Unataka kudumu kwenye utumishi wako, endelea kujipendekeza ndio njia sahihi

Apr 23, 2012
76
125
"IT'S DANGEROUS TO BE RIGHT WHEN THE GOVERNMENT IS WRONG ...," yaani kwa tafsiri isiyo rasmi sana ni; '.., ni hatari sana kuwa sahihi wakati serikali ikiwa haiko sahihi'..., maneno hayo yametamkwa na mwandishi, mwanahistoria na mwanafalsafa wa kifaransa ambaye alikuwa akiitwa François-Marie Arouet maarufu kama "de plume Voltaire".,

Pia ukisoma "THE 48 LAWS OF POWER " za Robert Green, Law (sheria) number 1: Never Outshine The Master.., (Act less smarter than your boss, Present your ideas in a way that they echo your boss's thought, Discreet flattery is very powerful.)

.., sheria hii namba moja (1) ya Robert Green inataka kwamba; uwafanye wale walio juu yako wajisikie wenye nguvu na mamlaka, katika utashi wako wa kuwafurahisha na kuwapendezesha hakikisha hauoneshi kipaji chako chote, usifanye zaidi ya wakubwa zako,

Sheria hii inataka usiwe na weledi, ujuzi, utaalamu zaidi ya wakubwa zako, sheria hii inaeleza, ukitaka kufanikiwa mbele ya wakubwa zako (watawala) hakikisha kwamba unamsifia huyo mtawala, unamsafisha na kumpongeza bila uoga hata kwa unafiki, and you will attain the height of power,

Dhumuni la somo hili;
> wasilisha mawazo yako katika njia ambayo yanarandana na mawazo ya 'bosi' wako,
> Jitahidi kutokuwa mwerevu zaidi ya 'Bosi' wako katika eneo lolote mbele yake.
> usiichukulie kazi yako, shughuli yako mbele ya 'bosi' wako kama kazi/shughuli ya mpito.
> mara zote hakikisha unatafuta ushauri wa shughuli yako au ushauri wowote kutoka kwa 'bosi' wako,
> tunza siri, jipendekeze mbele ya 'bosi' wako, ukitaka kufanikiwa ni lazima ujipendekeze, tafuta huruma ya 'bosi' wako.,

Kuna kisa cha aliyekuwa waziri wa fedha wa Ufaransa katika karne ya 17 anaitwa Nicholas Fouquet, ambaye aliingia katika mgogoro na mwajiri wake, mfalme Louis XIV.., kuna kisa kimoja kirefu (nitaeleza baadae), mwaka 1661 mfalme Louis XIV alimfunga Nicolas Fouquet miaka 20 jela.., wakiwa wametofautiana katika kutafuta sifa nzuri kwa wafaransa (umma)

KISA CHA UGOMVI HUO;
Umma wa Ufaransa, hususani katika jiji la Bordeaux, ulimpenda sana waziri huyo wa fedha (Nicholas Fouquet) kwa sababu alijenga kiwanda cha kutengeneza na kusindikia 'wine' katika mji huo (ni mzaliwa wa huko).., na viwanda vya namna hiyo kwa kifaransa hujulikana kwa jina la 'château'.., wananchi walimpenda Nicholas Fouquet kwa sababu ya kuwakumbuka katika uzalishaji wao wa Zabibu., alijenga kiwanda hicho katika shamba lake la Vaux-le-Vicomte!

Kitu cha kushangaza zaidi..., baada ya Mfalme Louis XIV kumfunga jela Nicholas Fouquet, mfalme huyu alijenga kiwanda kikubwa mara dufu kuliko kile cha Fouquet, kiwanda hiki alikijenga katika eneo la Versailles, maarufu kama 'Palace of Versailles'

HAPA TUNAJIFUNZA; mfalme Louis XIV hakupendezwa na sifa ambazo waziri wake wa fedha (Nicholas Fouquet) alikuwa amezipata na kuwa mtu maarufu katika eneo hilo kuliko yeye.., na ndiyo maana wakati mfalme Louis XIV akiwa na miaka 23 mwaka 1661, alifanya ziara katika eneo la Vaux-le-Vicomte, alipozaliwa Fouquet, na kumtumbua kabla ya kumfunga jela (kwa makosa ya kutokufuata itifaki).., (King Louis XIV was out shined by his minister of finance,)

Kwanini Nicholas Fouquet alitumbuliwa; He unintentionally outshone his master, King Louis XIV, making the King feel insecure. (remember, to Act less smarter than your boss) in the 48 laws of power!

KWANINI SOMO HILI; leo tuko kwenye zama za kujipendekeza ili 'bosi' wako akuone, akuteue na asikutengue.., akupandishe cheo na asikuhamishe idara.., zama za kujipendekeza hizi.., somo hili linawatosha sana wale watumishi walioficha taaluma zao na wanatumia 'kauli mbiu za bosi wao'.., watumishi waoga, watumishi wenye kupenda kujipendekeza kwa wakubwa wa kazi, watumishi wenye kujificha na kutokupenda kuutumia ujuzi wao katika maeneo yao ya kazi!

NB; wakati mwingine nitawapa simulizi za namna "Galileo Galilei maarufu kama Galleo" alivyotumia kanuni za sheria hizi kufanikiwa.., huyu alikuwa ni mtu kutoka Italia, aliishi kati ya mwaka 1564-1642.., alikuwa ni mwanafalsafa, mbobezi wa hesabu, fizikia, uhandisi, na ameshiriki sehemu kubwa sana katika mapinduzi ya sayansi (scientific revolution) katika karne ya 17 kuelekea karne ya 18..,

.., anajulikana pia kama baba wa fizikia, baba wa ugunduzi wa njia za kisayansi, baba wa sayansi, pia 'the father of Observational astronomy' wataalam wa sayansi wanaelewa mambo haya!

Ahsante!


Martin Maranja Masese (MMM)
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom