Unashabikia adhabu ya viboko au uko upande gani?

Unashabikia adhabu ya viboko au uko upande gani?

PRINCEd

JF-Expert Member
Joined
Dec 14, 2015
Posts
862
Reaction score
625
Sheria inayoruhusu adhabu ya viboko mashulen ina mkanganyiko katika utekelezaji wake ambao binafsi naamini ndo utata unapoanziaa....

1. Sheria inasema wazi kuwa itolewe kwa kosa kubwa la utovu wa nidhamu kadili itakavyoonekana
Kosa kubwa ni lipi....?? Kuchoma bweni..? Kumfyoza mwalimu...? Au kuandika matusi kwenye mtihani..? Utoro au kupiga kelele darasani..?

2. Adhabu itolewe na mkuu wa shule au mwalimu aliyekamisiwa na mkuu wa shule kwa maandishi...??

Watoto watende kosa wako 15 mkuu wq shule aandike vibali 15..?? Mwalimu achape wanafunzi 15...kila siku....?

3. Adhabu ikitolewa iandikwe kwenye kitabu (blackbook)...? Kitabu mara ngapii...?

4. Idadi ya viboko ni 4 (maximum) yaan hata kumchapa mwanafunzi fimbo moja au mbili mwalimu asubiri mkuu ampe kibali...???

5. Mwanafunzi wa kike achapwe na mwalimu wa kike, kosa la utovu wa nidham litendeke darasani mwalimu amtoe mwanafunzi ampeleke kwa mkuu wa shule yeye ndo aseme ili kosa ni la fimbo amwandkie kibali amtoe hapo ampeleke kwa mwalimu wa kike ambaye yuko willing..?? Kuchapa....??

Hapa ndo hoja fikirishii zinakujaa...

Kuna watu katika suala lililotokea mbeya wanaona wanafunzi wametenda jinai walistahili kufikishwa mahakamani na sio kuchapwa na RC...??? Serious...??


"BY- LAWS" za kiuanafunzi zinazuia mwanafunzi kutenda jinai, ili ni kosa la kumfukuza mwanafunzi moja kwa moja, then jinai haishi siku moja mahakaman ikawa imehukumiwa tayari sasa tufanye uchunguzi ufanyike kwa mwaka mzima, mtoto yuko mahakaman mayb kila mwezi wenzio wanasoma........atafahuluje mitihani yake sawa..? wakati lazima atapoteza masomo na pysochological tourture za hapa na pale...?

Walikutwa na simu......Mwanafunzi kukutwa na simu ni kosa la kufukuzwa shule moja kwa moja, mfano ishu ya Mbeya wangapi wangefukuzwa shule pale...?kwan sheria inasema kumiliki au kutumia tu hapa hata yule aliyeigusa anasepa....najua walikuwa wanatumia na wenzao....??

Vipi mwanafunzi akipatikana na hatia akaamuliwa kulipa fidia iwe kulijenga bweni..Wazazi wangpi kati ya wale watoto wana uwezo wa kulijenga bwenii au hukumu iwe kifungo Je...?? Vipi uyu mwanafunzi kuhukumiwa kifungo...?? Mwanafunzi gerezanii??

Kumbe yotee haya yanawezaa kuwa solved kwa fimbo 4 za RC...???[emoji1787]."kicheko"

Binafsii sijaridhika na ile laki 2 au laki 5 naona ni nyingi mno mayb ingekuwa laki kwa kwa laki mbili kwa waliokamatwa na simu...i stand to be corrected

Uwa nawaza siku walimu wakiamua kuwapeleka mahakaman wanafunzi kwa jinai wanazotenda uko mashuleni magereza hayatatosha...

Wanafunzi wakileo wana mapungufu makubwa katika malezi uko majumbani, wazazi wengine wanawapiga watoto wao makofii mijeredii n.k hawana walijualo katika child develpment na saikolojia za watoto, mtoto anakuwa mtukutu anaota usugu lawama zinakuwa kwa walimu thn tunademand walimu au kuwabeza kuwa awajasomea malezi...

......Tanzania ni Yetu Tushirikiane Kuijenga.....
 
Inategemea mtu kalelewa vipi, kama umelelewa kwa ukatili au kwa upendo, waliolelewa bila ya mapenzi ya Wazazi na wamekuwa wakipigwa kama wanyama wanaona ni kawaida, waliolelewa kwa upendo na wazazi wao watapinga kupiga mtoto kama ngoma.

Hivyo ni swala gumu sana ni sawa na ubishani wa Yanga vs Simba au Dini Uislamu vs Ukristo, au wanaoamini Mungu vs wasioamini, hamuwezi kufikia muafaka!
 
Sheria ifuatwe, hatuwezi kuwa na taifa la viongozi wanaovunja sheria na wakaendelea kuangaliwa tu.

Tena ikiwezekana vifutwe kabisa, Kuna shule moja ya wasichana kwa miaka mingi huwa inashika nafasi ya kwanza kitaifa Kwenye mtihani wa kidato cha nne.Kuna dogo alikuwa anasoma pale aliwahi kuniambia toka aanze kusoma pale hajawahi ona mtu kachapwa kiboko.

Na hawana tatizo lolote, madogo wanafaulu na wana nidhamu.

Kuchapana chapana viboko ni ujima.
 
Mkuu, viboko ni universal, hakuna nchi duniani ambayo viboko havitumiki au havijawahi kutumika, hao wazungu a.k.a mabeberu wanaojifanya kustaarabika sasa walikuwa wakichapana mno.

