Unanini nasi we mzungu?

Unanini nasi we mzungu?

umeshusha nondo za kufa mtu kuliko uwezo wangu wa kuzichakata mkuu.
hebu nipe kwa ufupi hitimisho japo nimepitia.
Adui wa mwafrika ni mwafika mwenyewe.

Hakuna mkoloni mzungu au mnyonyaji bila waafrika wenyewe kutengana

Jambo la Msingi ni kuimarisha umoja na mshikamano wetu.

Kazi ya kujenga umoja wetu kwa asilimia kubwa ipo mikononi mwa serikali.
Serikali ikiamua kulisambaratisha taifa ni dakika moja. Serikali ikiamua kuwagawanya watu ili iwe rahisi kwao kutawala ni dakika moja. Ni kugawa hela tu na vyeo kwa yule aliye tayari kuwakomoa wenzake.

Hakuna mkoloni anayeingia mahali bila watawala kufanya makosa ya kuwagawa wananchi.

Kuwa na Taifa Imara ni lazima kwanza tuwapende waafrika wenzetu tunaoishi nao. Huwezi kuwapenda waafrika wa nchi jirani kama unawachukia waafrika walioko ndani ya nchi yako.

Naamini katika mshikamano na umoja wenye kumjali kila mtu.

Sio kila anayepinga au kukosoa basi anastahili kipigwa mabomu na marungu na kuumizwa tu hata bila kutafakari yale anayokosoa kama yana msingi.
Wakati mwingine wale wanaokosoa au kupinga ingekua vizuri wakaitwa wakakaa meza moja na watawala na kujadili kwa kina hata wiki nzima kujadilo tu mstakabali mwema wa nchi kwa pamoja bila kupigana marungu na kuwekana ndani wakati mtawala amepewa tu mamlaka ya kuongoza watu waishi maisha bora yenye furaha na amani moyoni.
Kukaa meza moja na ndugu zako mliohitilafiana sio unyonge wala kupoteza heshima au mamlaka na sio woga Bali ni kujenga umoja na mshikamano.

Tunaweza kabisa kujenga taifa bora lenye kupingana kwa hoja na kukubaliana kutokukubaliana.

Kwa nini waliopewa nguvu ya kidola wasiwe wepesi kuunganisha watu ambazo ni ndugu moja kwa upendo bila kutoa mwanya kwa wa wengine kukimbilia kwa Wazungu ili kuhitaji msaada na kuonewa huruma.

Hivi unafikiri mtu ambaye amepoteza ndugu,wazazi na marafiki wakati huo huo anatafutwa awekwe gerezani tena kwa kipigo kikali kama cha Bob Wine kwa sababu ya kukosa haki ya kulindwa na kuwa huru unategemea ataona umuhimu gani wa amani wakati amani inakuwa kama ina wenyewe. Mtu huyo ni rahisi kuungana na maadui kutoka popote.

Kuna Mtu kwa ujinga tu anamwona Mchina aliyevaa vazi tu la chama chake kuwa ni bora kuliko Mtanzania na mwafrika mwenzake ambaye huenda hata wajukuu zake wataoana na kuwa familia moja!

Turejeshe upendo wetu kama watanzania na waafrika ili tujenge uzalendo kwa nchi zetu.
Hakuna cha Muzungu wala Muchina atakayekuja kupora utaifa wetu na kutujengea uhasama.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyu jamaa alitutawala akatunyonya na kutumaskinisha kwa viwango vya juu.
Hajawahi kutulipa fidia tumekubali yaishe.


Sasa cha ajabu hadi Sasa Bado anatufuatilia tu. Anakwamisha miradi yetu, anatupa mikopo ya masharti nyonyevu.

Kama haitoshi anaharibu kabisa vijana na vizazi vijavyo kwa maushoga na usagaji, kubomoa mizizi ya maadili yetu. Leo hata kijana akichumbia hadi ampigie magoti mke mtarajiwa huku akimvisha kipete.

Unarubuni vijana wetu wanakuwa vibaraka wako.


Unanini nasi mzungu, si utuache tuendelee na ishu zetu jamani
umasikini wako mzungu hahusik hata kidogo mbona kuna nchi zilitawaliwa kama sisi lakini leo hazikamatiki kiuchumi!??umasikini wako ua umasikini wetu unaletwa na viongozi wenye maono mabovu wasio na mitazamo na fikra pevu
 
umasikini wako mzungu hahusik hata kidogo mbona kuna nchi zilitawaliwa kama sisi lakini leo hazikamatiki kiuchumi!??umasikini wako ua umasikini wetu unaletwa na viongozi wenye maono mabovu wasio na mitazamo na fikra pevu
tatizo sio viongozi mkuu.
tatizo ni familia.
mzungu anatupigia hapo hapo,
mzungu anatakiwa atuhurumie mkuu. sio kufanyana fursa kwa udhaifu wa mwenzako aisee. sio fair kabisa mkuu.
 
Kwa hiyo uwezo wako wa kufikiri mtoa mada umeishia kwenye kuwalaumu wazungu? Hii haina tofauti na ramli chonganishi.
uwezo wa mada umeishia kuwalaumu wazungu sio uwezo wangu mkuu.
kuwqchnganisha wabongo na wazungu ni hatua nzuri kuelekea ushindi au kupata majibu sahihi bosi.
 
mkuu mzungu hajali, anaweza kuwapanga tena akawapa walibya za usoo tena na kuchikichia zake kusikojulikana.
mimi nieshuhudia lizungu jingajinga tu, ila lilivyogeuka na kutawala kila mtu hadi leo hakuna anayejua.
Hahah et jinga jinga hahaha u made my day

Tatizo haya majamaa ni majanja janja sana.
Saiv yameingia na gia ya kutoa misaada aisee
 
uwezo wa mada umeishia kuwalaumu wazungu sio uwezo wangu mkuu.
kuwqchnganisha wabongo na wazungu ni hatua nzuri kuelekea ushindi au kupata majibu sahihi bosi.
Sikubaliani na mtazamo wako ila naheshimu mawazo yako.
 
ndio maana niko macho mkuu. sitaki ujinga. Hata mimi mwenyewe sijiamini namwamini Mungu tu.
yaani ukizubaa tu, unaweza kujikuta mateka wa mikakati ya wazungu. Ukiwakwepa utakutana na wagagagigikoko wa huku bongo ambao ukipiga hatua WANANUNA, Ukifeli wanasherekea.
Ila mkuu wazungu noma zaidi, maana wakiamua kuipiga ngwala CCM hata kesho mbali.
Mungu mwenyewe umeletewa!!
Ova...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom