Dar es Salaam: Mchakato wa ufuatiliaji simu zilizoibiwa kupitia Vituo vya Polisi una ‘harufu ya michezo michafu’

NBica

Member
Sep 13, 2010
42
40
IMEI number.jpg

Baadhi ya Watu waliotoa ripoti za kuibiwa simu katika vituo vya Polisi Stakishari Ukonga Jijini Dar es Salaam na katika Kituo cha Kilwa Roads Police wanasema kila wanapofuatilia simu zao zilizoripotiwa kuibiwa huzikuta kwa watu ambao wamezinunua kutoka kwa watu waliopewa simu hizo na maafande.

Baadhi ya Simu zinazoripotiwa kupotea hazipatikani au aliyeibiwa huzungushwa hadi kufikia hatua ya kukata tamaa na kuacha kufuatilia kutokanana na usumbufu.

Lakini kiuhalisia baadhi ya askari hufuatilia kwa urahisi kabisa simu hizi na kuzipata na baadaye huziuza kupitia mnyororo wa watu wa katikati ili wasiweze kujulikana.

WIZI WA SIMU
Wizi wa simu si jambo geni kwa Dar es Salaam lakini uwepo wa usajili wa kadi za simu na maendeleo ya teknolojia kulileta matumaini ya kwamba sasa wizi huo utapungua, kwani aliyebiwa simu ataweza kuifuatilia simu yake kupitia IMEI Namba au Application maalumu.

WhatsApp Image 2025-01-07 at 15.57.10.jpeg
Pamoja na maeneleo yote hayo kwa sasa hali ni tofauti, simu zinaibiwa na hazipatikani kwa ukubwa ule ambao ulitegemewa.

USHUHUDA
Mmoja wa waathirika wa wizi wa simu kutoka Kituo cha Kilwa Road anasema aliripoti kuibiwa simu Novemba 2023, akakabidhiwa Askari wa kufuatilia suala lake hilo kituoni hapo.

Kwa mujibu wa muathirika huyo anasema Afande anayefuatilia simu yake alimshauri kuwa itachukua muda mrefu kwani hupeleka IMEI Namba nyingi TCRA kwa ajili ya ufuatiliaji, hivyo inaweza ikachukua muda mrefu.

‘Aliniambia aniunganishe na mtu ambaye anafuatilia kupitia Application ambayo hiyo Application ni bure hatua za mwanzo lakini baadaye itakupasa ulipie, nikakubali na nikaanza kuwasiliana na huyo mtu’.

Baada ya kuanza kufuatilia aliipata katika eneo la Kimara, akatakiwa kuilipia kiasi cha Shilingi 50,000 na nauli na malipo ya huduma ni 50,000, hivyo alilipa Shilingi 100,000 ili waweze kwenda na afande anayefuatilia kesi wakamkamate lakini walipofika eneo la tukio walimkuta ndugu yake na aliawaambia huyo mtu amesafiri lakini anakaa maeneo hayo na kupewa namba ya anayetumia simu hiyo ambaye alisema yupo Mkoani.

Walipoendelea kumbana mtu huyo akasema amenunua simu hiyo kutoka kwa Mgambo ambaye huyo Mgambo aliitoa kwa Afande fulani (akamtaja kwa jina).

Kilichofuata baada ya hapo simu haikupatikana tena japokuwa mhusika bado anaifuatilia mpaka sasa kwa matumaini kidogo ya kuipata.

Kesi nyingine ya Kituo cha Stakishari, Muathirika wa wizi alipoibiwa simu alijaribu kufuatilia mwenyewe kupitia Application na kuiona simu yake lakini ilipofika hatua ya kulipia alikwama, hivyo atafute msaada wa polisi.

Askari Polisi anayefuatilia kesi yake alimtaka kulipa Sh 120,000 ili aweze kumalizia ufuatiliaji lakini baada ya kulipa na kufuatilia kwa muda mchache, polisi alidai haioni simu hiyo popote kila anapoifuatilia, hivyo kesi iliishia hapo hapo na simu haijapatikana.

HALI HALISI
Hii ni mifano ya kesi katika kesi nyingi za namna hiyo. Ufuatiliaji wa simu iliyoibiwa kwa njia ya IMEI Namba unafanya kazi vizuri na simu ina uwezo wa kupatikana kwa urahisi sana lakini changamoto ni urasimu na vikwazo kutoka kwa baadhi ya Askari ambao wanaamua kuchukua jukumu la kuuza wao simu hizo na kesi kuishia hewani.

Pia soma ~ Waziri Bashungwa: Wanaolalamika kuibiwa Simu wanakutana na Nenda rudi nyingi kituo cha Polisi
 
Hivi bado mnashangaa hawa polisi wa Tanzania na mambo yao? Tena msiwalaumu kabisa. Hivi mnadhani hawajui kuwa mtoto wa rais anapita na maburungutu ya fedha ili kuhonga wanaokosoa serikali? Kama hali iko hivyo unataka wao wafe njaa? Acha na wao wale kwa urefu wa kamba zao.
 
View attachment 3195155

Baadhi ya Watu waliotoa ripoti za kuibiwa simu katika vituo vya Polisi Stakishari Ukonga Jijini Dar es Salaam na katika Kituo cha Kilwa Roads Police wanasema kila wanapofuatilia simu zao zilizoripotiwa kuibiwa huzikuta kwa watu ambao wamezinunua kutoka kwa watu waliopewa simu hizo na maafande.

Baadhi ya Simu zinazoripotiwa kupotea hazipatikani au aliyeibiwa huzungushwa hadi kufikia hatua ya kukata tamaa na kuacha kufuatilia kutokanana na usumbufu.

Lakini kiuhalisia baadhi ya askari hufuatilia kwa urahisi kabisa simu hizi na kuzipata na baadaye huziuza kupitia mnyororo wa watu wa katikati ili wasiweze kujulikana.

WIZI WA SIMU

Wizi wa simu si jambo geni kwa Dar es Salaam lakini uwepo wa usajili wa kadi za simu na maendeleo ya teknolojia kulileta matumaini ya kwamba sasa wizi huo utapungua, kwani aliyebiwa simu ataweza kuifuatilia simu yake kupitia IMEI Namba au Application maalumu.

View attachment 3195158
Pamoja na maeneleo yote hayo kwa sasa hali ni tofauti, simu zinaibiwa na hazipatikani kwa ukubwa ule ambao ulitegemewa.

USHUHUDA

Mmoja wa waathirika wa wizi wa simu kutoka Kituo cha Kilwa Road anasema aliripoti kuibiwa simu Novemba 2023, akakabidhiwa Askari wa kufuatilia suala lake hilo kituoni hapo.

Kwa mujibu wa muathirika huyo anasema Afande anayefuatilia simu yake alimshauri kuwa itachukua muda mrefu kwani hupeleka IMEI Namba nyingi TCRA kwa ajili ya ufuatiliaji, hivyo inaweza ikachukua muda mrefu.

‘Aliniambia aniunganishe na mtu ambaye anafuatilia kupitia Application ambayo hiyo Application ni bure hatua za mwanzo lakini baadaye itakupasa ulipie, nikakubali na nikaanza kuwasiliana na huyo mtu’.

Baada ya kuanza kufuatilia aliipata katika eneo la Kimara, akatakiwa kuilipia kiasi cha Shilingi 50,000 na nauli na malipo ya huduma ni 50,000, hivyo alilipa Shilingi 100,000 ili waweze kwenda na afande anayefuatilia kesi wakamkamate lakini walipofika eneo la tukio walimkuta ndugu yake na aliawaambia huyo mtu amesafiri lakini anakaa maeneo hayo na kupewa namba ya anayetumia simu hiyo ambaye alisema yupo Mkoani.

Walipoendelea kumbana mtu huyo akasema amenunua simu hiyo kutoka kwa Mgambo ambaye huyo Mgambo aliitoa kwa Afande fulani (akamtaja kwa jina).

Kilichofuata baada ya hapo simu haikupatikana tena japokuwa mhusika bado anaifuatilia mpaka sasa kwa matumaini kidogo ya kuipata.

Kesi nyingine ya Kituo cha Stakishari, Muathirika wa wizi alipoibiwa simu alijaribu kufuatilia mwenyewe kupitia Application na kuiona simu yake lakini ilipofika hatua ya kulipia alikwama, hivyo atafute msaada wa polisi.

Askari Polisi anayefuatilia kesi yake alimtaka kulipa Sh 120,000 ili aweze kumalizia ufuatiliaji lakini baada ya kulipa na kufuatilia kwa muda mchache, polisi alidai haioni simu hiyo popote kila anapoifuatilia, hivyo kesi iliishia hapo hapo na simu haijapatikana.

