Unakula na kusaza, jirani kala nini...? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Unakula na kusaza, jirani kala nini...?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mtambuzi, Oct 4, 2012.

 1. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #1
  Oct 4, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Wengi wetu tuna kwenda misikitini, makanisani, na hata jamatini na kwenye mahekalu au kutambika. Kote huko lugha ya upendo inazungumzwa sana. vitabu vyetu vitukufu vinatuambia kwamba ni jambo muafaka na heri zaidi kuwapenda jirani zetu kama sisi tunavyo jipenda wenyewe. Jirani zetu kwenye vitabu hivyo ina maana ya mtu yeyote ambaye uko naye katika kipindi husika. Hii ina maana kwamba tunashauriwa kumpenda kila mtu mahali popote tulipo na alipo.

  Lakini jambo la ajabu na linalo sikitisha ni kwamba ni wachache sana kati yetu ambao wana upendo kwa watu wengine zaidi ya nafsi zao. Kila mmoja kati yetu anataka kuhakikisha kwamba amepata nafasi amefaidika yeye na kuridhisha nafsi yake kwa mapana yote ndipo amfikirie au kumkumbuka mwingine, kama hata hivyo itatokea kumfikiria au kumkumbuka huyo mwingine.

  Leo hii Tanzania iliyokua ikiamini katika thamani ya mtu kwa utu wake na mchango wake kwa jamii imebadilika na kuanza kuamini katika mali kama kigezo mahususi cha kupimia utu wa mtu. Leo hii kila mmoja anajitahidi kwa njia yoyote apate mali ili kuhuisha thamani yake. Katika juhudi hizi wengi wetu tumejikuta tukitoka katika ubinadamu na kuingia kwenye hali ya unyama halisi.

  Pengo kati ya wale walionacho na wasionacho linazidi kuwa kubwa kila kukicha. Walionacho kwa bahati mbaya wanazidi kujilimbikizia na kutapanya mali walizonazo kwa nia ya kufurahisha nafsi zao zaidi bila kujua kwamba pembeni kuna wengi ambao ndio waliowafanya wao kuwa nacho wakipiga mikambi ya kifo kwa njaa na maradhi.

  Kila aliye nacho leo anajitahidi kushindana na mwingine kutokana na udhaifu wa nafsi. anataka kujenga nyumba ya ghorofa anataka kununua gari la milioni mia moja zuri zaidi ya lile la mwingine, anataka kusafiri ulaya kutalii kila baada ya mwezi mmoja, zaidi ya yule mwenzake anayekwenda kila baada ya miezi mitatu.Imefika mahali ambapo sio dhambi hata kidogo kwetu kujiuliza kama kuna ridhiko la kweli la moyo kwetu sisi kufanya "matanuzi" yaliyopindukia wakati kuna wale waliotuzunguka ambao wangetamani kupata hata moja ya milioni kumi ya kile ulicho nacho ili nao waweze kuishi kama binadamu.

  Inakuwaje basi tunathubutu kwenda kanisani au misikitini na kupiga goti au kusujudu tukimwomba Mungu mwenye upendo atupe nusura, wakati mioyo yetu ni migumu kiasi hicho!
  Naona umefika wakati ambapo wale walionacho wanatakiwa wajiulize wanajisikia vipi kuona kwamba wamezungukwa na watu wenye dhiki na mateso. Wanafaidi kitu gani katikati ya ulitima wa wengine? Je, kweli watayaita hayo walio nayo ni mafanikio, wakati wanajua wazi kabisa kwamba wangeweza kutoa hata moja kwa milioni ya kile walichonacho ili kuwasaidia wengine, lakini kamwe hawajawahi kufanya hivyo?

  Tujifunze kujiuliza kila siku swali hili; mimi ninakula na kusaza, je jirani ana uwezo wa kupata hata kile ninachosaza mimi?
   
 2. lara 1

  lara 1 JF-Expert Member

  #2
  Oct 4, 2012
  Joined: Jun 10, 2012
  Messages: 15,444
  Likes Received: 10,122
  Trophy Points: 280
  Bwana awe nawe mchana wa Leo!!!, manake NIMTOKA KUMSINDIKIZA MTU KWA MTAALAMU WA KIENYEJI AKAMALIZE JIRANI YAKE (USHOGA KAZIIIII!) mchana huu huu, alafu kuingia humu, nakutana na Ujumbe mkali toka kwako! Kidogo nimpigie alieenda kumalizwa, ila nimeghairi najishika ninaposhikiliwa!!! LOL!
   
 3. Gunda66

  Gunda66 JF-Expert Member

  #3
  Oct 4, 2012
  Joined: Mar 8, 2012
  Messages: 508
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 45
  Wazee wa zamani hawakukosea walivyosema "Aliyeshiba hamtambui mwenye njaa", kwa jinsi Tanzania hii huo utajiri unavyopatikana (kukwepa kodi, biashara haramu, ufisadi n.k) wanaona kama wanaokosa ni wanajitakia pasipokujua kwamba wao ni wanyonyaji
  Mtambuzi ni kweli muda mwingine inatubidi tuangalie na kupima kutokana na hali halisi ya jamii inayotuzunguka kwasababu sote ni binadamu na tumeumbwa ili kusaidiana katika matatizo na wakati wa furaha pia,, Huo ndio "UBINADAMU"
   
 4. Blaine

  Blaine JF-Expert Member

  #4
  Oct 4, 2012
  Joined: Jan 11, 2012
  Messages: 2,285
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  kila mbuzi atakula kwa urefu wa kamba yake
   
 5. HorsePower

  HorsePower JF-Expert Member

  #5
  Oct 4, 2012
  Joined: Aug 22, 2008
  Messages: 3,617
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Ubinadamu kazi sana!
   
 6. Root

  Root JF-Expert Member

  #6
  Oct 4, 2012
  Joined: Jan 23, 2012
  Messages: 26,238
  Likes Received: 12,949
  Trophy Points: 280
  Yesu alisema siku za mwisho upendo wa wengi utapoa so sishangai hayo kutokea

  Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
   
 7. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #7
  Oct 4, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  Kila siku tunafundishwa 'to mind our own bussiness' sio?

  sasa nitajuaje kama jirani kalala njaa kama hajaja kuniambia?

  hivi kwa nini mtu awe na njaaa na ashindwe kujishusha na kuomba msaada?


  kwa nini mwenye nacho ndo ajishushe kwenda kumsaidia mtu ambae hasemi?


  na hivi mwenye nacho akitumia chake si ndo anakuwa mteja wa asie nacho?
  na kulipa kodi ya kununua dawa za masikini mahosipitalini?
  au?????
   
 8. Mao ze dong

  Mao ze dong JF-Expert Member

  #8
  Oct 4, 2012
  Joined: Aug 28, 2012
  Messages: 567
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 45
  wote nyie ni wauaji yaani upo tayar kumsindikiza jiran yako akamharibu mtu ilihali ukiwa unamfaham huyo mtu,je akishakuwa kichaa au akifa unafaidika nini
  kweli Mungu atusaidie
   
 9. Mao ze dong

  Mao ze dong JF-Expert Member

  #9
  Oct 4, 2012
  Joined: Aug 28, 2012
  Messages: 567
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 45
  kamwe hauwezi kumtumikia Mungu na mali,(mt 6:24-25)
   
 10. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #10
  Oct 4, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  Define 'kubarikiwa'..
  ukitazama sana kubarikiwa ni kuondokana na umasikini
  watu matajiri unaweza sema 'wamebarikiwa' pia
   
 11. Mao ze dong

  Mao ze dong JF-Expert Member

  #11
  Oct 4, 2012
  Joined: Aug 28, 2012
  Messages: 567
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 45
  Maskini siku zote hana rafiki na anachukiwa
  mithali 14:20,19:4
   
 12. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #12
  Oct 4, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 302
  Trophy Points: 160
  mmh, the fittest will survive
   
 13. Root

  Root JF-Expert Member

  #13
  Oct 4, 2012
  Joined: Jan 23, 2012
  Messages: 26,238
  Likes Received: 12,949
  Trophy Points: 280
  Labda nini kinasababisha hadi hao watu wafikie hapo walipo?

  Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
   
 14. farkhina

  farkhina Platinum Member

  #14
  Oct 4, 2012
  Joined: Mar 14, 2012
  Messages: 12,831
  Likes Received: 775
  Trophy Points: 280
  No comment....

  Sent from my BlackBerry 9100 using JamiiForums
   
 15. Root

  Root JF-Expert Member

  #15
  Oct 4, 2012
  Joined: Jan 23, 2012
  Messages: 26,238
  Likes Received: 12,949
  Trophy Points: 280
  lara 1 punguza hasira bana huyo alikuwa anatania tu

  Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 16. lara 1

  lara 1 JF-Expert Member

  #16
  Oct 4, 2012
  Joined: Jun 10, 2012
  Messages: 15,444
  Likes Received: 10,122
  Trophy Points: 280
  Hahahaaaaa! NANI KANUNA? Nishasema leo NIMENUNA MWENYEWE! Watu wanataka kunipindua kwenye serikali yangu najiona, mchana kweupe Kwanini watu wanacheat thread! Ngoja basi nifute!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 17. Root

  Root JF-Expert Member

  #17
  Oct 4, 2012
  Joined: Jan 23, 2012
  Messages: 26,238
  Likes Received: 12,949
  Trophy Points: 280
  Hasira za BBM haya bana alikuwa anakupima tu kuona kama unaweza yaani ni sawa na vita ya Iran vs Israel kupimana nguvu

  Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
   
 18. Mao ze dong

  Mao ze dong JF-Expert Member

  #18
  Oct 4, 2012
  Joined: Aug 28, 2012
  Messages: 567
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 45
  Nakukatalia coz kila mali inachanzo chake mf uiz,nguvu za giza,uridhi,rushwa,kutapeli nk je hizi nazo ni baraka
   
 19. MadameX

  MadameX JF-Expert Member

  #19
  Oct 8, 2012
  Joined: Dec 27, 2009
  Messages: 7,847
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Kubarikiwa kuna aina nyingi..... kuwa tajiri ni mtihani na sio necessary baraka, maaana matumizi ya hiyo mali nayo ni pasua kichwa. Mali inaweza kufanya ukakufuru na kumkosea mungu ama ikufanye mwenye kuzidi kuwa karibu na mungu kutokana na unavyokumbuka binadamu wenzako.
   
Loading...