yako yote utakua mtu wa kawaida tuu

Vien

JF-Expert Member
Joined
Mar 6, 2020
Posts
7,275
Reaction score
11,775
Kila mmoja wetu amepewa talanta na kipawa cha kipekee. Lakini wengi wanapoteza muda wao wakijaribu kufanya mambo ambayo hawana uwezo nayo. Matokeo? Maisha yao yote yanakua ya wastani tu, na hata wakiondoka katika uso wa dunia hawata acha historia wala alama yoyote katika huu ulimwengu

Angalia watu waliofanikiwa kweli. Wachezaji kama Cristiano Ronaldo au Lionel Messi walitambua kuwa mpira wa miguu ndio field yao. Walijituma kila siku, wakiboresha kila kitu walichokuwa nacho, na leo hii wako kwenye kiwango cha juu duniani.

Katika muziki hususani hapa africa,Wasanii kama Burna Boy na Davido na wengineo wengi waligundua vipawa vyao vya kipekee vya kuimba na kuandika nyimbo zinazogusa mioyo ya watu. Hawa hawakujaribu kuwa wanasiasa au madaktari; walijua nini kinawapa maisha yenye maana, na walifanya kazi hiyo kwa bidii kubwa leo hii ni watu wenye hadhi ya juu

Kama biashara, fikiria Elon Musk, Aliko Dangote au Oprah Winfrey. Walitambua uwezo wao, wakapambania ndoto zao katika field ambazo zilikuwa sahihi kwao. Matokeo? Dunia inakumbuka juhudi zao, na wameshika nafasi ambazo wengi hawawezi kufikia.

Kinyume chake, kuna watu wengi wanaokosa kujua wapi wana uwezo mkubwa mwishowe wanaingia katika mambo ambayo hawana uwezo nayo, wanaingia kwenye kazi ambazo hawajazaliwa kuja kuzifanya, au kujaribu biashara ambazo hazina uhusiano na talanta zao. Hii inapelekea maisha yao yote kuwa ya wastani tu, bila na alama kubwa hapa duniani.

Tunaona mfano hapa Tanzania: kuna watu wanaopenda sana soko la mitindo, lakini hawana ubunifu au mitindo yakipekee, wanacopy tu yale yanayofanyiwa wengine. Matokeo yake hawana impact kubwa, wanabaki tu watu wa kawaida.
Lakini wengine, kama Diamond Platnumz, walitambua talanta yao, wakawekeza katika muziki na ujasiriamali wao, na leo hii wana historia inayoonekana.

Hii ni sababu kwanini ni muhimu kujua field yako na kudumisha kipawa chako. Sio tu kwaajili yako, bali pia kwa vizazi vyako. Hii ndiyo njia ya kuhakikisha tunaunda maisha yenye maana, tunabaki na legacy, na hatutakuwa tu “watu wa wastani” duniani.

Tambua field yako, jitume kwenye kipawa chako, usiruhusu shinikizo la jamii au mabadiliko yasiyo sahihi kuvuruga ndoto zako. Ukiweka juhudi zako kwenye eneo sahihi, maisha yako hayatakuwa ya wastani tu, bali utaacha historia halisi.
 
Kwenye mguu wangu wa KUSHOTO MUNGU aliweka kipaji cha ajabu kusakata mpira wa miguu.

Ni kitu nilikua situmii nguvu..nilikua nawapita watu kama messi ukija kwa fujo kunipiga rafu utashangaa u fasta wa akili na mwili..Kuna beki niliruka nao juu wakaja kunirukia nikawatoka wakagongana na kushindwa kuendelea na MECHI nilifanya mengi SANA uwanjani

Penati za maudhii free kick za hatare..nguvu speed akili ya mpira bila nguvuuuuuuuu..nilikua nalijua lango kisasa sawa nick nyingi VAN MAGORI HATAREEE

Ilikuchukua dakika kadhaa mpira ukiwa kwenye mguu wangu KUGUNDUA uwezo wa ajabu ambao ulikua kwenye miguu yangu..

Wapo walio acha shughuli zao na kuja kuniandalia wengine wengi wasio nijua walinituza pesa na wapo walio nitabiria mambo makubwa sana kwenye soka.

Mpira unge nipa pesa ungenipa mtaji unge nunua magari unge Jenga majumba ila tu Mimi enzi zetu siku uamini mpira wa miguu mpira enzi zetu mpira haukuchezwa na watoto wa vigogo, wafanya biashara hata watoto wa vibopa mpira ni mchezooo WA watoto wa ki maskini enzi zile

Nikakutanaga na brother mmoja akasema mdogo angu achana na mpira hauna future na kweli Nika acha mipira Nika kaza ELIMU

Ngoja nipumzike
 
Kwenye mguu wangu wa KUSHOTO MUNGU aliweka kipaji cha ajabu kusakata mpira wa miguu.

Ilikuchukua dakika kadhaa mpira ukiwa kwenye mguu wangu KUGUNDUA uwezo wa ajabu ambao ulikua kwenye miguu yangu..

Wapo walio acha shughuli zao na kuja kuniandalia wengine wengi wasio nijua walinituza pesa na wapo walio nitabiria mambo makubwa sana kwenye soka.

Mpira unge nipa pesa ungenipa mtaji unge nunua magari unge Jenga majumba ila tu Mimi enzi zetu siku uamini mpira wa miguu mpira enzi zetu mpira haukuchezwa na watoto wa vigogo, wafanya biashara hata watoto wa vibopa mpira ni mchezooo WA watoto wa ki maskini enzi zile

Nikakutanaga na brother mmoja akasema mdogo angu achana na mpira hauna future na kweli Nika acha mipira Nika kaza ELIMU

Ngoja nipumzike
Mkubwa pengine leo hii ungekua mchezaji mkubwa sana na ungepeperusha Flag
 
Mkubwa pengine leo hii ungekua mchezaji mkubwa sana na ungepeperusha Flag
True sitanii wachezaji wa aina yangu kwa Tanzania ni kama pacome na chama kwa level za NYUMBANI..

Nipo faster na maamuzii ya chap na akili nyingi za mpira hata niki kanyaga ardhii..kitu pekee ulikua unitoe ni mpira wa miguu ila Mimi Nika udharau pia enzi zetu mpira haukua na pesa kama Sasa..
 
Back
Top Bottom