Unataka Kutajirika? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Unataka Kutajirika?

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by eRRy, Dec 26, 2009.

 1. eRRy

  eRRy JF-Expert Member

  #1
  Dec 26, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 1,080
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  KUNA mawazo mengi ya biashara duniani yanayoweza kutuondoa kwenye umasikini na kutuweka huru! Hasa kwenye nchi za Ulimwengu wa Tatu ambako kuna matatizo mengi, pia kuna biashara nyingi! Huu kwangu ni ukweli. Hivyo, unachotakiwa kufanya ndugu msomaji wangu ni kutafuta tatizo katika jamii unayoishi ndani yake na kulitafutia suluhisho, ukishalipata tayari utakuwa umeshapata biashara yako.

  Ni lazima ukumbuke si lazima wazo liwe jipya, baadhi yetu kila siku tunatafuta mawazo mapya, chukua hata mawazo ya zamani kisha uyaongezee thamani, watu wataona ni kitu kipya na watakimbilia kwako kukinunua na utapata fedha.

  Hebu chukua mfano wa mlango wa nyumba, hilo si wazo jipya, kila mmoja wetu anajua mlango ni mahali pa kutokea au kuingilia ndani ya nyumba au kitu chochote na milango ilikuwepo tangu enzi zile za Nuhu akijenga Safina, lakini kuna watu wakaja kuuongeza thamani kidogo mlango kwa kutengeneza milango iitwayo Automatic Doors, yaani milango ya kufunguka yenyewe.

  Watu hawa waligundua tatizo kwamba watu wengi wamekufa wavivu kufungua milango sababu ya kuongezeka kwa shughuli duniani, wao wakatengeneza mlango ambao hufunguka mara tu mtu akisimama mbele yake, je, hawakufanya biashara? Tayari watu hawa walitengeneza mamilioni ya dola na hivi ninavyoandika waraka huu ni matajiri wakubwa.

  Hiki ndicho ninachotaka tufanye, ni lazima tufanye kila kinachowezekana kupata wazo la biashara na njia ya kupata wazo hilo ni kugundua tatizo na kulitafutia ufumbuzi! Watu wengi duniani wanafikiri kikwazo kikubwa cha mafanikio yao ni mtaji, ndiyo maana kila mtu ukikutana naye na kumuuliza tatizo lako ni nini? Atakujibu “Mtaji” ukimuuliza tena “Shilingi ngapi zinatosha?” Atakujibu “Milioni moja” na ukimwongezea swali jingine “Ukishazipata utafanya nini?” Atakujibu “Nitaangalia sasa.”

  Hapa ndipo tatizo lilipo, watu wengi hawana mawazo ya biashara na hawajui jinsi ya kuyapata, tayari nimekwishawafundisheni jinsi ya kupata wazo la biashara, kilichopo sasa ni ninyi kutafuta tatizo na kujaribu kulitatua! Kamwe usiogope, wala usisikilize sana moyo wako, mara nyingi utakuvunja moyo, songa mbele katika hali ya kujiamini, unaweza! Kila unachokifikiria unaweza kukifanya, wala usivunjwe moyo na mtu yeyote kama kweli umedhamiria kufanikiwa basi elewa inawezekana na mafanikio ni ya kila mtu aliyeamua, si ya kundi fulani la watu. Kijana mmoja alimfuata mtu mmoja tajiri na kumuuliza:

  “Nawezaje kuwa tajiri kama wewe?”
  “Unataka kuwa tajiri?”
  “Ndiyo.”

  “Tukutane kesho alfajiri ufukweni.”
  “Ahsante mzee.”
  Kijana akarejea nyumbani akiwa na furaha nyingi, moyoni akiamini siku iliyofuata asubuhi alikuwa anakwenda ufukweni kupewa utajiri na mzee huyo.

  Saa kumi na moja alfajiri alikuwepo ufukweni akitetemeka kwa sababu ya baridi, moyoni mwake alidhani tajiri asingetokea lakini ilipogonga saa kumi na mbili kamili, gari la kifahari liliegesha ufukweni na mzee aliyevalia kanzu nyeusi akashuka na kumfuata kijana huyo.

  “Umekwishafika?”
  “Ndiyo.”

  “Haya vua nguo.”
  “Nivue?” Kijana akuliza kwa mshtuko.
  “Ndiyo, usiogope, wewe vua tu.”

  Kwa hofu nyingi huku akitetemeka kijana akavua nguo zote na kubaki na nguo ya ndani peke yake, ndipo tajiri akamwamuru aingie majini na kuanza kutembea kwenda mbele kwenye kina kirefu, kila alipokwenda mita chache aligeuka nyuma kumwangalia mzee ambaye alimwonesha ishara ya kusonga mbele, akazidi kwenda hatimaye maji yakafika kidevuni.
  “Niendelee?” Akauliza.
  “Kama unaka kuwa tajiri endelea kijana.”

