Unaweza kukaa muda gani bila kuishika simu?

The Certified

JF-Expert Member
Feb 10, 2016
910
774
_94741490_thinkstockphotos-638883272.jpg

Unaweza kukaa muda gani bila kuwa na simu yako, kabla ya kuanza kuhangaika?

Mfano uwe umeisahau pahali, imeisha chaji au labda umelazimishwa kuizima na kuiweka mbali?

Wanasaikolojia wamegundua kwamba jibu lake litakuwa dakika chache sana - hasa iwapo umri wako ni kati ya miaka 18 na 26.
Baada ya kufanya utafiti, waligundua kwamba watu ambao walipokonywa simu walikuwa na uwezekano wa juu wa kuonyesha tabia ya "mfadhaiko" wakilinganishwa na watu walioachwa kukaa na simu zao.

Washiriki, baada ya kupokonywa simu zao, walipopewa simu - hata kama hazikuwa zao - walionesha kuwa na kiwango cha chini kidogo cha mfadhaiko.

_94742828_gettyimages-463160160.jpg

Haichukui muda kabla ya dalili za mfadhaiko kuanza kuonekana watu wanapotenganishwa na simu zao
Watafiti wanasema siku hizi watu wameanza kutumia simu kama mbadala badala ya kutangamana na watu.

Wanalinganisha na jinsi mtoto anavyotuliwa hata kwa blanketi wazazi wake wanapokuwa mbali.

Utafiti huo ulianywa na wataalamu kutoka Chuo Kikuu cha Eotvos Lorand nchini Hungary.
Veronika Konok, mmoja wa watafiti, anasema: "Binadamu anaweza kuunga uhusiano mzito sana na vifaa, na vitu kama vile picha za watu muhimu kwake, au wanasesere.

"Simu ni muhimu sana kwa sababu bali na kuwa kifaa muhimu, pia ni hutusaidia kujumuika na wengine kupitia teknolojia."

_94742827_gettyimages-631871004.jpg

Simu ya mtu mwingine inatosha kupunguzia wengi mfadhaiko
Utafiti huo ulifanywa miongoni mwa kundi la vijana wa miaka 18 hadi 26, ambao tabia zao zilinakiliwa kupitia video na mapigo yao ya moyo kupimwa.

Walipokonywa simu walionyesha dalili za mfadhaiko.

_94747236_gettyimages-628153934.jpg

Simu hufanya kazi kama kitulizo kwa binadamu
Veronika anasema anafikiri vijana wamekuwa na uhusiano mkubwa na simu zao.

"Watoto wanaotumia simu kuanzia utotoni, nafikiri uhusiano wao na simu utakuwa hata zaidi."

Matokeo yake si ya kushangaza, kwani simu yako ikiishiwa na chaji au uipoteze kwa muda, mwenyewe unfahamu kwamba unaweza kutatizika si haba.
Wasiwasi wa kuwa mbali na simu yako hata umepewa jina - unaitwanomophobia, ambao ni ufupisho wa "no-mobile-phone phobia".

Tatizo hilo huathiri vijana wanne kati ya watano kwa mujibu wa baadhi ya utafiti.
 
One hour tops....zaidi ya hapo sijawahi km simu ina chaji na bundle siwezi kukaa zaidi ya lisaa sijaishika hata nichek notifications tu
 
mimi huwa naona binadamu wa sasa na simu ni kama mwanamke wa kiafrika na magari,suala liwe linatembea tu,tosha kabisa!
 
Aidha kwa Wanafunzi hao huzitumia simu hizo za kisasa kwa karibu saa tano na nusu ya muda wao kwa siku.

Matokeo yake ni kuwa asilimia 25 ya watoto ama mmoja kati ya wanafunzi 4 ametajwa kuwa na uraibu wa simu hizo.

Simu za kisasa za mkononi katika kamataifa ya Asia zimekua kama ibaada.

Kwa mfano, nchini Japan, kuna desturi maalum ya simu za mkononi inayojulikana kama Keitai;Wanatumia simu za mikononi za kisasa kutumiana picha za chakula na vitu mbalimbali.

Lakini utumizi huu wa simu za mkononi kwa kiasi cha kupindukia umewapata baadhi yao katika mazingira yasiyo ya kawaida.
 
Niliwahi kujiuliza alietengeneza simu alikuwa na lengo gani hasa?
Kufanya biashara, kuifanya dunia iwe kama kijiji au nini haswa?
Majibu yote niliyoyafikiria sikiona kama yana faa kuwa ndio sababu ya msingi ya mawasiliano ya simu kuvumbuliwa, na kwa kuwa ni mfatiliaji mzuri wa movie za kijasusi, naamini kunasababu ya msingi ambayo hatupaswi kuifahamu sisi wafuata upepo.
Hako kaugonjwa kwa monophobia nadhani ni sehemu ya mpango wa kuvumbuliwa simu duniani, na sababu kubwa huenda ikawa ni MIND CONTROL.
WE SHOULD WORK UP, we should not be a part of others agendas.
 
Niliwahi kujiuliza alietengeneza simu alikuwa na lengo gani hasa?
Kufanya biashara, kuifanya dunia iwe kama kijiji au nini haswa?
Majibu yote niliyoyafikiria sikiona kana yana faa kuwa ndio sababu ya msingi ya mawasiliano ya simu kuvumbuliwa, na kuwa ni mfatiliaji mzuri wa movie za kijasusi, naamini kunasababu ya msingi ambayo hatupaswi kuifahamu.
Hako kaugonjwa kwa monophobia nadhani ni sehemu ya mpango wa kuvumbuliwa simu duniani,
WE SHOULD WORK UP, we should not be a part of others agendas.
Well said mkuu hata mimi najiuliza sana
 
Back
Top Bottom