Assalaaam alykum.
Ndugu yangu, hakuna shaka siku moja watu watakusanyika kwa ajili ya kifo chako.
Na tambua kuwa kaburi lako ndo kituo cha kwanza katika maisha ya akhera, maisha yenye tabu na mashaka kama hukuwa na maandalizi mema na yatakuwa ya raha na amani kama ulijiandaa vyema.
Kwa hiyo kuna haja kubwa mno kuwa na muda wa kutafakari ni kwa namna gani tunaandaa maisha yetu baada ya kufa kwetu.
Wengi mmebahatika kwenda shule hadi level mbalimbali, mkiwa shule mlikuwa mnafaulu si kwa bahati mbaya bali kwa mikakati na mahesabu ya hali ya juu kwa taufiq ya Allah, Basi mahesabu na mikakati inafaa zaidi itumike kwenye kutafuta pepo na kuuepuka moto kwa msaada wa Allah mtukufu.
UZI HUU NI KWA AJILI YA kuusiana sisi waislamu kwenye mambo mbalimbali hasa ni vipi Tutatumia vyema UHAI huu wa muda mfupi kwa ajili ya kunufaika nao baada ya kufa kwetu.
Dunia ni kama tupo tunafanya open exam, na kila mtu ana muda wake maalum wa kufanya hii open exam. Na majibu ya kujaza yapo waziii. Tutumie wakati vizuri kwan hatujui lini tutaambiwa stop (writing).
KIUFUPI ni kwamba ikiwa wewe unapata uzito kwenye kutekeleza ibada fulani kama swala n.k basi waweza kuwashirikisha ndugu zako hapa wakakushauri wao wanafanikiwa vipi, kuliko kushinda ukihangaika na mambo ambayo hayana faida na wewe.
Lakini tujue kutekeleza ibada si ujanja bali ni taufiq ya Allah, Namuomba Allah atuwafikishe sote tudumu katika kumtwii yeye katika maamrisho na makatazo yake. Na atufanyie wepesi kuziendea kheri na kuepuka mambo ya haraam. Atusamehe madhambi yetu na Atuzawadie mwisho mwemaa. Aaamiiiin.
Nilipoteleza nibainishieni na Allah anisamehe.
Allah mtukufu ndiye mjuzi.