Katika mfumo ya maendeleo sisi tupo nyuma ya mabeberu kwa karne kadhaa, lakini kwa ulimbukeni wetu tunalazimisha kuishi maisha yao.

Wacha tuchapane kwanza tutaacha huko mbeleni ikibidi.
 
Mkuu wa mkoa kama mzazi kawaadhibu vijana watukutu waliochoma bweni kwa sababu wamekamatiwa simu zao ambazo ni kinyume ya sheria mtoto kuwa na simu shuleni.

hao watoto walistahili hiyo adhabu.
 
Inategemea mtu kalelewa vipi, kama umelelewa kwa ukatili au kwa upendo, waliolelewa bila ya mapenzi ya Wazazi na wamekuwa wakipigwa kama wanyama wanaona ni kawaida, waliolelewa kwa upendo na wazazi wao watapinga kupiga mtoto kama ngoma.

Hivyo ni swala gumu sana ni sawa na ubishani wa Yanga vs Simba au Dini Uislamu vs Ukristo, au wanaoamini Mungu vs wasioamini, hamuwezi kufikia muafaka!
Mkuu uko sahihi kuwa waliolelewa kwa ukatili kwa vichapo, matusi na kejeli, wataona yale aliyofanya RC ni sawa,

Na waliolelewa kwa mapenzi kwa kuelimishwa na kufahamishwa bila ya kufanyiwa ukatili, vichapo, matusi na kejeli wataona yale alivyoyafanya RC sio sawa..

Wanasaikolojia wanasema, mtoto akimuona mama ake anapigwa na Baba basi na yeye atampiga mkewe, na hii uovu utaendelea kizazi chote..

Kizazi cha Kitanzania kimeona mama anapigwa na baba, na sisi tunaendeleza kichapo na ukatili kwa watoto wetu kuanzia majumbani mpaka mashuleni..

Uovu unaendelea, kwani ubongo wetu unatwambia bila ya kufanya ukatili wa kuchapa na vingenevyo bado unakuwa hujatuma meseji ikafahamika..

Tanzania imekuwa SADIST country, Raisi, RC, Walimu, Wazazi, wote wanaamini katika kumpa mtoto maumivu ndio solution..

Mungu ibariki Tanzania na watoto wote..
 
Mkuu, viboko ni universal, hakuna nchi duniani ambayo viboko havitumiki au havijawahi kutumika, hao wazungu a.k.a mabeberu wanaojifanya kustaarabika sasa walikuwa wakichapana mno.

Katika mfumo ya maendeleo sisi tupo nyuma ya mabeberu kwa karne kadhaa, lakini kwa ulimbukeni wetu tunalazimisha kuishi maisha yao.

Wacha tuchapane kwanza tutaacha huko mbeleni ikibidi.
Inaonyesha Ulichapwa sana, ulimuona mama akipewa kichapo cha nguvu na Baba,.

Wewe unaendeleza "the Circle of evil", unafanya vile alivyofanya Baba kwa Mama na kwako, bila shaka unawachapa sana watoto wako..

Unaamini kumpa mtu maumivu ndio solution, ndio atafahamu unachosema, kwako wewe kukaa mezani na kumfamisha mtu kwa maneno ni ujinga na upumbavu..

Sikulaumu Mkuu, nalaumu malezi uliyo lelewa.
 
Kwani hao wanafunzi walipigwa na kitu kizito au walichapwa tu kwa fimbo? Wanastahili kuadhibiwa huwezi kuharibu miundombinu ya shule kisa hasira za kunyang'anywa simu. Madogo wamezingua sana
 
Mpumbavu ni wewe ambae hajui dunia nzima wanafunzi wanamiliki simu
na dunia nzima kuna shule za boarding
au unafikiri shule za boarding na simu zipo Tanzania tu?
Ona sasa unavyopanic badala ya kujibu swali langu.
Nakuuliza tena, unajua madhara ya mwanafunzi wa boarding kumiliki simu?
 
Mpumbavu ni wewe ambae hajui dunia nzima wanafunzi wanamiliki simu
na dunia nzima kuna shule za boarding

au unafikiri shule za boarding na simu zipo Tanzania tu?
Utaratibu wa hii ufataji wa sheria hii ndo uko katika njia ngum na hazitekelezeki
 
Ona sasa unavyopanic badala ya kujibu swali langu.
Nakuuliza tena, unajua madhara ya mwanafunzi wa boarding kumiliki simu?

Wewe unajua madhara ya mwanafunzi kumiliki computer?
unajua smart phone ni computer?
unajua hata kwamba kuna kampeni ya kuhakikisha shule zote
kuanzia za msingi ziwe na computers za internet?

wewe hujui vitu vingi kumbe
 
Mkuu, viboko ni universal, hakuna nchi duniani ambayo viboko havitumiki au havijawahi kutumika, hao wazungu a.k.a mabeberu wanaojifanya kustaarabika sasa walikuwa wakichapana mno.

Katika mfumo ya maendeleo sisi tupo nyuma ya mabeberu kwa karne kadhaa, lakini kwa ulimbukeni wetu tunalazimisha kuishi maisha yao.

Wacha tuchapane kwanza tutaacha huko mbeleni ikibidi.
viboko universal chief [emoji23][emoji23][emoji23]
 
Back
Top Bottom