Unalifahamu kundi la UB40?

Nyimbo za UB40 nizipendazo ni pamoja na Red Red Wine, Here I'm Baby, I Got You Baby, If it Happens Again, Sing Our Own Song na Tell it Like it is.

Huyo Chrissie Hynde aliyewaona UB40 na kisha kuamua kuwafadhili ndiye aliimba nao wimbo wa "I Got You Baby".

Pia Chrissie Hynde akiwa na kundi lake la The Prentenders wametoa vibao vingi sana. Mwezi July 1985, UB40 na The Prentenders walishiriki onyesho moja kubwa sana lililoitwa "Live Aid" ambalo ilifanyika Wembley Stadium nchini Uingereza ili kuchangia wahanga wa njaa nchini Ethiopia. Kati ya nyimbo zilizoimbwa na The Prentenders kwenye tamasha hilo ni pamoja na "Message of Love", "Stop Your Sobbing" na "Talk of the Town".

Washiriki wengine katika tamasha hilo walikuwa ni mzaliwa wa Zanzibar Freddie Mercury na kundi lake la Queen, Mark Knopfler na kundi lake la Dire Straits, The Beach Boys, Bono na kundi lake la U2, David Bowie, The Who, Simple Minds, Madonna, Phil Collins, Paul Young na Santana kwa uchache.
 
Nilienda kwenye concert yao .
I had a great time.
I love UB40.

Sikuwa najua sana historia yao nimejifunza mengi asante .
mimi pia nliwahi kwenda kwa concert yao kwa kweli sintokaa nisahau. Nashkuru zidi kutembelea MTOKAMBALI kwa mengi kuhusiana na MAISHA, MUZIKI, AFYA NA MENGINE MEENGI .
 
Msondo Ngoma wanaimba Ila wapate pombe Na mademu
HA HA HA HAAAAAAAAAAAAAAAA
Dah! aksante sana ndugu wewe ni muziki na muziki ni wewe. I like that.
 
HA HA HA HAAAAAAAAAAAAAAAA

Dah! aksante sana ndugu wewe ni muziki na muziki ni wewe. I like that.
Nafikiri mwezi wa 10 Mwaka Jana, nilienda kuwaona Msondo Ngoma, aisee wamechakaa vibaya sana. Baba yake Chid Benz Na Romario wamelewa vibaya sana sasa sijui ni stress au ndio stimu, maana wenyewe ndio wakongwe waliobaki Na hawana Hali.
 
Kumbe baba yake Chid Benz nae ni mwanamuziki na yuko Msondo?
 
Nafikiri mwezi wa 10 Mwaka Jana, nilienda kuwaona Msondo Ngoma, aisee wamechakaa vibaya sana. Baba yake Chid Benz Na Romario wamelewa vibaya sana sasa sijui ni stress au ndio stimu, maana wenyewe ndio wakongwe waliobaki Na hawana Hali.
Tatizo ni kwamba waliokua wakiiamsha msondo wote washatangulia mbele za haki.
 
Hebu ongea na moderator akusaidie kurekebisha heading
 
Ninachofahamu juu ya UB 40 ni kwamba kuna jamaa mmoja alikuwa mahiri saana kwa kuimba kwenye safu ya mbele akiitwa Ali Campbell almaarufu kama the "Voice of UB 40" na punde baada ya jamaa kuwamwaga na kundi likafia hapo.

Nadhani ukisikiliza kwa umakini nyimbo nyingi za UB 40 utagundua kuna sauti unaisikia zaidi kuliko zingine basi huyo ndo Ali Campbell.

Nawakubali saana UB 40.
 
Huyu hapa dio Ali Campbell, kwenye picha hiyo ya wengi ndie anaeonekana wa kwanza alikuwa lead singer watu wakampachika jina la "The voice of UB 40".

Cheers!
 
Attachments

  • 1459449700786.jpg
    6.5 KB · Views: 41
  • 1459449711486.jpg
    7.9 KB · Views: 34
Mid nakipenda kibao cha wise man say a.k.a I can't help falling in love with you yaani sauti, midundo na vyombo vyake sichoki kuusikiliza. Ingawa wimbo wenyewe kiuhalisia ulianza imbwa na Elvis presley
 
yeah
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…