Hiyo mchepuko ni noma hiyo sema jamaa wamekosa tu uwekezaji ila wanajitahidi sana kuigiza uhalisia wa maisha ya mtaani.
Nacho wapendea hao jamaa huwa hawataki kufanya igizo ndani ya igizo.
Mfano Movie inazungumzia ishu ya drugs na wahalifu walioshindikana mtaani zile script zote za ma gangster wakiwa wanatupiana maneno makali huwa yanatajwa kama yalivyo ili kusadifu uhalisia wa maisha ya kweli pindi inapotokea scenario kama hiyo.
Kwangu mimi haiwezi ku make sense naangalia movie au series ya watu wahuni wa mtaani wapo katikati ya ugomvi wameshikiana visu wanataka hadi kuuana wanatupiana maneno ya "mjinga wewe", "mpumbavu", "hauna akili"