Unataka kuoa Nigeria? App hii itakusaidia

Unataka kuoa Nigeria? App hii itakusaidia

Joined
Jun 3, 2014
Posts
28
Reaction score
16
Developers wa kinaijeria wametengeza App inayokokotoa kiwango cha mahari kulingana na sifa za mwanamke (wa kinaijeria) anayetarajiwa kuolewa. Kabla hatujaendelea unatahadharishwa kuwa App hii ni masihara tu ....vigezo na masharti kuzingatiwa.

Inavyofanya kazi ni rahisi. Mtumiaji wa app atachagua sifa ambazo mchumba wake anazo na app itaongeza au kupunguza mahari kulingana na hizo sifa.

BridePrice1.JPG


​
gere.JPG


Baada ya kukamilisha sifa zote, mwisho app itapeleka maombi kwa "elders" ambao watapiga total na kurudisha majibu ya kiasi kinachodaiwa.

Elders.JPG

​

App inapatikana: http://www.brideprice.com.ng/

Changamoto na fursa kwa Tanzanian coders:
Hii inaweza kuwa changamoto kwa coders wetu wa kike kutengeneza version ya app ya kike kwa ajili ya kumkubali au kumkataa mchumba wa kiume…sifa nadhani zikiwa "kazi", "kitambi" …..
Vile vile developers wa kiume wanaweza kutengeneza App hii ikiwa na sifa "relevant" kwa ajili ya soko la Tanzania…..

Habari imetoka: http://www.bofyatz.com/2014/10/unataka-kuoa-nigeria-app-hii-itakusaidia.html
 
Mimi kuo Mnigeria labda nirogwe. Yaani niko tofauti kabisa na hawa watu, Mungu anisamehe.
 
Back
Top Bottom