Unapomweleza Machafu yako ya zamani Habib/Habibty wako Huwa tunajenga au tunabomowa?

Nyoka_mzee

JF-Expert Member
Nov 26, 2016
3,695
5,520
Imezoeleka kwa watu wengi wake/waume ,kujikuta mtu anaeleza mambo yake ya nyuma.

Mfano utakuta mtu anakwambia; "mimi usinione hivi Nishapuyanga sana saivi nimeamuwa kustafu,au nishatembea na mwanaume wa kila aina ,.
Au ukute mtu anaanza kukuelezea ,machafu yake yote starehe alizofanya katoa mimba ngapi kaishi na mabwana wa ngapi? hivi hili huwa lina jenga au linabomoa?.

Maana nauliza hivi, maana yupo Dada mmoja (Jina kapuni) ambaye tunaheshimiana sana na amekuwa kama ni ndugu kwangu,Ila amekuwa na Tabia kila mwanaume anayeanza mahusiano naye basi lazima ataanza mweleza historia yake,aliishi na nanii na kama alizaa naye mtoto bahati mbaya basi atayazungumza ,na matokeo yake huishiwa kuachwa na kila mwanaume,
Nimejaribu mshauri aache kuzungumza mambo yalopita hanielewi,anachoniambia hawezi anza mahusiano kwa ulaghai anataka kuwa muwazi,lakini Tangu awe muwazi sijaona anachofaidika nacho zaidi ya kuachwa kila kukicha ...
Ebu tusaidiane wakuu lipi sahihi hapa ? Au mimi ndo nakosea kumshaur ,kwamba anavyofanya ni sahihi?
msaada plz wana jamvii
 
Kila mtu na mtazamo wake...anakupa tahadhari ili cku ukickia alikazwa na mjomba wako usishtuke
 
Swali hili "Hivi haya mambo kakufundisha nani? Ulikua unamfanyia A hivi hivi?" Nahisi linakera watu wa jinsi zote.
 
Back
Top Bottom