Unapata shida kupanga budget yako na namna ya kuzibiti pesa yako njia hii hapa

Jul 15, 2018
61
127
Kutoka meza ya mdau.
ELIMU YA MATUMIZI YA FEDHA
Fedha inatakiwa uwe na nidhamu nayo katika kuitumia. Kanuni ifuatayo imetumika kwenye vyanzo vyako vyote vya fedha ili uwe na mafanikio yenye amani.

Kanuni
•Fungu la kumi 10%
•Akiba 30%
•Matumizi 40%
•Dharura 10%
•Msaada 5%
•Sadaka 5
Jumla 100%

Hii kanuni inafanya kazi katika kila fedha unayopata kama pato lako la mwezi.

*Mfano* Kama unapata Sh. Laki 5 kwa mwezi (500,000/=) fungu la 10 ni Sh. 50,000/=, hii ni mali ya Mungu si yako. Unatakiwa utoe kanisani kila mwezi, pia hata kama umepewa fedha kama zawadi unapaswa uitolee fungu la 10.

Faida za Fungu la kumi
•Hulinda kazi au biashara unayoifanya dhidi ya adui.
•Magonjwa, ajali(vitu vitakavyokufanya utumie fedha bila mpangilio) n.k yanakuwa mbali nawe.

Akiba 30
•Fedha hii unaiweka kwa matumizi yako ya baadae kama kujenga, kusomesha, kulima, vitega uchumi n.k.
*mfano* kama pato lako kwa mwezi ni sh. 500,000/= asilimia 30 ni sh. 150,000/=

Matumizi 40
•Fedha hii itatumika kwa matumizi ya kila siku, chakula, maji, umeme n.k
•Hutumika pia kwa matumizi mengine ya starehe, mavazi n.k
•Kama pato lako kwa mwezi ni sh. 500,000/=, asilimia 40 ni sh. 200,000/=
• *angalizo* matumizi yasizidi fedha hiyo.

Dharura 10
•Hii ni fedha unayotunza kwa ajili ya mambo usiyoyatalajia kama msiba, magonjwa au kukwama jambo lolote n.k.
•Kama pato lako ni sh. 500,000/= unatunza sh. 50,000/= kwa ajili ya dharura kwa mwezi.

Msaada 5%
•Hii ni fedha ya msaada kwa watu wenye shida; watoto yatima, wajane, walemavu n.k
• kama pato lako kwa mwezi ni sh. 500,000/= unatunza sh. 25,000/= kwa ajili ya msaada.

Sadaka 5%
•Kama pato lako kwa mwezi ni sh. 500,000/= tenga sh. 25,000/= kwa ajili ya sadaka kwa mwezi.
•Igawe fedha hii Mara 4 kwa sababu mwezi una jumapili 4 ambapo utapata ni sh. 6,250/=. Hivyo kila jumapili utaenda kutoa sh. 6,250/=.

Kumbuka;
Kitu chochote kinachoitwa sadaka kiombee kabla hujakitoa kama siku mbili 2 au 3 ndipo uitoe sadaka.
•Jaribu na anza hata na kidogo kidogo, kuwa na nidhamu ya fedha uone nayo itakavyokuheshimu.
MUNGU IBARIKI KAZI YA MIKONO YANGU NA KWA IMANI TUTASHINDA
 
Sawa money planner ingawa mgawanyo wako mbona ume base sana kwenye kutoa sadaka sana
Kama vile
Msaada
Sadaka
Fungu la kumi.
Hapo kwenye akiba (30) na matumizi (40)?
Asante kwa mchanganuo wako.
 
sadaka sio lazima fedha
Kwa hiyo huko kwenye sadaka na msaada leta huku kwenye akiba, alafu bakiza fungu la kumi,
 
Nzuri lakini imelenga zaidi watu wa kundi fulani.

1. Sisi ambao tuna kipato cha Tshs.500,000/= na tunaishi mbali na familia zetu.. umetufikiliaje, maana hiyo 40% haitoshi.

2. Nauli/Mafuta kwenda kazini na kurudi.

3. Sadaka ya Mke/ Watoto!?

4. Kwa sisi ambao tunategemewa na wazazi wetu, umetuweka fungu gani!?

NB: 40% ni unrealistic... huwezi sema ununue chakula, mavazi, viatu na starehe ndogo ndogo ikatosha.
 
Mkuu unaweza uka a
Nzuri lakini imelenga zaidi watu wa kundi fulani.

1. Sisi ambao tuna kipato cha Tshs.500,000/= na tunaishi mbali na familia zetu.. umetufikiliaje, maana hiyo 40% haitoshi.

2. Nauli/Mafuta kwenda kazini na kurudi.

3. Sadaka ya Mke/ Watoto!??

4. Kwa sisi ambao tunategemewa na wazazi wetu, umetuweka fungu gani!?

NB: 40% ni unrealistic... huwezi sema ununue chakula, mavazi, viatu na starehe ndogo ndogo ikatosha.
Unaweza uka adjust kadiri ya mahitaji yako, mazingira na aina ya familia ila hakikisha kila kipengere tajwa hapo juu umekizingatia walau kwa kiasi fulani
Haswa kwa akiba na zarura..


N.B
Mimi niliyeleta mchanganuo si mwandishi halisi wa kazi hiyo
Nimeichukua kutoka kwa mtu ambaye hakujitambulisha na kuedit kidogo tu.
 
Sisi waislamu umetufikiriaje ukisema sadaka zinatolewa jumapili tu? Afu sisi hatuna fungu la kumi ujue.
 
Usafiri tu wa kwenda kazini kwangu na kurudi ni 60,000 kwa mwezi, kuna bajeti ya serengeti lite 3 kila siku,hapo tayari 210,000 hapo bado familia haijala,haijasoma,haijatibiwa,haijaenda kusalimia bibi/babu/ shangazi nk,sijala kazini,sijapigwa mzinga na naomi wa ofisini!! Haitoshi
 
Angalia hii, sadaka na Dhaka asilimia15, akba asilimia5, uwekezaj/mtaj asilimia10, matumz asilimia70; ya kipato chako
 
Yaani Mimi nikatoe fungu la 10 kwa gwajima au mwamposa kwel Mimi naweza kufanya miujiza Kama hyo.. Sina hakika ni Bora hyo fungu la kumi lishuke kwenye akiba tu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom