Unanini nasi we mzungu?

Unanini nasi we mzungu?

matunduizi

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2018
Posts
9,514
Reaction score
23,525
Huyu jamaa alitutawala akatunyonya na kutumaskinisha kwa viwango vya juu.
Hajawahi kutulipa fidia tumekubali yaishe.

Sasa cha ajabu hadi Sasa Bado anatufuatilia tu. Anakwamisha miradi yetu, anatupa mikopo ya masharti nyonyevu.

Kama haitoshi anaharibu kabisa vijana na vizazi vijavyo kwa maushoga na usagaji, kubomoa mizizi ya maadili yetu. Leo hata kijana akichumbia hadi ampigie magoti mke mtarajiwa huku akimvisha kipete.

Unarubuni vijana wetu wanakuwa vibaraka wako.

Unanini nasi mzungu, si utuache tuendelee na ishu zetu jamani
 
Naona una-revise notes zako za History of Africa before the 19th C
hahahah
hapana mkuu, hata mkuu wetu amelaani sana hiyo leo pale mwanza south. wajinga sana hawa jamaa.
wanatuchulia poa sana.
 
Mzungu yeye hajali ujinga wako anawekeza kwenye ujinga wako huohuo, huwezi kuwekeza kwa mjanja na ukafanikiwa
kweli mkuu hawa jamaa hawana utu.
unavyolegea ndivyo unavyotafunwa. ukijitoa fahamu ukajifanya hamnazo wanakugeuza supu kabisa.
hawa jamaa Mola anawaona.
wao ni wazee wa win-loose tu kila kitu hadi makanisani.
 
jaribu kumpeleka kortini huyo 'Jamaa' yako...huenda fidia ikatoka
 
Sio wazungu tu hata waswahili wenzetu, ndiyo maana ccm inaendelea kututawala
ndio maana niko macho mkuu. sitaki ujinga. Hata mimi mwenyewe sijiamini namwamini Mungu tu.
yaani ukizubaa tu, unaweza kujikuta mateka wa mikakati ya wazungu. Ukiwakwepa utakutana na wagagagigikoko wa huku bongo ambao ukipiga hatua WANANUNA, Ukifeli wanasherekea.
Ila mkuu wazungu noma zaidi, maana wakiamua kuipiga ngwala CCM hata kesho mbali.
 
Tena bora ya mzungu kuliko mswahili, hebu angalia wakina chenge na wenzake walivyochota hela na hakuna wa kuwagusa
 
Kama tutaweza kuachana na mambo yao yote waliyotuletea basi tuwatangaze kuwa ni watu wabaya sana.

Lakini kama mambo mambo waliyotuletea ndiyo tunayoyatumia kwa manufaa binafsi na familia binafsi . Na kwa hakika wanufaika Wakuu wa mifumo ya kikoloni ni watawala sio wananchi. Mwananchi wa kawaida hata pasipokua na mfumo wowote anaishi tu na kulima viazi vyake vya asili na kula hana shida ya kupanda midege kwenda ulaya au matreni ya mwendo kasi. Hayo yote ni taamaa zetu za kutaka kuwa kama wakoloni wetu unaowakejeli.

Kama pia tutaweza kuachana na utawala na mifumo ya kikoloni ya kuwa na mihimili mitatu ya dola basi tutawakeji na kuwaambia waachane na sisi. Turudi kwa machifu wetu wa zamani tuanze kuporana mifugo na wanawake. Kila kabila lijitawale kupitia machifu.

Yani Chifua Mazengo awe na nchi yake na Chifu Kimweri nchi yake.

Mkwawa awe na nchi yake na Mirambo nchi yake.
Tuachane na silaha walizowaletea watawala wanaozitumia kiwaangamiza wananchi wao kwa mabomu na marugu na risasi za moto za Mzungu na mwarabu.
Turudi kwenye zana zetu za asili za ngao na pinde na mishale na mikuki.

Tusihangaile tena na matumizi ya miundo mbinu iliyoanzishwa na serikali ya mkoloni.
Karibu miji yote ya mikoa na wilaya ilianzishwa na wakoloni.