  Akiwa na hamu ya kuwa tajiri akaendelea mpaka maji yakagusa pua, akageuka tena kumwangalia tajiri ambaye kwa ishara alimwambia asonge mbele zaidi mpaka maji yakafunika kichwa! Akabaki humo kwa karibu dakika moja akihangaikia hewa, mambo yalivyozidi kuwa magumu akakurupuka na kukitoa kichwa chake nje kisha kutembea mpaka ufukweni ambako tajiri alimwita.

  “Hebu niambie ulipokuwa chini ya maji ulijisikiaje?”
  “Vibaya mno, ningeendelea kubaki ningekufa.”
  “Ulikuwa unahitaji nini?”
  “Nilikuwa nahitaji kitu kimoja tu, nacho ni hewa ya oksjeni.”

  “Basi kijana, kiu uliyokuwa nayo kwa hewa ya oksijeni ukiwa chini ya maji, kama ndiyo itakuwa hamu yako kwenye mafanikio, ni lazima utajirike! Kwa hiyo njia ya wewe kutajirika ni kuwa na kiu kali ya mafanikio kama uliyokuwa nayo chini ya maji, hiyo ndiyo itakayokuzalishia wazo la wewe kutoka kwenye umasikini, kwaheri,” tajiri akasema na kuingia garini, huyo akaondoka na kumwacha kijana ameketi mchangani.

  Kilichosemwa na tajiri kwangu mimi ni ukweli kabisa, kama ndugu msomaji umedhamiria kutoka kwenye hali ngumu uliyonayo hivi sasa, basi ni lazima uwe na kiu kali ya mafanikio! Kiu hiyo ndiyo itakayokuondoa mahali ulipo. Unaweza kuwa una shida nyingi sana leo, pengine umekata tamaa na kuona wewe ni wa hivyo hivyo mpaka kaburini, nakutangazia wazi leo kwamba, hapo ulipo si mahali pako! Uko hapo kwa muda tu ukisubiri kwenda mahali unapostahili, ni kama mtu akiwa kwenye chumba cha kusubiria ndege kabla hajapanda.

  Usikate tamaa, tafuta wazo la wewe kuondoka mahali ulipo, usiridhike na nafasi uliyonayo leo, kuna mahali pazuri zaidi ya hapo ulipo panapokusubiri! Usiwe mjinga wa kuegesha gari na kuvuta ‘hendibreki’ wakati safari bado inaendelea, simama, anza kitu hata kama ni kidogo kiasi gani lakini ufikirie kwa upana, mwisho wa siku ulianza bila kitu, lakini utamaliza ukiwa na kila kitu.

  Wengi wetu huwa tunakuwa na mawazo mazuri sana ya biashara, lakini tunayatupa kwa sababu hatuna kitu au kile! Hauhitaji kuwa na kila kitu kufanikiwa, unaanza na ulichonacho mkononi kisha mbele utakutana na kila kitu. Wazo la biashara ndilo litakaloleta fedha, suala la mtaji utatoka wapi siyo lako, unachotakiwa kufanya wewe ni kuhakikisha unanyanyuka mahali ulipo na kuanza kuzunguka huku na kule, ukitafuta mtu mwenye fedha lakini hana wazo, huyo ndiye atakayekupa mtaji wa wewe kufanya biashara kama jinsi kijana aliyekwenda India na kuwaona Wahindi hawana viatu alivyofanya na leo hii ni bilionea.

  Ninachoamini mimi Mungu hawezi kukupa wazo, halafu akakunyima msaada! Huu kwangu mimi ni ukweli, naamini kila kitu chema kinachotokea duniani ni Mungu anafanya kazi yake, hajakoma kuumba, bado anaendelea! Lakini Mungu hawezi kushuka leo, akiwa Mungu na namna alivyo na kufungua duka, utaweza kwenda kununua kiberiti dukani kwa Mungu? Mungu anatisha.

  Hivyo anachofanya Mungu huwa anagawa mawazo kwa watu mbalimbali na kuwataka watekeleze mambo hayo ili kuwasaidia wanadamu, aliingia akilini mwa Thomas Edson, mwanasayansi huyo akatengeneza umeme, leo hii dunia nzima inakwenda kwa sababu ya umeme! Vivyo hivyo kwako msomaji, Mungu anapokupa wazo, usikae nalo tu au kuogopa kuchukua hatua kwa sababu huna hiki au kile, songa mbele utashangaa utakapokutana na misaada ambayo hukuwahi kuitarajia kutoka kwa watu ambao wala hukuwahi kuwafahamu.

  Wengi wetu tunaishia katika kusitasita bila kuchukua hatua wakati Mungu anataka utekelezaji wa haraka na kwa sababu hawezi kumbembeleza mtu, utakaposita kwa muda mrefu yeye atachukua wazo hilo hilo na kumpelekea mtu mwingine ambaye atalichukua na kusonga nalo mbele! Mwezi mmoja baadaye, utapita kwenye mtaa huo huo ambao wewe ulitaka kufungua hotelini na kukuta tayari imekwishafunguliwa na kumfuata mwenye hoteli kumwambia “Hakyanani tena na mimi nilikuwa na wazo hili hili.”

  Ni kweli ulikuwa na wazo hilo lakini ulichelewa, Mungu akalihamishia kwa aliyefungua hoteli. Ndugu msomaji hebu jiulize, ni mara ngapi umewaza kufanya jambo halafu wewe mwenyewe ukaishia kujipinga?

  Mara nyingi mno! Mungu alikupa mawazo mengi ya kukuondoa hapo ulipo kwenda katika hatua nyingine lakini ukaendelea kusita, matokeo yako wazo lako likapelekwa kwa mtu mwingine kwa sababu Mungu hataki kupoteza muda bali anataka kuwahudumia watu wake haraka iwezekanavyo.

  Pambana na hali hii ya kusita ambayo ni adui mkubwa wa maendeleo ya watu wengi duniani, usikubali kabisa! Chukua hatua kwenda mbele, tafuta tatizo katika jamii unayoishi ndani yake, ukishalipata basi litafutie suluhisho, ukifanikiwa tayari utakuwa umeshapata kitu cha kukukomboa, kumbuka ukiwa na kiu kali ya mafanikio lazima utagundua wazo la kukuondoa hapo ulipo na lengo lako litatimia, utakachotakiwa kufanya baada ya hapo ni mpango wa kuelekea kwenye mafanikio.
  Hatua ya tatu:

  Mpango wa kutimiza lengo
  Baada ya kuongelea lengo, hebu sasa tuelekezane juu ya nini cha kufanya ili uweze kulifikia lengo hilo, hapa ndipo tunaingia kwenye somo liitwalo Mpango ambalo wenzentu Waingereza huliita Bussiness Plan. Kama unataka kufanikiwa maishani mwako ni lazima uwe na mpango, mafanikio yanayotokea kama ajali hayapo, kama yapo basi ni mmoja kati ya watu milioni moja na hatadumu sana kwenye mafanikio hayo.

  Watu wengi sana hushinda Bingo na kupata mamilioni ya shilingi kwa wakati mmoja, bila kupanga, kama kuna mpango ulifanyika basi ni wa kununua tiketi na kuidumbukiza kwenye kisanduku! Ni vizuri sana kuwafuatilia watu hawa baada ya miaka mitano au kumi ili kuona wanaendeleaje, utakachokikuta kitakusikitisha, wengi watakuwa wamekwishafilisika na kuingia kwenye ulevi na wengine utakuja wameshajinyonga.

  Hii ni kwa sababu mafanikio yalikuja kama ajali, bila kupangiliwa! Kama hivi sasa unaposoma waraka huu uko kazini, basi kabla hujaondoka ndani ya nyumba yako ulitengeneza mpango wa safari, kwamba naondoka hapa, nakwenda pale, kisha pale na mwisho kazini! Vivyo hivyo katika ulimwengu wa kutafuta mafanikio kuna safari inayohitaji mpango.

  Mimi humfananisha mtu yeyote anayeingia kwenye safari ya kutafuta mafanikio (The Pursuit of Success) bila mpango, kuwa sawa kabisa na mtu anayekwenda kwenye dirisha la kukatisha tiketi na kuomba auziwe tiketi bila kujua anakoelekea! Hiki ni kichekesho, ninachofahamu mimi ni lazima mtu ujue unakwenda wapi ndipo uende kukata tiketi yako, vivyo hivyo katika maisha ni lazima ujue unakwenda wapi na jinsi ya kufika huko! Unataka fedha, kiasi gani? Na pia jinsi ya kuzipata. Kunaweza kuawa na mipango ya aina mbili, ya muda mfupi na mrefu lakini yote miwili ni lazima ukufikishe unakotaka kwenda.

  Nilipoanza kufanya biashara unayoifanya mwaka 1998, tatizo langu kubwa lilikuwa ni umasikini, niliichukia sana hali hii. Ni kweli huko nyuma kabla ya mwaka huo nikiwa kijana mdogo kabisa nilifanikiwa kupata fedha nyingi huko machimboni, lakini zikaisha na nikarejea kwenye umasikini tena, hilo kwangu lilikuwa ni tatizo, ilikuwa ni lazima nipange mpango wa kuondoka hapo, kwani kichwa na akili yangu ilikuwa ni ile ile.

  Je, nilitumia mpango gani mpaka nikafanikiwa kufika hapa nilipo tena? Fuatilia wiki ijayo nikupe siri zangu.


  [​IMG]
   
 2. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #2
  Dec 26, 2009
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  Mi tayari ni tajiri...
  Nataka kujua namna ya kuwa na furaha while
  i am very rich.....
   
 3. eRRy

  eRRy JF-Expert Member

  #3
  Dec 26, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 1,080
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135

  Kauze Vyote Uwagawie masikini-Jesus Christ
   
 4. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #4
  Dec 26, 2009
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  kama ndo hivyo sasa
  unakuja washauri watu wawe
  matajiri ili iweje?
   
 5. Tripo9

  Tripo9 JF-Expert Member

  #5
  Dec 26, 2009
  Joined: Sep 9, 2009
  Messages: 2,168
  Likes Received: 65
  Trophy Points: 145
  C mchezo mkubwa waraka wako huu. Kumbe mi nmezungukwa na utajir eeeh! Mi ngoja niangalie ntatajirika vp kupitia hali ya hewa hii ya hapa Dar, joto mpaka 32deg of centgrad?! Lazma ntokee hapahapa
   
 6. L

  Lampart Senior Member

  #6
  Dec 26, 2009
  Joined: Sep 18, 2009
  Messages: 138
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  It goes without saying!
  >ili iweje?
  .......ili ukauze utajiri wote ukawagawie maskini!!!
  I don't think it makes sense at all. Sio wewe utarejea kule kule kwenye umaskini sasa tena utakuwa umefanya nini????

   
 7. eRRy

  eRRy JF-Expert Member

  #7
  Dec 27, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 1,080
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Huyu Anataka furaha na si Utajiri!
   
 8. eRRy

  eRRy JF-Expert Member

  #8
  Dec 27, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 1,080
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  [​IMG]
   
 9. L

  Lampart Senior Member

  #9
  Dec 28, 2009
  Joined: Sep 18, 2009
  Messages: 138
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Furaha bila ya utajiri wa aina yoyote ile haiwezekani kabisa!!!
  Else, utakuwa unajidanganya kuwa eti umo kwenye furaha!!
   
 10. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #10
  Dec 28, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  Mkuu Unatangaza Matajiri Duniani mbona hutangazi masikini duniani Nchi Masikini Duniani ni Nchi gani? naona kuwa ni Tanzania ni Masikini sana Duniani ni Binadamu gani? naomba jibu kwako?
   
 11. Abunwasi

  Abunwasi JF-Expert Member

  #11
  Dec 28, 2009
  Joined: Jun 25, 2009
  Messages: 3,166
  Likes Received: 1,061
  Trophy Points: 280
  Ni article nzuri sana kwani wengi wanafikiria kuwa ukosefu wa mitaji kuwa chanzo cha umasikini lakini hata wakipata mitaji[mapesa ya JK] hiyo haikuwafikisha popote. Na hata mmoja akibuni mradi na ukawa na mafanikio basi kila mtu ataiga mradi huo mpaka inafikia kugombania wateja ambayo inaleta hali ya kuwa na diminishing returns hadi kufilisika.
  Nadhani ungetayarisha makala na kupeleka kwenye magazeti [hasa ya udaku ndiyo yenye wasomaji wengi] pengine itasaidia kubadilisha fikra za wengi kuwa mtaji mkubwa ndiyo msingi mzuri wa mafanikio
   
 12. KIFARU

  KIFARU Senior Member

  #12
  Dec 28, 2009
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 172
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  UtAjiri ni kwa ajili ya kuweza kuyakabili mazingira unayoishi na mabadiliko ya kimaisha tunayoenda nayo, ila amini usiamini, furaha za watu, watu wanazigeuza kujipatia pesa, hivyo usitegemee furaha yako isi ku-cost hata pesa,kama unataka furaha usiwe mtu wakutelekeza wajibu wako hapa duniani, inabidi ujidanganye everything is fine,hata maudhi uone sio maudhi
   
 13. T

  TUMY JF-Expert Member

  #13
  Dec 28, 2009
  Joined: Apr 22, 2009
  Messages: 706
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  makala nzuri.
   
 14. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #14
  Dec 28, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  next time uwe una acknowledge SOURCES za makala bwana mkubwa!......
   
 15. m

  majogajo JF-Expert Member

  #15
  Apr 5, 2012
  Joined: Oct 9, 2011
  Messages: 321
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  hii ni sarakasi nyingine tana.........
   
Loading...