Unavyoweza kujikinga na programu/software bandia | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Unavyoweza kujikinga na programu/software bandia

Discussion in 'Tech, Gadgets & Science Forum' started by Yona F. Maro, Jun 3, 2010.

 1. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #1
  Jun 3, 2010
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  [FONT=&quot]UNAVYOWEZA KUJIKINGA NA PROGRAMU/SOFTWARE BANDIA [/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot]Yona Fares Maro [/FONT]
  [FONT=&quot]May 2010[/FONT]
  [FONT=&quot]www.ictpub.blogspot.com [/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot]Inasemekana Utumiaji wa Programu/Leseni bandia umesababisha hasara ya zaidi ya dola bilioni 50 kwa mwaka uliopita kati ya hizo 10 zimepotea kwa nchi zilizo amerika ya kaskazini . Kwa Ulaya ya kati na Mashariki ni zaidi ya 66 ya programu zinazotumika zinaleseni bandia ,Kwenye Baadhi ya nchi Bara Asia na Ulaya mashariki zaidi ya Asilimia 90 ya programu zinazotumika ni bandia .[/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot]Hii haijumuishi zile programu za bure na zingine ambazo zinatolewa kwa ajili ya shuguli za taasisi mbalimbali haswa za elimu kama mashule na vyuo , inasikitisha kuona kwamba taasisi zetu nyingi nchini hazijaanza bado kunufaika na baadhi ya programu zinazotolewa bure na baadhi ya kampuni kwajili ya matumizi yao ya kila siku .[/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot]Mpaka ninavyoandika sasa hivi kuna baadhi ya bidhaa za programu zimeacha kutengenezwa kutokana na tatizo hili sugu au baadhi ya bidhaa zimeacha kuendelezwa kutokana na kuibiwa leseni na aina nyingine ya hati miliki kwenye programu hizo na baadhi ya kampuni zimekufa au kufungwa .[/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot]Nchi zetu zinazoendelea ndio ziko kwenye hatua za mwanzo kwenye maendeleo ya Teknohama lazima serikali za nchi hizi kufanya utaratibu wa kushugulikia suala hili mapema zaidi kabla hali haijawa mbaya zaidi mfano nchini Kenya baadhi ya watu walikamatwa mwezi uliopita kwa tuhuma za kuhusika kwenye ulanguzi wa programu bandia na wameshafikishwa mahakamani .[/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot]Kwa Tanzania miaka michache iliyopita kuna makundi ya watu waliwahi kukamatwa huko nyuma kutokana na hujuma hizi haijulikani kesi zao ziliendeleaje lakini baadhi ya maduka yaliyokuwa yanauza programu/leseni hayo yamebadilisha majina na kuendelea kufanya kazi kama kawaida .[/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot]Kuna njia kama 2 hivi hivi za haraka ambazo mtu anaweza kugundua kwa urahisi nyingine unaweza kusoma kwenye mtandao kuweza kutambua .[/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot]1 – Kwa sasa programu nyingi zinahitaji mtumiaji kuunganisha kompyuta yake kwenye mtandao ili aweze kusajili programu hiyo akishafanya hivyo afahamike na aweze kupatiwa huduma zingine za kuboresha programu hiyo siku za baadaye , Sasa kama yako hujasajili kwa njia ya mtandao au kama unaleseni yake ni vizuri uchomeke kwenye mtandao kudhibitisha kama kweli leseni ni halali .[/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot]2 – Hata kama Ukiunganisha kwenye mtandao kuna baadhi ya wahalifu ambao wanauza au kuweka programu hizi kwenye kompuya za watu wanawaandikia au kuwaambia wateja wao cha kufanya ili asiweze kutambulika mfano programu hiyo itazimwa sehemu ya kufanya updates au kuwasiliana unapochomeka kwenye mtandao Kama programu yako iko kwa mfumo wa CD jaribu kuangalia kama kuna vitu kama crack , Keygen , Activator ,SerialGen Ukiwa na antivirus nzuri huwa inafuta Vitu hivyo moja kwa moja .[/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot]3 – Kwa wale watumiaji wa Bidhaa za Autodesk bidhaa yao Maarufu ni AUTOCAD kuna kitu kinaitwa Dynamic Blocks hizi huwezi kuzipata au haziweza kufanya kazi vizuri kwa mfano umeweka milango kwenye mchoro wa nyumba , ukiwa na Leseni bandia Programu haitoweza Kuhesabu milango , Lakini ukiwa na halali itaweza fanya hivyo [/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot]4 – Njia hii ya mwisho bado iko kwenye Utata wa kisheria kwa sababu unahusiana zaidi na kitu kinachoitwa CLOUD COMPUTING ambapo Taasisi au watu wanaweza kufanya kazi popote duniani kuhusu Kazi vitu vyao vingine vikiwa vimehifadhiwa kwenye Komputa zingine mbali na hapo , hii bado inasumbua wengi kwenye masuala ya leseni na masuala mengine ya usalama kwa watu wanaowasiliana au kufanya kazi kwa njia hii hata hivyo ndipo tunapoenda huko .[/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot]Njia hizo nilizotaja hapo juu hazihusiki pale kwa mfano komputa yako inapokuwa na matatizo mengine kama baadhi ya vitu haviko sawa mfano mfumo wa saa kwenye komputa yako ukiwa tofauti unaweza kupata tabu ya usajili ya programu zako kwa njia ya mtandao , ingawa kuna baadhi ya programu ambazo hazina tatizo kwenye saa unapotaka kusajili .