HALI HALISI

Hii ni mifano ya kesi katika kesi nyingi za namna hiyo. Ufuatiliaji wa simu iliyoibiwa kwa njia ya IMEI Namba unafanya kazi vizuri na simu ina uwezo wa kupatikana kwa urahisi sana lakini changamoto ni urasimu na vikwazo kutoka kwa baadhi ya Askari ambao wanaamua kuchukua jukumu la kuuza wao simu hizo na kesi kuishia hewani.
Mimi nashauri yafuatayo
  1. Utengenezwe mfumo na Mamlaka za mawasiliano ikibidi kiwe kitengo ndani ya TCRA,
  2. Wananchi wakiibiwa wajaze form online ikionyesha detais za mmiliki na simu yake polisi na mmiliki wasijuane
  3. Boss wa polisi awape kazi polisi watrack hizo simu, utendaji wao upimwe kwa idadi ya simu zitakazokamatwa
  4. Mwananchi aarifiwe kufuata simu yake sehemu maalumu bila usumbufu
 
Nilimbulia kuchambua namba za simu na kupigishwa simu almost 500 za watu aliowasiliana nao na ndugu zake bila mafanikio...nkajisemea labda kwa kuwa sikutoa chochochote ila siwezi kuibiwa mara mbili nkapotezea...kwa kweli sijawahi shudia mtu kafanikiwa kwa hilo suala ni ujanja ujanja tu
 
Polisi wala rushwa,juzi tu wamerekodiwa wakipokea rushwa hazarani. Ndo uwaamini wakutafutie simu yako,kila mtu achunge mzigo wake ukiibiwa ndo kwisha hiyo nunua nyingine.
 
Nilimbulia kuchambua namba za simu na kupigishwa simu almost 500 za watu aliowasiliana nao na ndugu zake bila mafanikio...nkajisemea labda kwa kuwa sikutoa chochochote ila siwezi kuibiwa mara mbili nkapotezea...kwa kweli sijawahi shudia mtu kafanikiwa kwa hilo suala ni ujanja ujanja tu
Mimi nishawahi kushuhudia, kuna bint yetu alitoroka shule akaiba simu ya bibi yake, ilikuwa dodoma kondoa. Tulipoenda polisi tulitoa 50,000 tukaitrack simu yake, na baadaye tukatoa tena 50,000 kuitrack namba ya huyo mtu aliekuwa kamtorosha..
Tuliwakamatia temeke mikoroshini
 
Mimi nashauri yafuatayo
  1. Utengenezwe mfumo na Mamlaka za mawasiliano ikibidi kiwe kitengo ndani ya TCRA,
  2. Wananchi wakiibiwa wajaze form online ikionyesha detais za mmiliki na simu yake polisi na mmiliki wasijuane
  3. Boss wa polisi awape kazi polisi watrack hizo simu, utendaji wao upimwe kwa idadi ya simu zitakazokamatwa
  4. Mwananchi aarifiwe kufuata simu yake sehemu maalumu bila usumbufu
Hapa utakuwa umehamisha tu ulaji kutoka kwa polisi na kuwapa shavu TCRA bado mambo yataendelea vilevile
 
Baadhi ya Watu waliotoa ripoti za kuibiwa simu katika vituo vya Polisi Stakishari Ukonga Jijini Dar es Salaam na katika Kituo cha Kilwa Roads Police wanasema kila wanapofuatilia simu zao zilizoripotiwa kuibiwa huzikuta kwa watu ambao wamezinunua kutoka kwa watu waliopewa simu hizo na maafande.

Baadhi ya Simu zinazoripotiwa kupotea hazipatikani au aliyeibiwa huzungushwa hadi kufikia hatua ya kukata tamaa na kuacha kufuatilia kutokanana na usumbufu.

Lakini kiuhalisia baadhi ya askari hufuatilia kwa urahisi kabisa simu hizi na kuzipata na baadaye huziuza kupitia mnyororo wa watu wa katikati ili wasiweze kujulikana.

WIZI WA SIMU
Wizi wa simu si jambo geni kwa Dar es Salaam lakini uwepo wa usajili wa kadi za simu na maendeleo ya teknolojia kulileta matumaini ya kwamba sasa wizi huo utapungua, kwani aliyebiwa simu ataweza kuifuatilia simu yake kupitia IMEI Namba au Application maalumu.

Pamoja na maeneleo yote hayo kwa sasa hali ni tofauti, simu zinaibiwa na hazipatikani kwa ukubwa ule ambao ulitegemewa.

USHUHUDA
Mmoja wa waathirika wa wizi wa simu kutoka Kituo cha Kilwa Road anasema aliripoti kuibiwa simu Novemba 2023, akakabidhiwa Askari wa kufuatilia suala lake hilo kituoni hapo.

Kwa mujibu wa muathirika huyo anasema Afande anayefuatilia simu yake alimshauri kuwa itachukua muda mrefu kwani hupeleka IMEI Namba nyingi TCRA kwa ajili ya ufuatiliaji, hivyo inaweza ikachukua muda mrefu.

