Unataka kuoa? Oa ukijisikia kutoka moyoni!

Ligogoma

JF-Expert Member
Joined
Aug 27, 2010
Posts
3,502
Reaction score
6,458
Heloo!!!

Ndoa nyingi siku hizi zinavunjika! Zinavunjika kwa sababu upande mmoja una feel hauwezi kubeba jukumu la ndoa!

Kwa nini?

Kwa sababu vijana wanaoa kama fashion, kuiga, kutafuta hadhi na wengine kutafuta hata kipato tena unakuta ni kipato cha nauli za likizo tu ofisini! Zikitokea changamoto za ndoa hawapo tayari kuzikabili!

Kabla ya kuoa, jisikie kwanza unahitaji kuoa, jisikie unahitaji kuwa na mzigo wa familia yako, jisikie unatamani majukumu, jisikie unatamani changamoto mpya katika maisha!

Ukioa kwa kupata hisia katika nafsi, changamoto za ndoa kwako zitakuwa si mzigo kama zilivyo changamoto za familia yako ya awali (baba, mama na nduguzo) ambao tatizo lolote upo tayari kulikabili na si kuwatenga na kukimbia!

Why umkimbie/umkimbize mkeo ilhali tabia hizo hizo umeweza kuzivumilia miaka nenda rudi na hujazikimbia kutoka kwa dada yako?

Nilipofikisha miaka 27 nilijisikia kabisa nahitaji changamoto za ndoa, nilioa nina miaka 29. Rafiki yangu kipenzi nae akaona aoe baada ya mimi kuoa hivyo mwaka uliofuata akiwa na miaka 31 akavuta jiko.

Mwaka mmoja baadae akaachana na mkewe wakiwa na mtoto mmoja, kwa madai mwanamke anamzingua sana tabia mbovu na hafai kuwa mke!

Miaka sita baadae akiwa na miaka takribani 38 akajisikia kuoa sasa, bahati nzuri akamkumbuka mwanae na mkewe walioachana hivyo wakatafutana na bahati mwanamke nae hakuwa kwenye mahusiano thabiti tangu walipoachana hivyo ikarahisisha kurudiana kwao.

Miaka kadhaa sasa wanaishi pamoja raha mustarehe na wameongeza familia, nimemuuliza jamaa yangu vipi mkeo hakuzingui tena!

Akanijibu "Nahisi ule ulikuwa ni utoto, mke wangu kumbe ananipenda sana na kadiri alivyokuwa anaonyesha upendo nikaona kero kama nabanwa banwa, anataka kunitawala, nachungwa, nipo kifungoni na kadhalika. Ajabu maisha ni yale yale lakini sasa hivi nayafurahia sana"

Muoe vijana, muoe mkiwa tayari kwa kuoa kiakili, kimwili na kihisia.

Nimemaliza
 
Miaka kadhaa sasa wanaishi pamoja raha mustarehe na wameongeza famili.

Wanaotaka kuoa singo mama wapitie hapa, siku yoyote likihitajika linapepea.... Hakuna cha mahusiano stable.
 
Ila kweli hii ya kitaka kuoa ili kupunguza gharama za kubadilisha papuchi ufaingia mmenge bure.... Bora uendelee kugharamikia papuchi nyi gi uwezavyo mpaka pale moja itakayokufaaa.
 
Cha ajabu wewe una weza kuoa kutoka moyoni na mkeo akakubali kuolewa kutoka kwenye mapafu...tatizo Ndiyo linapo anza.

Sent using Jamii Forums mobile app

Ni kweli kabisa ila amini kwamba, unapokuwa umekua kifikra na kiakili! Hata marafiki watabadilika na huko utapata wachumba matured pia!
 
Siku hizi mtu anaoa au kuolewa kumkomesha ex wake fulani..sasa cha kushangaza Arusha is so olewa anakuja tambua kumbe eeb ndoa sio kisasi..wala relavancha..ndio imepita hyo ataanza kucheat etc etc basi ndoa inavunjika.

Sent from my SM-J410F using JamiiForums mobile app
 
Kifupi dhima ya ndoa siku hizi imeharibika, siyo kila anayepanga ndoa anamaanisha kuoa/kuolewa! Wengine wazugaji tu
 
Ila kweli hii ya kitaka kuoa ili kupunguza gharama za kubadilisha papuchi ufaingia mmenge bure.... Bora uendelee kugharamikia papuchi nyi gi uwezavyo mpaka pale moja itakayokufaaa.

Dogo! Kuoa si kujihakikishia papuchi tu, unaweza kuoa na mwezi mzima papuchi unaisikia kwenye bomba!

Ndoa ni mlundikano wa michakato inayoweza kukufanya hata muda wa kula papuchi usiwepo japo umeiweka ndani!
 
Mhm hayo sasa unayataka mwenyewe. Sababu kuu ya watu kuoana ni kugegedana hamna jingine. Mambo ya sijui kusaidiana maisha hizo ni somjo tuu na mwanaume wala hutakiwi kiliwaza hilo.
Mke bwana namwambia mrembo kabisa kuwa tumeoana kupeana burudani hapa mambo sijui ya kuja kunisaidia kujenga life hayapo maana nilishajenga ndio maana ukanikubali
 
Back
Top Bottom