[/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot]Kama huamini Nenda www.filehippo.com Nenda kwenye Antivirus Tafuta AVG 9.0 Weka kwenye komputa yako itakwambia unatakiwa ufanye updates badilisha muda weka tarehe na mwaka 2009 utaona inakwambia Antivirus yako iko updated hilo ni tatizo kubwa kwenye AVG kwa kipindi kirefu hata Kampuni la Microsoft liliwahi kuwa na Tatizo Hili kwenye matoleo yake fulani ya Windows XP .[/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot]Kuna baadhi ya nchi duniani baadhi ya kampuni zinaogopa kuwekeza katika masuala ya teknohama haswa kwenye masuala ya programu kwa sababu ya nchi hizo kuwa na tatizo hili na hata serikali za nchi hizo hazijaamua kwa kiasi kikubwa kuwekeza haswa kuwa na sheria kali za masuala haya .[/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot]Utumiaji wa Programu/Leseni bandia ni aina ya wizi Kwa nchi ya marekani Mtu anayekamatwa na kosa hilo faini yake ni zaidi ya dola Alfu 25 na miaka 5 Jela pia humlazimisha mtuhumiwa kulipia bei mara tatu ya gharama nzima ya programu hiyo ambayo amekamatwa nayo kwa kufanya uhalifu huo Kwa habari zaidi unaweza kuangalia No Electronic Theft Act , Digital Millienium Copyright Act , Copyright Act, Title 17 of the U.S. Code[/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot]Ingawa kwa kufanya hivi wahalifu wamesaidia kwa kiasi kikubwa kuleta ushindani katika njia za kulinda leseni na programu hizo kwenye masoko lakini pia umesahabisha programu nyingi kuwa bei gali kutokana na kuwekeza kwenye suala hilo kuu sana .[/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot]Kwenye somo langu lililopita niliwaambia wazazi wachunge watoto na vijana wao wanaochukuwa programu na vingine toka kwa rafiki zao kwenda kuweka kwenye kompyuta za nyumbani pia kampuni ziwe na miongozo yake ya kiteknohama inayoweza kusaidia kupunguza tatizo hili [/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot]Leo hii kuna mambo kidogo ya kuongezea haswa kwa kampuni na mashirika ambayo yanategemea sana TEKNOHAMA kwenye shuguli zao za kila siku .[/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot]1 – Kutumia kampuni zilizohuru Kufanya uchunguzi wa masuala ya Programu na leseni za programu unazotumia kwenye shirika au kampuni yako .[/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot]2-[FONT=&quot] [/FONT][/FONT][FONT=&quot]Mnatakiwa kuwa na mfumo wa kuhifadhi kumbukumbu za programu na leseni za programu mnazonunua kwa ajili ya kazi na shuguli zenu mbalimbali .[/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot]3-[FONT=&quot] [/FONT][/FONT][FONT=&quot]Mnatakiwa kuelimisha wafanyakazi na watumiaji wengine wa rasilimali hizo huko makazini kuhusu suala hili[/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot]4-[FONT=&quot] [/FONT][/FONT][FONT=&quot]Kwa kuwa mtakuwa na miongozo ya kiteknohama ni vizuri wafanyakazi wote wakubaliane na muongozo huo kwa kuingia mkataba na kampuni au shirika lako na kupatiwa adhabu kali endapo itabainika amekwenda kinyume na makubaliano [/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot]5-[FONT=&quot] [/FONT][/FONT][FONT=&quot]Kwa mashule na taasisi zingine za kielimu mnatakiwa kuwaweka wanafunzi na wafanyakazi wenu sawa tatizo hili limeenea sana mashuleni na kwenye taasisi za elimu ya juu nchini wakati kuna kampuni zinazotoa programu nyingi bure au kwa gharama nafuu zaidi kwa ajili ya wanafunzi na taasisi hizo za elimu .[/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot]Kwa msaada zaidi na maelezo tembelea FAST The Federation Against Software Theft , SIIA The Software & Information Industry Association (SIIA), CAAST The Canadian Alliance Against Software Theft (CAAST) , Business Software Alliance (BSA) , World Intellectual Property Organization, U.S. Patent and Trademark Office.[/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot]Kwa kumalizia tu niwakumbushe watu hata unavyotumia programu kwenye eneo ambalo leseni yake haijapangiwa huko ujue nalo ni kosa kwa mfano Wizara ya Afya inaamua kununua Operating system kwajili ya Wizara hiyo lakini mfanyakazi ambaye si mwaminifu anachukuwa baadhi na kwenda kuweka kwenye komputa zake mitaani hata kama leseni ni halali lakini imewekwa sehemu ambayo si yake kwahiyo ni kosa .[/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot]Huko nyuma Niliwahi kushauri Mashirika Ya kiserikali Kuingia makubaliano na kampuni zinazozalisha programu hizi kwajili ya kuuziana programu na huduma zingine maalumu kwajili ya shirika au wizara husika tu kutumia njia hii itasaidia sana kupunguza uhalifu kwa sababu mtu hatoweza kutumia Programu nje ya mipaka yake ya kazi na kutakuwa na uhakika wa usalama .[/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot]Kama[/FONT][FONT=&quot] una maswali maoni na cha kuongeza unaweza kuchangia utakapokuta Ujumbe huu kwenye kurasa za Mtandao wowote wa Mtandao .[/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot]Yona Fares Maro [/FONT]
  [FONT=&quot]May 2010[/FONT]
  [FONT=&quot]www.ictpub.blogspot.com [/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
   
Loading...