Unapoamua kumsaidia mtu kwa ulichobarikiwa

Jayspeed

Senior Member
Feb 23, 2014
156
168
Leo napenda kuongelea swala la mafanikio kupitia mtu yaani mtu aliefanikiwa anapoamua kuwasaidia wengine wafanikiwe kama yeye au hata zaidi yake hasa vijana wanaposaidaiana kama vijana
Cha kushukuru Mungu wapo wengi walioamua kusaidia wengine wafanikiwe kama wao au zaidi mfano mzuri ni @josephkusaga. @ericshigongo @joelnanauka, @mwalimchurchill @masoudkipanya, @jokatemwegelo na wengine wengi walioamua kuwakomboa vijana kwenye umaskini huu

Kuna watu wamefanikiwa sana kila nyanja lakini hawako tayari kushirikiana na watu wengine ili nao wafanikiwe. Watu hawa wana wivu lakini si wivu wa maendeleo, wivu wao ni wivu ule wa kwanini afanikiwe haraka kuliko mimi wivu wa kiubinafsi (selfishness)
Unapotoa mawazo yako kusaidia wengine hata kiimani Mungu hukubariki
Sio kila jambo lina hitaji msaada wa pesa muda mwingine ushauri tu humsaidia mtu kufika anapotaka

Ukiwa umefanikiwa kwenye nyanja zote kihalali na ukaamua kusaidia wengine wafanikiwe kama wewe haiwezi kuathiri mafanikio yako hata kidogo
Na unapoamua kumsaidia mtu amini kuwa anaweza kufanikiwa zaidi yako hilo lisikutie kinyongo hata bali unatakiwa kujipongeza kuwa una mtu ambae atajivunia mafanikio yake kupitia wewe..
Mfano mzuri ni kwa hayati bruce lee mpiganaji wa karate na mcheza filamu mashuhuri alieacha historia mpaka leo ya kuwa mpiganaji karate anaepigana kwa haraka zaidi ..kufanikiwa kwenye karate kwa bruce lee kunatokana na msaada wa mwalimu wake aliejulikana kwa jina la IP Man. Ip Man aliamua atumie msemo wa "Ukitembea peke yako unafika haraka ila ukitembea na wenzako pamoja mnafika salama"

Kufanikiwa kwa bruce kulimfanya mwalimu wake IP Man kujulikana zaidi mpaka kufikia hatua IP Man watu wanatengeneza filamu zake..
msaada alioutoa IP Man kwa bruce ulimsaidia na yeye japo hakutambua hilo yeye alifanya kazi yake kama mwalimu tu basi..
hapo jiulize je IP Man angekataa kumfundisha bruce huenda pasingekuwepo na bruce na pia IP Man jina lake lisingekuwa kubwa hvi leo.. Kubali kitoa msaada unapohitajika na unapotoa msaada toa bila kukumbuka ulimsaidia mtu fulani..mtu uliemsaidia yeye anatakiwa akumbuke nlisaidiwa na mtu fulani

Kuanzia leo writing speech zangu zote zitakuwa znapatikana Insatgram na kisha kuja huku

By Jay Speed
 
Back
Top Bottom