Unakumbuka haya maneno ya Nyerere? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Unakumbuka haya maneno ya Nyerere?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by massai, Apr 30, 2012.

 1. m

  massai JF-Expert Member

  #1
  Apr 30, 2012
  Joined: May 2, 2011
  Messages: 655
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  leo wazanzibari wanaandamana hawataki muungano,watanganyika wanasema muungano si halali na hauna manufaa,vipi juliasi angekua hai haya mambo yangezungumzwa kwa staili gani?.sikumbuki ni mwaka gani,wabunge walikua wakiujadili muungano.Nyerere aliingia bila taarifa ndani ya bunge akasema anaetaka muungano akae huku na asietaka muungano akae huku,vipi angekua hai leo tungesikia kauli gani kuhusu matamko yake??
   
 2. Escobar

  Escobar JF-Expert Member

  #2
  Apr 30, 2012
  Joined: Sep 16, 2011
  Messages: 576
  Likes Received: 217
  Trophy Points: 60
  Mkuu hiyo mbona simpo tu, ingekuwa leo ndio kauliza mimi ningekaa upande huu!
   
 3. Jaji

  Jaji Senior Member

  #3
  May 1, 2012
  Joined: Sep 4, 2011
  Messages: 138
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ila magamba wangemuogopa....
   
 4. M

  Massenberg JF-Expert Member

  #4
  May 1, 2012
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 1,173
  Likes Received: 1,061
  Trophy Points: 280
  Nyerere baba yake nani? Hakuna mwenye akili za kisasa ambaye angemsikiliza, sana sana angeulizwa alete hati ya muungano na aseme lini ilifanyika kura ya maoni kujua kama watu waliutaka huo muungano wake.
   
 5. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #5
  May 1, 2012
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,650
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Hivi kwa nini kuna watu wanaogopa sana referendum ya muungano?

  Watu waamue wenyewe kama wanautaka muungano au la. Hakuna ubaya wowote kabisa kwenye hilo.
   
 6. kibol

  kibol JF-Expert Member

  #6
  May 1, 2012
  Joined: Apr 24, 2012
  Messages: 3,137
  Likes Received: 379
  Trophy Points: 180
  mimi mwenyewe na propose watu wapewe uhuru waamue ama kusuka au kunyoa,sijui viongozi wetu wanahofia kitu gani.
   
 7. Xuma

  Xuma JF-Expert Member

  #7
  May 1, 2012
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 631
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  muungano hauna maana kwa sasa japokuwa ukiwekwa sawa ni dili kubwa kwa Tanganyika!
   
 8. Gang Chomba

  Gang Chomba JF-Expert Member

  #8
  May 1, 2012
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 8,790
  Likes Received: 810
  Trophy Points: 280
  Hayati Karume aliwaambia wazenji kuwa ''MUUNGANO NI KAMA KOTI, LIKIKUBANA LIVUE''...
  Na ndio maana poyoyo wale wakiikumbuka kauli hii basi ni lazima waandamane kutaka Muungzno uvunjike.
   
 9. K

  KISUNGURA Member

  #9
  May 1, 2012
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 32
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Nyerere alikuwepo enzi za WADANGANYIKA lakini kwa sasa hawezi kuwaletea upuuzi huo WATANGANYIKA.
   
 10. F

  FICUS CAPENSIS New Member

  #10
  May 1, 2012
  Joined: May 1, 2012
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mwl Nyerere aliota na kuishi ndoto na Tanzania anayotaka kuwaachia wajukuu na vitukuu hadi vilembwe vyake. Ni kweli kama tungekimbilia ubepari na kuachana na dhana ya ujamaa tusingekuwa hapa tulipo? na je hivi matamanio ya mwl hayatekelezeki bali ninadharia tu?? Ukiwa kama mtanzania unafikiri tumepiga hatua kwenda mbele au nyuma toka mwl atutoke?tama dhana ya mwl ya uwajibikaji wa viongozi ilikuwa ni udikteta?Kwani leo tunaona mawaziri wakikosa msimamo wa pamoja katika mambo ya msingi ya nchi hasa swala la dowans na mengineyo. wanajamii mnafikiri Tanzania tuiendeayo vizazi vya nyuma yetu vitamlaumu nani? Je kama wanajamii tunanafasi gani ya kuwajuza wenzetu ili kwa michakato iliyopo ya Katiba na upepo wa mageuzi ya fikra mgando hapo awali tuijenge Tanzania ya ndoto za Mwl Nyerere? Leo deni la taifa linakuwa kila kukicha,inakadiriwa kila mtanzania atapaswa kuchangia milioni 350 kwa deni linalokadiriwa kufikia trilioni 16, na watanzania milioni 40.

  Unafikiri tunaweza? Mimi nasema tunaweza. Tafakari unachangia nini ili kujenga Tanzania mpya yenye kuheshimu utu wa mtu katika misingi ya kidemokrasia na uwajibikaji wa viongozi kwa mali na rasilimali za nchi kwa uma?
  Naitafuta Tanzania ya ndoto za mwl. Je waijua?
   
 11. n

  nketi JF-Expert Member

  #11
  May 1, 2012
  Joined: Feb 15, 2012
  Messages: 555
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  aaagh......
   
 12. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #12
  May 1, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  nyerere alitufanyia mengi sana enzi hizo but wakati ule msomi alikua peke yake angekua hai leo hii angeona jinsi ambavyo watz wasomi wanajua maendeleo na hatuna akili za kiconservatives ka za kwake...with all due respect yeye pia amechangia kua nyuma kimaendeleo ukilinganisha na nchi zingine za afrika au ulimwenguni...so sio kila kitu angesema tungemsikiliza
   
 13. b

  bdo JF-Expert Member

  #13
  May 1, 2012
  Joined: Nov 20, 2006
  Messages: 5,712
  Likes Received: 1,611
  Trophy Points: 280
  hizo kura za maoni mara nyingi zinachelewesha mambo...kila kitu kura za maoni?
   
 14. b

  bdo JF-Expert Member

  #14
  May 1, 2012
  Joined: Nov 20, 2006
  Messages: 5,712
  Likes Received: 1,611
  Trophy Points: 280
  nenda kalale wewe... unazungumzia wasomi gani?Dr. Kawambwa, Prof.Maghembe, Dr. Mathayo D. Matayo, Dr. Nagu, Dr.Nchimbi, Dr.kya, Dr. Haji Mponda?etc au Dr. Bana -UDSM? , wameshindwa hata kukemea wizi wa halmashauri, lete hoja ingine tafadhali
   
 15. N

  Ningu Member

  #15
  May 1, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 75
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hivi mipaka ya Tanganyika na Zanzibar ipo wapi? Nauliza hivi kwa sababu hata kama nchi hizi ziliungana basi zilikuwa na mipaka yake! Mbina ramani hazioneshi..? Au mtoto wa mkulima alikuwa sahihi aliposema Zanzibar si nchi!
   
 16. Edward Teller

  Edward Teller JF-Expert Member

  #16
  May 1, 2012
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 3,818
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  utakuwa dili kivipi?
   
 17. m

  massai JF-Expert Member

  #17
  May 1, 2012
  Joined: May 2, 2011
  Messages: 655
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  changamoto ni kubwa sana mkuu,nikiangalia toka mwalimu atutoke hakuna hatua tuliyopiga kwenda mbele,1.kama ni suala la uchumi bado tupo kwenye hali tete sana,tumeshindwa kuuinua uchumi kwa raslimali tulizonazo na sanasana ni tumejiongezea madeni badala ya kuyamaliza kabisa.dhahabu zimeisha au zinakaribia kuisha bado deni linazidi kukua.2.elimu tuliyonayo sasa ni sawa na maigizo,tuna maprofesor ambao wamefoji vyeti na wanavaa milegezo,kuna elimu hapo.3.hatuna uzalendo,watu wanakwiba na kuwekeza kwenye mabenki ya nje.mgeni anathaminiwa kvliko mwenyeji.ubinafsishaji uliopo ni sawa na ukoloni kwani hauna manufaa kwa mzawa yaidi ya manyanyaso kwa ujira mdogo
   
 18. m

  massai JF-Expert Member

  #18
  May 1, 2012
  Joined: May 2, 2011
  Messages: 655
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  hakika wasomi wa enzi ya nyerere huwezi linganisha na hayo matakataka uliyoyaorodhesha hata kidogo.hakuna doctor hapo wala profesor wote vilaza hao,angali undani wao utakuta ni wamefoji vyeti na vyuo walipopata hayo masomo ni vya kata.wezi hao hakuna mzalendo hata mmoja hapo
   
 19. m

  massai JF-Expert Member

  #19
  May 1, 2012
  Joined: May 2, 2011
  Messages: 655
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  lazima muungano ujadiliwe kwa kupigwa kura ya kuukubali au kuukataa,hiln halipingiki wanajitahidi kuuchelewesha tu alakini time will tell...
   
Loading...