‘Aliniambia aniunganishe na mtu ambaye anafuatilia kupitia Application ambayo hiyo Application ni bure hatua za mwanzo lakini baadaye itakupasa ulipie, nikakubali na nikaanza kuwasiliana na huyo mtu’.

Baada ya kuanza kufuatilia aliipata katika eneo la Kimara, akatakiwa kuilipia kiasi cha Shilingi 50,000 na nauli na malipo ya huduma ni 50,000, hivyo alilipa Shilingi 100,000 ili waweze kwenda na afande anayefuatilia kesi wakamkamate lakini walipofika eneo la tukio walimkuta ndugu yake na aliawaambia huyo mtu amesafiri lakini anakaa maeneo hayo na kupewa namba ya anayetumia simu hiyo ambaye alisema yupo Mkoani.

Walipoendelea kumbana mtu huyo akasema amenunua simu hiyo kutoka kwa Mgambo ambaye huyo Mgambo aliitoa kwa Afande fulani (akamtaja kwa jina).

Kilichofuata baada ya hapo simu haikupatikana tena japokuwa mhusika bado anaifuatilia mpaka sasa kwa matumaini kidogo ya kuipata.

Kesi nyingine ya Kituo cha Stakishari, Muathirika wa wizi alipoibiwa simu alijaribu kufuatilia mwenyewe kupitia Application na kuiona simu yake lakini ilipofika hatua ya kulipia alikwama, hivyo atafute msaada wa polisi.

Askari Polisi anayefuatilia kesi yake alimtaka kulipa Sh 120,000 ili aweze kumalizia ufuatiliaji lakini baada ya kulipa na kufuatilia kwa muda mchache, polisi alidai haioni simu hiyo popote kila anapoifuatilia, hivyo kesi iliishia hapo hapo na simu haijapatikana.

HALI HALISI
Hii ni mifano ya kesi katika kesi nyingi za namna hiyo. Ufuatiliaji wa simu iliyoibiwa kwa njia ya IMEI Namba unafanya kazi vizuri na simu ina uwezo wa kupatikana kwa urahisi sana lakini changamoto ni urasimu na vikwazo kutoka kwa baadhi ya Askari ambao wanaamua kuchukua jukumu la kuuza wao simu hizo na kesi kuishia hewani.
Huu mchezo niliwahi kuchezewa mwaka 2015.
Niliibiwa simu kwa kukwapuliwa na bodaboda nilipoenda kuripoti polisi nikapewa mpelelezi wa kuifuatilia simu yangu.
Na yule afande alinishtua akaanza kuniuliza maswali.
Afande:Simu yako ni Samsung nyeusi?
Mimi:ndiyo
Afande:Hiyo simu yako ina kioo kipana na kwa juu kina kreki
Mimi:ndiyo
Baada ya hapo nikapata uhakika kwamba simu yangu ameiona mahali maana alama alizozitaja ndio vilevile simu yangu ilivyo alipatia kila kitu.
Baadae akaniambia nimpe 100,000Tsh ashughulikie kuitafuta nikalipa baada ya hapo ikawa ni danadana tu na sikuipata.
Kwa hiyo haya mambo siku nyingi yapo.
 
Wakuu bado tulie na taaluma za maadkali wetu. Asilimia kubwa kigezo cha kuingilia jeshini la askari ni division form four na polisi wengi hawaendi kusoma mishahara yao ipo chini toka 2018 mpaka 2021 ana v3 tu. Ni jeshi la mbumbu kiasi wao kukubali amri tu basi
 
Naomba kuuliza police anae anza kazi analipwa bei gani na senior analipwa bei gan?? Kwa salary scale ya TZ achana na allowance zingine??
 
Mimi sijawahi kuwa na Imani Na Polisi kwenye ufatiliaji wa Kitu Kilichopotea kabisa huwa sitaki hata kupoteza senti tano kwenye huo Mchakato i would rather go and buy new equipment mana Kusema ufatilie na Police ni wastage of time and resources
 
Naomba kuuliza police anae anza kazi analipwa bei gani na senior analipwa bei gan?? Kwa salary scale ya TZ achana na allowance zingine??
unataka ujue chanzo kwa nini wanapenda rushwa sio?Chanzo cha rushwa sio mishahara yao midogo bali mfumo mzima wa kiutendaji ndani ya jeshi hili na nchi kwa ujumla.
 
Data hizo ziingizwe kwenye mtandao walio ibiwa aweze kuona updates na Jina la afande husika na aliye pokea I app rejeshwa na mengi zaidi

Itawabana tuuuuu
 
Back
Top Bottom