Unapotembea na mume wa mtu, kubali wewe ni mwanamke daraja la pili

timetoloveyourself

JF-Expert Member
Mar 24, 2015
206
206
Kipindi utakapokubali kutoka kimapenzi na mme wa mtu, utakuwa umekubaliana kuwa mwanamke wa daraja la pili. Na siku zote mtu wa daraja la pili ni mtu wa daraja la chini ukilinganisha na daraja la kwanza.

Angalia sasa kama yupo na wewe na mke wake akapiga simu atamdanganya mkewe kwamba yupo ofisini au katika kikao na hautakuwa na ujasiri wa kuingilia mawasiliano yake. Pia anapokua nyumbani kwake kwa mkewe huwezi kumpigia au hata kumtumia text.

Dada yangu wewe ni mdoli? Anakuchukua kwenu na gari yake anakupeleka katika vyumba vya hotel lakini mke wake amemkabidhi nyumba nzima. Dada yangu shtuka!

Anakutembelea nyumbani kwako na unamtambulisha kwa rafiki zako na majirani kwamba ni boyfriend wako bila kujua unajizibia nafasi za kupata mtu sahihi wa kuweza kujenga nae maisha. Na mbaya zaidi hupajui hata yeye anapoishi.

Dada yangu mpaka lini utaendelea kujiharibia future yako? Anatoka na wewe out na anakununulia kila aina ya pombe na wakati huo huo hawezi kumruhusu mkewe kunywa pombe ya aina yoyote ile. Akili ya kawaida ikwambie kwamba anafanya hivyo ili ulewe vilivyo na apate wasaa wa kukukandamiza vizuri kitandani.

Dada yangu je mwili wako ni wa majaribio? Anakupa mimba na anakupa pesa uende ukaitoe lakini mke wake akipata mimba nyumbani ni sherehe na anampa pesa za kuandaa martenity dress na vitu vya mtoto.

Dada yangu kumbuka tayari anayo familia yake, kama ulikua hujui jamaa huwaelezea marafiki zake yote mnayofanya hotelini, lakini hata siku moja hawezi kuwalezea yale anayofanya na mkewe. Hii inafanya marafiki zake wakuone kama mwanamke wa hadhi ya chini kabisa.

Unazo picha zake katika simu yako na ume save namba yake kwa majina mazuri kama Sweetheart, My love, etc.Lakini picha zako haziwezi kupatikana ktk simu yake na namba yako amei Save kama Fundi Genereta, Fundi gari, Mzibua Chemba.

Unatakiwa ukumbuke kwamba mwanamke asie na akili sehemu zake za siri ndizo zitakazoumia zaidi.

Amka dada yangu unatumika
Nimeicopy somewhere.
Je ni kweli au wivu tu kwa dada zetu wanaopendwa na hao wanaojiita waume za watu?
 
Wadada wengi wanatizama pesa na mali za waume wa wenzao ndio zinawapagawisha. Na ni hao hao wakiibiwa waume wanalalamika. Tulia umpate wako.
 
Wadada wengi wanatizama pesa na mali za waume wa wenzao ndio zinawapagawisha. Na ni hao hao wakiibiwa waume wanalalamika. Tulia umpate wako.
Teh,there is something behind your post my dear,I guess yule kaka kapata mdada mwingine humu,unamrushia madongo mwenzio?uuupss...okei ngoja niendelee kuangalia
 
Teh,there is something behind your post my dear,I guess yule kaka kapata mdada mwingine humu,unamrushia madongo mwenzio?uuupss...okei ngoja niendelee kuangalia
Jambo usilolijua ni sawa na usiku wa giza. Jifunze tu wakati mwingine kusoma kitu bila kukihusisha na mtu. Sio lazima kila anachoandika mtu kinamuhusu directly. Hii ni jamii usichukulie kila kitu kuwa sahihi kwa hisia zako.
 
Hivi yule kaka mme wa mtu humu aliacha kukusumbua eeh?
Ndugu,usidhani kila aandikacho mtu humu hata akiubeba uhusika ahusika yeye. Hizi I'd tu sometimes ziko mbali na uhalisia kabisa.
Soma ujumbe fanyia kazi ikiwa unakuhusu ujumbe umekufikia ikiwa haukuhusu yupo uliomfikia.
Laiti ungepata nafasi ya kumjua huyu unaemfikiria ungestaajabu labda ni mtu aina gani umlinganishe.
Jifunze kuelewa ujumbe na Sio personal attack. Kwa wanaofikiria critically tayari wamekwisha kukujua kuwa wewe una shida gani psychologically though hutoweza kujijua kiurahisi.
Kuna member aliwahi leta uzi akachambua members wenye psychological problems ambao wanaishi full stressed ambao aliwatambua kupitia michango yao ktk thread za watu.
Naanza kumuelewa.
Soma uzi elewa content changia namna hiyo kinyume chake ni kujidhihirisha ulivo wewe ambapo mtu hatotumia nguvu kukujua unasumbuliwa na nini.
 
Mimi sipendi watu wanaochepuka lakini ni lazima tuelezane ukweli.

Nyie wakina dada/mama mna ila. Mkishaolewa tu mnajibweteza sana.

Ukitoka kazini wala hujitahidi kuona kama dada msaidizi amepika chakula chenye muonjo anaoupenda mumeo. Saa nyingine ile mitomaso ya wakati wa uchumba mume haioni tena. Sasa huyu bwana akipata mchepuko unaomuandalia mahanjulmati mazuri na kupewa attention kama mfalme basi anapagawa.

Kwa hiyo wa daraja la pili ni wewe mke unaeachwa solemba wakati mchepuko unanunuliwa gari, unajengewa nyumba, na wanaweza kuanza familia nyingine huko.

Wanaume kuchepuka ni hulka zao lakini mara nyingi wake mnachangia kiasi kikubwa.

Ni lini mara ya mwisho wewe kama mke umesave hela na kumshtuliza mumeo kuwa weekend hii twende visiwani tukavinjari - my treat? Hakuna. Wanaume wanapenda michepuko kwa sababu wanadekezwa huko. Hapo nyumbani ni ngebe na kejeli tu ndio maana mnawekwa daraja la pili na mchepuko anapandishwa la kwanza.
 
Ndugu,usidhani kila aandikacho mtu humu hata akiubeba uhusika ahusika yeye. Hizi I'd tu sometimes ziko mbali na uhalisia kabisa.
Soma ujumbe fanyia kazi ikiwa unakuhusu ujumbe umekufikia ikiwa haukuhusu yupo uliomfikia.
Laiti ungepata nafasi ya kumjua huyu unaemfikiria ungestaajabu labda ni mtu aina gani umlinganishe.
Jifunze kuelewa ujumbe na Sio personal attack. Kwa wanaofikiria critically tayari wamekwisha kukujua kuwa wewe una shida gani psychologically though hutoweza kujijua kiurahisi.
Kuna member aliwahi leta uzi akachambua members wenye psychological problems ambao wanaishi full stressed ambao aliwatambua kupitia michango yao ktk thread za watu.
Naanza kumuelewa.
Soma uzi elewa content changia namna hiyo kinyume chake ni kujidhihirisha ulivo wewe ambapo mtu hatotumia nguvu kukujua unasumbuliwa na nini.
Mistari miwili kwa essay yote hiii,walahi umevurugwa...sasa hapa nanii anaonekana stressed,teh okei ngoja nipite kimya kimya hayanihusu...
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom