Hiyo vita ilinikuta katika eneo hilo na nakumbuka mgogoro ulianzia siku ile Askofu Kweka alialikwa kuja Usa River kuweka jiwe la msingi, nilikuwepo siku hiyo katika eneo la tukio, lakini kulikuwa na minong'ono ya chini kwa chini watu wakipinga ujio wake. baada ya kuweka hilo jiwe la msingi msafara ukaondika kwenda katika kumbi wa sherehe kwa ajili ya maakuli. huku nyuma wahafidhina wakaling'oa lile jiwe la msingi na kulifunga kwenye bahasha na kulipeleka nyumbani kwake na kumkabidhi mkewe kuwa ni mzigo wa mzee. Askofu Kweka aliporudi nyumbani kwake jioni ndio akakutana na hilo jiwe la msingi alilotoka kuliweka. ikabidi mkakati wa ulinzi madhubuti ufanywe na jiwe la msingi likawekwa chini ya FFU na ulinzi ukaimarishwa hadi likakauka. Kimbembe ndio kikaanzia hapo na watu kuanza kuchomana mishale na kukatana kwa mapanga. Nakumbuka alikuja Waziri mkuu mzee Malecela baada ya kutumwa na Raisi wa wakati huo Ali Hassan Mwinyi. Wakati akiwa mkoani Arusha akijaribu kutatua mgogoro huo, ndipo ilipotokea ile ajali mbaya iliyohusisha Familia ya mzee mmoja tajiri niliyemfahamu kwa jina moja la RIMOY ambapo familia yake ya watoto watano kama sikosei na mkewe walipoteza maisha katika eneo la njia panda ya MOMELA ikihusisha basi na gari dogo la huyo mzee. Ni bahati tu, ni yule mzee pekee aliyenusurika katika ajali hiyo na alilazwa katika hospitali ya KCMC. Ni wakati huo akijaribu kususluhisha mgogoro huo Mzee Malecela alikwenda kumjulia hali huyo mzee na kumpa pole kwa kupoteza familia yake katika ajali hiyo. Alikuwa ni waziri wa Mambo ya Ndani pekee aliyeweza kutatua ule mgogoro. Chanzo cha mgogoro huo ni kuonekana kwamba makao makuu ya dayosisi yaliyokuwa mkoani Kilimanjaro yamejaa wachaga na misaada mingi inaelekezwa kwenye makanisa ya mkoani Kilimanjaro na yale ya Meru yakiwa yametelekezwa. Walikuwa na malalamiko mengi sana wakati huo na walikuwa wanapinga uongozi wa Askofu Kweka waziwazi.... Nawasilisha.............