Ahsante Mkuu.Well said Mkuu.
Mwanadamu anavutiwa zaidi na kutazama yale yasiyofaa kwa mwenzake... Umfanyie 99 mazuri afu ukosee moja kuna uwezekano mkubwa sana akawa anakukumbuka kwa lile baya moja Tu.
Mwanadamu anavutiwa zaidi kumhukumu mwenzake kuliko kujitazama yeye kwanza (waswahili washasema ndugu nyani haoni kaliole ..Sio Nyani Ngabu lakini
Nakumbuka maandishi kwenye kitabu fulani.. watu wawili walienda hekaluni kusali.. Mmoja Mfarisayo na mwingine Mtoza ushuru. Yule mfarisayo akaanza kusali ''Nakushukuru Mungu kwa kuwa Mimi sio kama Mtoza ushuru... then akaaendelea kutoa sifa zake anazodhani zinampa stahili yeye, pointi hapa alianza kumponda na kujistahilisha yeye kwanza.
Ni wangapi tunaowanyanyasa n kuwahukumu wafanyakazi wetu wa ndani, wafagiaji ofisini? wahudumu mahotelini na Bar etc? wale walio chini yetu kisa tu tunawaona hawastahili... Vipi wale walio kinyume na sisi?
Asante sana kaka Kitoabu kwa kutukumbusha kuwa sisi hatustahili kuliko wengine.. tena pengine hao tunaowahukumu wana haki na stahili kuliko sisi. Kikubwa tujifunze kujitathimini na kujisahihisha kuliko kuwanyooshea wengine vidole.
Kwan mtu akiwa mwizi hutakiwi kumuita mwizi?..kama mtu malaya unamwita malaya tu hamna kuoneana haya.
Kwa hiyo na wewe ukikuita Malaya utoana pouwa tu
mara nyingi wanaoita wenzao hvyo ndo wale malaya maarufu, asiejua hayo mambo ni wachache mno wenye ujasiri huo wa kutukana matusi makubwa hvyo.Wahanga walionya kua usichopenda kufanyiwa na mwenzio basiujue na mwenzio hapendi umfanyie kitu hicho.
Japokua binaadamu ni kiumbe mpenda sifa lakini hakuna anaependa kupewa sifa ya umalaya.
Sijajua tunatumia vigezo gani kupeana sifa hii, kama ni kweli kama tunavyo kalilishwa kua "malaya" niyule anaetoka/ aliyewahi toka na mpenzi zaidi ya mmoja, je nani anaeweza kukikwepa kikombe hichi? Hivi yupo mmoja wetu katiyetu sisi huku MMU, JF na jamii kiujumla asie wahi badili mpenzi zaidi ya mmoja?
(Yaani tangu aijue starehe hile hajawahi badili ladha nyingine zaidi ya hiyo aliyo nayo kwa sasa) kama yupo mtu huyo huyo anyoshe kidole juu.
Sasa kwanini tunadhubutu kunyoosheana kidole na kuitana "malaya"? Unaupata wapi ujasiri wakumuita mwenzeko"MALAYA"Mwisho.JIFANYEKAMA HAUONI, ILI UISHI VIZURI NA WAPINZANI.