Emc2
JF-Expert Member
- Sep 26, 2011
- 16,808
- 16,951
Wanadamu tumeumbwa kuwa na matamanio, kutamani kufikia ndoto yako. Lakini kwenda kufikia kwenye ndoto lazima kunavitu hapa katikati lazima vifanyike. Huwezi ukajikuta tu umefikia kile unachotamani. Ukiwa unapesa nyingi, kidogo au hauna kabisa unawaza siku moja ufikie unapopataka.
Leo ninapenda kuongelea kutumia kitu ulicho nacho kutatua matatizo yanayokuzunguka. Kwa wasomaji wa vitabu vya dini mtakumbuka kulikuwa na safari ya wana wa israel kutoka misri kuelekea kanani, ilifika sehemu nyuma kunamaadui, mbele kunabahari halafu pembeni milima.
Watu wakaanza kumlilia Musa naye Musa akaanza kumlilia Mungu. Basi Mungu kamwambia unanini mkononi? Akasema fimbo. Akaambiwa yapige hayo maji na fimbo yako.
Katika hii stori tunajifunza kutumia kile ulicho nacho kufanya kitu kikubwa. Kuna baadhi ya watu wanatamani kufanya biashara lakini wanaona pesa zao bado hazijatimia. Wanasubiria ili ziweze kutimia waweze kufanya biashara. Kuna kitu kwa kiingereza kinaitwa "Dead Rock" You wait something which will not happen. Knamsemo wa kiswahili unasema Fimbo ya mbali haiui nyoka.
Tumia kile ulichonacho uweze kufanya mambo makubwa. Nguvu ya kufanya mambo makubwa ipo ndani ya maamuzi. Ukiamua sasa nataka kufanya kitu flani, hakika utakifanya. Maamuzi tena maamuzi sahihi. Unajua kunamaamuzi mengine sio sahihi kabisa kwa mfano mimi hapa Annael eti ninaamua nikaae ndani ya maji ya bahari siku saba niwe kama samaki. Hii haiwezekani hata siku moja.
Kuna wakati unakaa tuu sehemu, huna pesa huna chochote lakini wakati huo unanguvu, umemaliza chuo. Hivi kweli haiwezekani kufundisha tuition mitaani? au haiwezekani kweli kutumia nguvu nilizo nazo kujipatia kipato. Badala ya kusubiria kitu ambacho hakipo.
Kwa wasomaji wa biblia mtakubaliana na mimi kuwa kunasehemu imeandikwa aliyenacho huongezewa, asiye nacho na kile anadhani yuko nacho huondolewa. Hii inatufundisha kutotegemea kitu ambacho hakipo. Kile ulicho nacho ni nguvu kubwa sana katika chachu ya kukufanya usonge mbele.
Tumia ulicho nacho usisubiri ambacho hauna