Lazaro Samwel
Member
- Apr 27, 2019
- 33
- 26
Ukitaka kupata hela kama wanayopata washindani wako ambao inawezekana mpo soko moja na mnauza bidhaa ambazo zinataka kuendana au zinaendana kwa namna moja ama nyingine basi wewe jifunze kuuza bidhaa lakini ukitaka kuuza zaidi ya washindani wako ambao mpo soko moja jifunze kuuza huduma ya maboresho ambayo ipo ndani ya bidhaa yako.
Kwa kurahisiha kazi tunaweza tukaweka hivi “Ukitaka kufanya mauzo ambayo washindani wako wanayafanya kwenye biashara zao basi fanya kama wanavyofanya wao kwenye soko ambalo mpo pamoja lakini ukitaka kufanya mauzo ambayo washindani wako hawayafanyi kwenye biashara zao basi fanya kile ambacho washindani wako hawakifanyi kwa ubunifu kwenye biashara zao au wanaogopa kukifanya.
Leo nitarudia tena kuzungumza kauli hii lakini kwa wale ambao watatilia maanani itaenda kuwasaidia sana.
Kikawaida sokoni kuna ushindani mkubwa kwa wafanyabiashara ambao nao wanataka kuuza bidhaa ambazo wenzako wanauza au ambao wanataka kuwa kama washindani wao,lakini kuna ushindani mdogo sana kwa wafanyabiashara ambao wanaelewa kuna ushindani na wakatafuta eneo sokoni ambalo litaleta utambulisho wao kupitia bidhaa zao ambazo zinataka kuendana na za washindani wao.
Kwasababu wafanyabiashara wengi hawana ujuzi wa kuuza wengi ambao wanaanzisha biashara wanaingia sokoni kushindana na wengine kuuza bidhaa lakini kwa wale ambao wanajiongeza na kupata ujuzi vizuri wa biashara wanaingia sokoni kuuza maboreho ambayo wengine hawayaoni wala kuyasema kuwa yapo kwenye bidhaa zai ambazo wanaziuza kwa wateja wao,ndio maana mauzo yao sio ya kuridhisha.
Kosa ni kwamba wafanyabiashara wengi wanajua wanauza bidhaa/huduma zaidi ya kuelewa kwamba wanauza maboresho ya maisha ya wateja wao.
Unauza maboresho gani kupitia bidhaa yako?
Wakati mwenzako anauza kuwa na muda wa ziada,ongezeko la fedha, furaha , amani, ujasiri n.k wewe unauza maboresho gani kupitia bidhaa yako?
Nilishasema katika makala ambazo zimepita kwamba kama tangazo lako lolote ambalo umeandika halioneshi mwisho mteja wako atakuwa na hali gani tofauti na ya sasahivi kwenye maisha yake ni kiashiria tosha cha tangazo lako kufanya vibaya.
Nisikilize,kwako wewe unapouza bidhaa yako unaweza kuona unajza bidhaa kwasababu unataka hela lakini mteja haoni bidhaa kama bidhaa anaona usafiri wa kumsaidia kuboresha sehemu flani kwenye maisha yake.
Wewe unaweza kuona unauza sabuni yenye harufu nzuri ya kufanyia usafi kuondoa uchafu sugu lakini mteja anachokiona ni upatikani wa harufu nzuri nyumbani kwake na mwonekano mzuri wa nyumba yake baada ya kuondoa uchafu sugu sehemu mbalimbali ambao ulikuwa ukiletea mwonekano mbaya wa nyumna na kutengeneza harufu mbaya.
Mteja wako anaweza asiwe anaona sabuni tuu yenye harufu nzuri lakini anachokiona ni kujiamini mbele ya marafiki zake ambao huwa wanakuja kumtembelea kwasababu nyumba yake itakuwa safi.
Mteja atanunua sabuni yako kwasababu anajiona akikaribisha marafiki zake ambao alikuwa anagoma kuwakaribisha nyumbani kwake kutoka na alama za uchafu ambazo zilikuwepo ukutani n.k
Haya ndiyo ambayo unatakiwa kuyazungumza na kuyaandika kwenye matangazo yako.
Swali kwako ni kwamba huwa unamwonesha mteja wako hivi kwenye maelezo yako ya bidhaa ambazo unaziuza?
Nataka usiwe na akili ya kusema nauza mafuta ya kukuza nywele,nataka usiwe na akili ya kusema unauza keki tuu,nataka usiwe na akili ya kusema nauza supplement au bidhaa za program kwaajili ya kupunguza uzito.
This is nonsense na unaacha hela nyingi sana mezani kwa kila mteje ambaye unakutana naye.
Waza katika namna ambayo nimekuelekeza unapojua mteja wako anahitaji kufika wapi kutokana na changamoto ambazo umegundua anazo.
Naimani umejifunza kitu,kama utapenda kujifunza zaidi na kupata mentor ambaye atakusaidia katika biashara yako online na offline ili uweze kufanya vizuri kimauzo basi bonyeza wa.me/255678010334
Lazaro Samwel
Author-10 Books| Sales And Marketing Expert | Professional Copywriter
#akiliyaushindi