Unataka tuwe wazalendo wakati tunabaguliwa na kuishi kama raia daraja la 3? Acha ubaguzi, ukandamizaji na uonevu kwanza!

chiembe

JF-Expert Member
May 16, 2015
12,002
20,661
Siku hizi kumeibuka kundi la watu likisihi watanzania tuwe wazalendo

Uzalendo ni zao la jinsi unavyoishi na watu unaotaka wawe wazalendo!

Kama ndani ya taifa moja wana ccm wana haki kuliko wa vyama vingine,unatarajia wale wa vyama vingine watakuwa na upendo na nchi yao? Kama wabunge wa ccm wanaenda watakako wanafanya mikutano sehemu yoyote ya nchi bila kukamatwa na polisi,lakini wapinzani wanakamatwa,je katika mazingira haya unataka au unatarajia uzalendo?

Hapo tayari taifa limegawanyika mapande mawili,wale UZALENDO TUMBO/MASLAHI,hawa ni wale watoto wapendwa(sio wa kambo) hawabaguliwi,hawalishwi makombo,na WANATUSIHI TUWE WAZALENDO ili chakula chao kisiingie mchanga waendelee kula

Wengi wanaosihi uzalendo,ukiwachunguza ni watu wanaofaidika na mfumo uliopo(status quo)nadhani hata enzi ya biashara ya utumwa,waliokuwa wanafaidika nayo waliwaita waliokuwa wanaipinga "si wazalendo" uzalendo ni neno linalotumika na wanasiasa kama kichaka

Hivi Wazanzibari wanaoona figisu za uonevu dhidi ya CUF unatarajia na unawaomba wawe wazalendo? Uzalendo ni tunda la haki,tenda haki kwa wananchi uone kama hawatakuwa wazalendo wa kutupwa,nani asiyejua kwamba wanayofanyiwa CUF ni uonevu? Hawa unatarajia wawe wazalendo au waanze movement ya kuirudisha Zanzibar yao(hapa tayari uzalendo wa kuipenda jamhuri ya muungano unatoweka kwa kuwa Taasisi za Tanganyika ndizo zimekalia haki ya CUF)

Hivi unatarajia uzalendo kwa jinsi bunge linavyoendeshwa?

Mwisho,kuna uzalendo kuliko kufata katiba na sheria? Kufata katiba na sheria ndio uzalendo ambao kama taifa TULIJIWEKEA KAMA KIPIMO CHETU CHA JUU,mengine ni kuongeza tu,je tunafata katiba na sheria,

Maana kuna msemo kwamba SAMAKI HUOZA KUANZIA KICHWANI,yanayotokea tarime ,au kumkamata Mwalimu ambaye yeye/mwanafunzi wake hajui jina la mkuu wa wilaya,je ni ishara sasa uozo wa samaki wetu umetapakaa?

Uzalendo ni nini?
 
Uzalendo ni kujenga International airport Chattle,TRA office,Taa za Barabara, kivuko hata kama vitu hivyo having value for money as long as vimejengwa Chattle lazima tupige makofi.

Uzalendo ni kukubali upumbavu wote unaofanywa na serikali kama kuwabomolea RAIA wake nyumba,kufilisi wazawa,kujenga chuki,ubaguzi na visasi.Kuvunja mikataba hovyo hivyo,kuvunja sheria na Katiba ukiyapigia haya makofi basi lazima utaitwa Mzalendo
 
Uzalendo my foot!!Tena nikikuta mtu anaiba mali ya Serikali namlipa kabisa aendelee kuiba.Wao watuibie na kutumia kodi zetu vibaya alafu leo waje kutuambia tuwe wazalendo,labda kama kuwa mzalendo nalipwa nitakuwa.
 
Siku hizi kumeibuka kundi la watu likisihi watanzania tuwe wazalendo

Uzalendo ni zao la jinsi unavyoishi na watu unaotaka wawe wazalendo!

Kama ndani ya taifa moja wana ccm wana haki kuliko wa vyama vingine,unatarajia wale wa vyama vingine watakuwa na upendo na nchi yao? Kama wabunge wa ccm wanaenda watakako wanafanya mikutano sehemu yoyote ya nchi bila kukamatwa na polisi,lakini wapinzani wanakamatwa,je katika mazingira haya unataka au unatarajia uzalendo?

Hapo tayari taifa limegawanyika mapande mawili,wale UZALENDO TUMBO/MASLAHI,hawa ni wale watoto wapendwa(sio wa kambo) hawabaguliwi,hawalishwi makombo,na WANATUSIHI TUWE WAZALENDO ili chakula chao kisiingie mchanga waendelee kula

Wengi wanaosihi uzalendo,ukiwachunguza ni watu wanaofaidika na mfumo uliopo(status quo)nadhani hata enzi ya biashara ya utumwa,waliokuwa wanafaidika nayo waliwaita waliokuwa wanaipinga "si wazalendo" uzalendo ni neno linalotumika na wanasiasa kama kichaka

Hivi Wazanzibari wanaoona figisu za uonevu dhidi ya CUF unatarajia na unawaomba wawe wazalendo? Uzalendo ni tunda la haki,tena haki kwa wananchi uone kama hawatakuwa wazalendo wa kutupwa,nani asiyejua kwamba wanayofanyiwa CUF ni uonevu? Hawa unatarajia wawe wazalendo au waanze movement ya kuirudisha Zanzibar yao(hapa tayari uzalendo wa kuipenda jamhuri ya muungano unatoweka kwa kuwa Taasisi za Tanganyika ndizo zimekalia haki ya CUF)

Hivi unatarajia uzalendo kwa jinsi bunge linavyoendeshwa?

Mwisho,kuna uzalendo kuliko kufata katiba na sheria? Kufata katiba na sheria ndio uzalendo ambao kama taifa TULIJIWEKEA KAMA KIPIMO CHETU CHA JUU,mengine ni kuongeza tu,je tunafata katiba na sheria,

Maana kuna msemo kwamba SAMAKI HUOZA KUANZIA KICHWANI

Uzalendo ni nini?

U are absolutely right. Nyerere aliwahi kutuonya Dhambi ya ubaguzi ni mbaya kama kula nyama ya mtu kwamba mla hali mara moja na athari zake ni za muda mrefu sana. ukiangalia haraka haraka kwa jinsi mambo yanavyoendeshwa hapa nchini kwetu nyakati hizi kuna ubaguzi mkubwa sana tena wa waziwazi.

Sasa sijui huo uzalendo utatoka wapi kwa wale wanaonekana kwamba hawastahili kufaidi matunda ya nchi yao na kama sio kuwajengea chuki wale wanaoonekana kuwa wana haki ya kufaidi rasilimali kuliko wengine?! hii nchi ni yetu sote na ujenzi wake unatuhitaji sote kwa pamoja lakini kama kuna system imetengenezwa kuwaumiza watu fulani kwa kuwafaidisha au kuwapendelea wengine basi hatufiki popote kimaendeleo na kibaya zaidi hata maadui zetu wa kiuchumi wameshaligundua hilo na wanatumia mgawanyiko wetu kutugonga kila pande.

VIONGOZI wana tofauti kubwa sana sana sana na WATAWALA.Na kwa nchi kama ya kwetu hii na rasilimali tulizonazo tulihitaji VIONGOZI zaidi kuliko WATAWALA.kazi kwetu.
 
Uzalendo my foot.

_20170822_085648.JPG

Mnawabagua wengine kwa itikadi halafu mnataka uzalendo, Bulaya kaenda kuchangia ujenzi wa shule unamkamata, huku kina Musukuma wakifanya mikutano majimbo wanayotaka, leo CCM wanadai uzalendo, wa Canada waje tu nitawaonyesha na ndege zingine zilipo.
 
Uzalendo gani wa raia kutekwa nyara mchana kweupe?
Uzalendo gani wa Makonda kujiona kama mungu wa pili?
Uzalendo gani wa ukabila?
Uzalendo gani wa kufuta hata RB za polisi?
Uzalendo gani wa kuzihonga mahakama ziwaonee raia?
Uzalendo gani wa mkuu wa mkoa kuvamia vituo vya utangazaji(tv stations) na silaha?.
Uzalendo gani mkuu wa mkoa kaiba vyeti rais wa nchi anamlinda?
Hakuna uzalendo bila HAKI!!
 
Back
Top Bottom