Master plani za miji mingi na maeneo yenye rasilimali zilianinishwa na ramani za wakoloni.
Tuachane na mipaka aloanzisha mkoloni twende Uganda tukachimbe dhahabu tukiulizwa tujibu majibu mepesi kuwa hatutaki mambo yaliyoasisiwa na wakoloni.

Kifupi tu ni kwamba kama mifumo yote tunayotumia kuanzia ramani za nchi zetu na mifumo ya kidola na kiutawala ni ile ya mkoloni waliyotuletea tukaipenda na kuamua kuwafukuza ili tutawaliwe na wakoloni wenzetu weusi basi ni lazima kukubali kukosolewa na hata kuongozwa na kushauriwa na waasisi wa mifumo ya kuendesha kile kinachoitwa serikali na mifumo iliyowekwa kikatiba mana waasisi wa hiyo mifumo ni yao wazungu.

Lakini haiwezekani kujiendesha kama kisiwa wakati tunatumia mifumo yao yote kuanzia ulinzi ,mawasiliano , mahakama,bunge,dini na hata kipimo cha maendeleo ni kile kinachotokana na elimu ya mkoloni.
Hata rasilimali zetu wateja wake ni hao wakoloni wetu wa zamani. Bila mkoloni wetu kuweka thamani ya Tanzanite basi hayo madini yatabaki kama mbaazi.

Kwa sasa dunia ni kijiji tuache kuhubiri chuki dhidi ya binadamu wenzetu. Tusiiaminishe jamii yetu iliyojaa wajinga wengi kuwa adui yetu mkubwa ni mzungu wakati hatuna elimu ya kutosha wala teknolojia. Tuwape watu wetu elimu bora lakini sio kuwachonganisha na binadamu wenzetu .
Ndio maana Trump anachukiwa karibu dunia nzima kwa sababu ya matamko yake ya kibaguzi na ya kujenga chuki na dharau kwa binadamu wengine.
Nchi yetu ni maskini. Walitawala watangulizi wengine na wakaimarisha diplomasia na nchi nyingine na tukaendelea kuishi kwa amani kwenye nchi yetu.

Hata sisi tunapenda watoto wetu nao waende huko ng'ambo kupata elimu na ujuzi zaidi ili nao waje kuwa mawaziri na makatibu wa wizara. Nyie mmeshiba na familia zenu na mnategemea siasa muda wote kula mema ya nchi. Acheni taifa letu liendelee kuwa na mahusiano mazuri na mataifa mengine yaliyoendelea. Na muwaachi watufundishe namna bora ya kufanya ukoloni sio huu wa kutiana umaskini na vitisho kwa kupendeleana wakati sisi wote ni waafrika. Kosa moja anafanya mtu Fulani anaachwa kama vile ni mkoloni mzungu kati ya watumwa waafrika.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
umeshusha nondo za kufa mtu kuliko uwezo wangu wa kuzichakata mkuu.
hebu nipe kwa ufupi hitimisho japo nimepitia.
 
K

Kwel kabsa huyu jamaa ni kweree.ila alichowafanyia wa Libya hawatasahau😀
mkuu mzungu hajali, anaweza kuwapanga tena akawapa walibya za usoo tena na kuchikichia zake kusikojulikana.
mimi nieshuhudia lizungu jingajinga tu, ila lilivyogeuka na kutawala kila mtu hadi leo hakuna anayejua.
 
hafai mzungu mkuu.
bingwa wa kukufanya rafiki, kuja kushtuka umebaki skeletoni.
huu ujinga amemuambukiza mchina.
Na hata ukibaki skeleton hakuachi ng'oo ataendelea kuwekeza kwenye hizo skeleton zako, usicheze na mzungu wewe
 
😡😡😡
hatarii.
anaweza kusaga skeletoni ikawa unga akalishia bloila.
hana muda huyu mpuuzi. nikiwa nae karibu huwa nakuwa katika emergency mode.
ila hawa wabongo na vifitna vyao hawana lolote, mzungu mwisho mkuu.
😀😀
 
Back
Top Bottom