Kaunga
JF-Expert Member
- Nov 28, 2010
- 12,530
- 13,469
- Thread starter
- #21
please kaunga could you explain it in swahili or franch.
Kiufupi, huyo mkaka James ni kama walivyo wanaume wengi au ndoa nyingi. Mahusiano na mkewe ni ya kawaida sana kiasi kwamba hangojei muda wa kurudi nyumbani kwa hamasa.
Ijumaa anapenda kujichanganya na washkaji club, huku Mke akiwa nyumbani na mishughuli ya nyumbani.
Akiwa kazini akakutana na mdada ambaye alimkubali si kwa uzuri wake tu, bali kwa jinsi alivyo charming n.k.
So ikatokea akakutana naye usiku club, Yule dada hakuacha uchangamfu wake na akamuomba James wacheze mziki.
Baadaye mumewe bidada akajumuika nao, James aiashtuka sana kwani alifikiri huyo dada ni single (na possibly muwindaji). James akayafurahia maisha wanayoishi huyo dada na mumewe. Akatafakari maisha anayoishi yeye na mkewe, akakumbuka walivyokuwa wachumba; ndipo akaondoka kurudi nyumbani akiwa ameapa kuyabadilisha mahusiano yake.
Yule dada (grace) na mumewe dan wamejipangia siku yao peke yao ambapo wanafurahia maisha kana kwamba ni wapenzi tu.
Mtambuzi nimejaribu, ukizingatia natumia simu na niko kwenye gari. LOL
Last edited by a moderator: